HAYA NDIYO MATUMIZI SAHIHI YASIMU. - waleo blog

Breaking

Wednesday 25 March 2020

HAYA NDIYO MATUMIZI SAHIHI YASIMU.


#Uungwana

Rununu/simu ni moja ya kifaa cha mawasiliano kilichotengenezwa kiteknolojia,ambacho humsaidia binadamu katika shughuli zake.
Teknolojia hii imeleta mapinduzi makubwa sana ya kiuchumi na kijamii katika dunia tulio nayo hivi sasa.Mbali na teknolojia hiyo ya simu kuwa na athari kubwa,wapo baadhi ya watu katika sisi hawajayafahamu ama hufanya makusudi kwa kutotumia matumizi sahihi ya simu.Matumizi sahihi ya simu huweza kukuacha huru na mambo yako,ama kukutia matatizoni endapo huto yatendea haki.Leo makalani endapo Mungu akijaalia, natata niwaletee matumizi ya simu yafaayo na yasiyofaa.

Kuzungumza na simu wakati wa kula chakula;kitendo hiki sio kizuri sana na hakifai kiafya,maana huenda kikakusababishia kupaliwa na baadaye kikakupelekea R.I.P.Tuache na tubadilike.

Kutazama tupu/uchi zisizo halali kwako;wapo baadhi ya watu, hupenda tu kupakua na kutazama video na picha za ngono.Tabia hii imekatazwa na  dini zote kuu na hukumu yako ni jahhanamu ukifa katika hali hii..Najua utaguna wewe ambaye huamini katika dhahania,waache waamino,watafakari na kuridhika wafaidike.”badilika”

 Kusikiliza muziki wenye sauti ya juu kwenye mambo ya kijamii,mfano kwenye daladala’mikutanoni n.k.Baadhi ya watu huipenda sana tabia hii.Wambieni si katika matumizi sahihi ya simu.

Kutojibu ujumbe mfupi(sms) na kupuuzia simu zilizo kuita yaani missed call;miongoni mwetu huwa na tabia hii mbali na uchumi yaani kukosa salio ama simu ya mdeni wako.kiukweli wapo baadhi ya watu hujifanya ya kuwa wameendelea, punde ambapo rafiki/ndugu yake amtafutapo kwa kumpigia simu na hatimae kuitazama tu simu iitapo na mbali zaidi kuikata na kusema,’’ah! Huyu nae msumbufu”. Haya nayo kwa mujibu wa watengeneza hizo simu,wanasema kwamba si katika matumizi sahihi ya simu/rununu, yaani ni ulimbukeni/ushamba..Badilika wewe blaza meni na sista duu,kama ulikuwa unajua ni ujanja sasa wenye simu zao wamekuumbua.”Ha haa haaaaaaaaaa,,,.”.Usahihi wake ni huu hapa,kama anakudai wewe pokea na umpe faraja kwa upole juu  ya anachokudai.Kama ni ndugu yako na namba zako hukutaka azifahamu na humuitajii basi mpokee na umwambie,’’sitaki unisumbue sumbue na namba zangu uzifute,maana umezidi kuniomba omba pesa’’,tena unikome’’. Nafikiri kwa majibu haya,akikutafuta tena!!! Sijui atakuwa na akili gani…Kama ni mkeo/mpenzi wako umemchoka , basi ni bora upokee simu yake na umwambie ukweli, kuliko kuwa limbukeni wa kutopokea simu na kupuuza missed call.
Kuongea na simu msalani.
Kuongea kwa sauti ya juu na kuwakera watu.
Kuwalazimisha watu katika ujumbe/hadithi uzisomazo,wakufuatilie.
Kwa leo na weka kidau cha wino chini nitafanya upelelezi wangu baada ya ukumbusho na elimu hii.
Kwa lolote lile lihusulo makala zetu,katika maoni na ushauri.
Usisite hapa;;;;                      adamgome23@gmail.com
                                                 Mwanaharakati1992@gmail.com
                                                +255767611645
                                                0715080716

No comments:

Post a Comment

Pages