#UTALII
Kifaru ni
mnyama mwenye nguvu na aliyejengeka na kupambika na pembe moja (1) kubwa iliyo
gawanyika katika pacha mbili (2) usoni mwake.Kuna
aina mbili za kifaru, ambazo ni Kifaru mweupe na Kifaru mweusi.
Maeneo anakopatikana huyo Kifaru mweupe ni
katika nchi ya Uganda na nchi ya Afrika ya kusini(South Africa)/au rasi ya
tumaini jema.Kifaru mweusi nae anapatikana katika nchi ya Tanzania mkoa wa Arusha mbuga ya Serengeti , Ngorongoro na pia nchini Kenya.
Uhai wake. Wataalamu wa wanyama pori waliweza
kumchunguza mnyama huyu kifaru na
kubaini kuwa, kifaru anauwezo wa kuishi ndani ya miaka 40—50 kutokana na
mazingira anayoyapitia.
Kifaru anashika ujauzito ndani ya miezi 15—18, na dume
la kifaru ni kubwa kuliko jike.Chakula kikuu cha kifaru ni majani na hula
chakula hicho nyakati za asubuhi na jioni.
Kifaru aliyekamilika katika
ukubwa wake ana kilo 1000-1500.Lakini pia Kifaru ni moja kati ya wanyama watano[5] wakali duniani,
yaani (big five) hapa tunamaanisha uwepo wa Tembo, Simba, Chui na Nyati.
Ulinzi na upambanaji, Kifaru hutumia pembe yake kupambana na
Simba pindi anapotaka kuwadhuru
watotowe, na wakati mwingine hutumia kupigana wao kwa wao.Kifaru hutumia mkia wake kuukojolea na kumwagia binadamu
pindi atakapo panda juu ya mti, palee alipo taka kumfanyia uhalifu.
Adui mkubwa, tena mkubwa asiye na haya wala huruma kwa
mnyama Kifaru ni, mimi mwandishi wa
makala na msomaji wa makala
hii(binadamu) na wakati mwingine Simba huwinda watoto wa Kifaru.
‘’ Hakika
mkamilifu ni mungu pekee kama vile yesu alivyosema ndani ya Bibilia,’’Hakuna aliyemkamilifu yule ambaye
ametoka katika tumbo la mama yake’’.
Swali la mwandishi kwenu. Tumemkosea nini Kifaru mpaka
sisi binadamu ndio tunakuwa adui yake mkuu?.Tuacheni tabia hii’’.
Huyu ndiye kifaru kwa uchache..
Usisahau kufolo,maoni
na ushauri katika makala na habari mbali
mbali
Kwa huduma ya
utalii, usisahau kututazama hapa,
Malamboaziz14@gmail.com/0717475992/0782080716
No comments:
Post a Comment