#ELIMIKA
Ramli/bao ni kitendo cha kupandisha majini kichwani(pepo),kuchora
michoro
fulani fulani ima chini ya arthini ama karatasini kwa lengo la kugundua majambo
yaliyofichikana na yajayo.Mambo haya hufanywa
na waganga wa kishirikina(wachawi).
Kwa wale waishio kupitia mapokeo ya dini kuu mbili duniani yaani Uislamu na
Ukristo majibu kuhusu
ramli ni kama ifuatavyo.
BIBILIA
INASEMAJE.
Hali ya kupiga ramli imekatazwa na Mungu.
Imeandikwa katika Kumbukumbu la torati 18:9-13 "Utakapo
kwisha ingia katika nchi akupayo Bwana Mungu wako, usijifunze kutenda kwa mfano wa
machukizo ya mataifa yale na asionekane mtu yeyote ampitishaye mwanawe au binti
yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao
wala mtu atazamaye nyakati mbaya
wala mwenye kubashiri wala mtu alogaye kwa kupiga
mafundo wala mtu apandishaye pepo wala mchawi wala mtu aombaye wafu
kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo,
Bwana Mungu wako anawafukuza mbele yako."
Mungu ndiye ajuaye mambo yajayo. Imeandikwa, Isaya 8:19 "Na wakati
watakapokuambia tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi
walio na ndege na kunong,
ona je! haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je waende
kwa watu walio kufa
kwa ajili ya watu walio hai?."
UISLAMU UNASEMAJE NAO.
Aina zote za hawa watu ni sawa ikiwa ni mtabiri wa nyota,
kusoma viganja au
kupiga ramli na zote hizi zimekatazwa.Mwenyezi Mungu Anasema:
“Enyi Mlioamini! Bila shaka ulevi, na kamari, na
kuabudu masanamu, na kupiga ramli ni uchafu katika kazi za shetani. Basi
jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa” (5:
90).
Na Mtume Muhammad (S.a.w) amekataza
jambo hilo, hivyo inatakiwa tujiweke kando kabisa.
Mambo yote haya ni haramu na yeyote mwenye
kuamini kuwa jambo fulani limetokea kwa sababu ya
nyota kadhaa na kadhaa amemkanusha
Allaah kama Alivyosema katika hadithi ifuatayo:
(Yeyote atakaye jimai (kufanya kitendo cha ndoa) na mwanamke
mwenye hedhi, au kwa kutumia njia ya nyuma(kulawiti), au kumkaribia mtabiri na kuamini aliyoambiwa, basi amekufuru yale
aliyoteremshiwa Muhammad).
[Hadithi Sahihi, imesimuliwa na Mus-habu-Sunnan
na wengineo]
Na kufanya hivyo ni kuingia katika elimu ya ghaybu
(mambo yaliyofichika ya Allaah) ambayo hakuna aijuwae ila Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala) na humpeleka mtu kuingia katika shirki. Na Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala) humghufuria mtu dhambi zote ila shirki kama Alivyosema:
"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi
kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na
anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa"
[An-Nisaa: 48
Nasaha zetu ni kuwa tumuamini Allaah na nguzo
zilizobakia za Imani kama Qadar, hivyi tutaondokana na matatizo ya
kumkufuru Allaah kwa kwenda kuangaliliwa na hawa wapiga bao,
ramli na wengineo.
Hiyo ndio ramli na makatazo yake, pande kuu mbili
za dini zenye wafuasi wengi duniani.
Usikae mbali nasi zingine zafuata……..
Usisite
kwa maoni na lolote lile lihusulo sisi na tukifanyacho.
+255767611645
+255715080716
Mwanaharakati1992@gmail.com
No comments:
Post a Comment