MAJUKUMU MUHIMU YA DIWANI. - waleo blog

Breaking

Wednesday 1 April 2020

MAJUKUMU MUHIMU YA DIWANI.


#UTAWALA

Diwani nchini Tanzania ni mwakilishi wa wananchi wa kata yake, pia ni mwakilishi wa wananchi katika vikao vya baraza la madiwani la halmashauri anayoitumikia (halmashauri ya wilaya/manispaa/jiji/mji) kama ilivyoridhiwa katika sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa ya mwaka 1977 sura No.292-14(1).
Diwani pia ni mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata (ward development committee, WDC) kama ilivyoandikwa katika sheria ya serikali za mitaa No.7(31) ya mwaka 1982, iliyofanyiwa marekebisho na sheria No.6 ya mwaka 1999.


  • Kuwakilisha wananchi katika halmashauri. Diwani huwakilisha wakazi wote wa kata yake hivyo anatakiwa kuwa karibu na wapiga kura wake na kufikisha mbele ya Halmashauri na Kamati zake vipaumbele vya wananchi ili vijadiliwe na kutolewa maamuzi.

  • Kuhamasisha wananchi katika kulipa kodi na ushuru wa Halmashauri.

  •  Kusimamia matumizi ya fedha za halmashauri. Diwani anatakiwa kuhakikisha fedha za halmashauri zinatumiwa kwa  dhumuni/madhumuni yaliyokusudiwa na si vinginevyo.

  • Kuwa kiungo kati ya halmashauri na ngazi za msingi za serikali za mitaa. Diwani ni mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata. Atumie mamlaka hayo kuwasilisha kwenye halmashauri, maamuzi ya kata yake na vile vile kuwasilisha kwenye kata maamuzi ya halmashauri.

  • Kuhamasisha wananchi kuhusu vita dhidi ya umaskini. Katika kulitekeleza hili, ni lazima ajue kwa ufasaha hali ya kiuchumi na kijamii inayowakabili wananchi wake na kushirikiana nao ili kupanga mipango endelevu ya kujikwamua. 

  • Kufuatilia utekelezaji wa mipango yote ya wananchi na ya halmashauri, iIi kutimiza jukumu hili ipasavyo.Diwani anatakiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi yote ndani ya kata yake ambalo ni jimbo lake la uchaguzi bila kudai malipo yoyote toka kwenye halmashauri au wadau wengine. Kimsingi hii ndiyo kazi ambayo diwani aliahidi kuitekeleza wakati wa kampeni.

  •  Kutetea maamuzi ya halmashauri. Wakati wa majadiliano ndani ya Halmashauri, diwani ataelekeza na kutetea maoni yake au ya wakazi wa eneo lake. Hata hivyo, iwapo uamuzi utakaofikiwa na wengi utakuwa kinyume na matarajio yake atalazimika kuunga mkono maamuzi ya wengi yaliyofikiwa kidemokrasia.

  • Kuzingatia misingi yote ya utawala bora wakati wa kutekeleza majukumu yote ya udiwani.
Baada ya kusoma makala hii na kuielewa vyema,jukumu ni lako la kumtathmini(kutafakari/kufikiria) diwani wako kabla ya kumrejesha madarakani kwa mara nyingine.
NYONGEZA:Wakati unamtafakari diwani wako jiulize swali hili,’’Nilisha wahi kumkumbusha diwani wangu juu ya utendaji wake wa kazi?”.ha ha ha ha ha ha ,,,,,.

Maoni na ushauri,maana hakuna mkamilifu….Hapa chini
                                                                                                Mwanaharakati1992@gmail.com
                                                                                                adamgome96@gmail.com
                                                                                                +255767611645
                                                                                                +255715080716

No comments:

Post a Comment

Pages