UTAWALA BORA NI NINI? - waleo blog

Breaking

Wednesday, 1 April 2020

UTAWALA BORA NI NINI?



#Utawala
Maana ya utawala
Ni mchakato wa  kufanya maamuzi  na namna ambayo maamuzi yanatekelezwa au hayatekelezwi.
 Maana ya utawala bora
Utawala bora ni utaratibu wa utumiaji wa madaraka ya umma, kusimamia rasilimali ya nchi katika jitihada ya kuongeza na kutumia rasilimali hiyo kwa ajili ya kuinua hali ya maisha ya wananchi. Utumiaji huo wa madaraka huandamana na ushirikishaji wa wahusika wote katika kuhakikisha kuwa shughuli za umma zinaendeswa kwa kuzingatia mawazo na maslahi ya wengi,utawala wa sheria,ushirikishwaji wa wananchi, ”Wabunge wetu wanatusimamia”  haki , usawa, uwazi na uwajibikaji.
Misingi ya utawala bora
Demokrasia
Demokrasia ni utaratibu ambao  viongozi wa wananchi hupatikana kwa njia ya uchaguzi, unaoendeshwa  kwa njia ya haki inayompa mwananchi uhuru wa kuchagua kiongozi anayemtaka. Miongoni  mwa taratibu zinazopaswa kufuatwa katika kudumisha demokrasia ya kweli ni pamoja na watu kujijengea utamaduni wa:
§  Uvumilivu na staha kwa mitazamo na maoni tofauti ya kisiasa;
§  Kufuata na kuheshimu mawazo ya walio wengi;
§  Kutumia nguvu ya hoja na siyo hoja ya nguvu;
§  Kupingana bila ya kupigana; na
§  Kujikosoa,kukosoa,kukosolewa na kukosoana bila kuleana .

Shida iliyokubwa leo hii watu hutazama kuhusu utawala bora katika ujumla wake.Vyema tukajitafakari kwanza katika kuijenga hii misingi ya utawala bora kwa kuanza kufanya katika nyumba zetu,kazini,ofisini,shuleni n.k. Mtenzi mmoja anasema,”Hakiki mkono wako pindi uninyoosheyapo kidole kimoja. Na badili yake,vidole vilivyo vingi hukutazama wewe”.Maana yake ni nini? Ikiwa utahitaji kufanyiwa jambo Fulani,jiulize kwanza wewe umelifanyia nini jambo lile?.

Kwa leo nitakomea hapa,usiache kututembelea kwa vitu mbali mbali na vinono.


Tafakuri,maoni na nasaha ni hapa;
                                                                        +255767611645
                                                                        +255715080716
                                                adamgome96@gmail.com
                                                mwanaharakat1992@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Pages