Kiufupi,
wakati huu ushindani ulikuwa mkubwa sana na wanamuziki au waimbaji wengi
walihama kutoka bendi moja kwenda nyingine hasa kwa kufuatia utitiri wa mabendi
ya muziki wa dansi nchini. Kipindi hiki ndicho alichokuja mkali wa sauti nchini
Tanzania King of Melody (Christian Bella) akitokea nchini jamhuri ya kidemokrasia
ya Kongo. Kipindi hiki ndicho kilichounda
bendi ya Wajelajela Original (Stono Musical), baadaye FM Academia chini
ya ungozi wake Nyoshi
El Sadat. Hii FM Academy ilikuwa moja na Stono Musica kabla ya
kutengana na Nyoshi akabaki na jina halisi lakini kaongeza neno kama "The
Dream Team". Zama hizi wanamuziki vijana wa kikongo walifurika hasa kuja
nchini Tanzania.
Kwa
upande wa muziki wa kizazi kipya, ukiacha wale walioanza kabla ya 2000, hapa
anakuja Dully Sykes, Manzese Crew, Wandava Creek, Wehu Kumi Ngangari (W TEN
N), TID, Jay Moe, Ngwair, Daz Nundaz, Madee, Mandojo na Domo
Kaya, Mr. Blue, Complex, Dudu Baya, Juma Nature na FSG, A.Y., G.K., Q Chillah, MwanaFA, Lady Jay Dee na Ray C. Jay Dee ndiye msanii wa kwanza kurekodi albamu yenye
gharama kubwa mno kuliko zote tangu kuanza kwa muziki wa kizazi kipya. Kwa
kipindi kile cha mwanzoni mwa miaka ya 2000,ndiye aliyeanza kupiga video na Benchmark Production kwa kipindi
haikuwa rahisi sana kufanya kazi na kampuni hiyo. Jay Dee na A.Y. ni wasanii wa
mwanzo kabisa kuthubutu kutoka nje ya mipaka ya Tanzania katika kufanya muziki
na wasanii wa nchi za nje.
Hili
halijawahi kufanywa hapo awali na wasaniii wowote wa kizazi kipya isipokuwa
wawili hawa. Ray C, ni moja kati ya wasanii wa Bongo flava walioweza kufanya
vizuri, lakini nae anasa za maisha zilimfanya kufuta urithi wake wote katika
muziki. Haonekani tena thamani yake hasa kwa kujihusisha na matumizi ya dawa za
kulevya. Kulikuwa na makundi yaliyoingia na kutoka. Aidha kwa kukosa udhamini
au kujitangaza vya kutosha. Kundi kama Boyz from the Army, Born Crew, Hot Grils, Big Dog Pose (BDP), Hot Port Family, Wateule, Mambo Poa,
Uswahilini Matola, na wengine wengi waliingia na muda mchache
hawajafua dafu wakapotea jumla. Sehemu ya kikosi cha wanamuziki waliokuwa
wanajiita New Jack Family,
watoto wa Kariakoo. Nao walizingua sana katika tasnia ya muziki wa kizazi
kipya. Hasa kwa msanii wao Dully Sykes. Kundi kama G.W.M. baadaye likaja kuwa sehemu ya Wachuja
Nafaka huku kukiwa na ongezeko la Juma Nature na
Doro.
Wachuja
Nafaka lilikuwa kundi la mradi tu (super group) lililodumu muda mchache tu.
Wasanii wengine waliotamba katika 2001/2002/2003/2004 ni pamoja Zahrani a.k.a
Big Punisher wa Bongo, Spulla, Bushoke,
Mr. Nice ambaye kiukweli alitamba kupita
maelezo na nyimbo za kuchukua hala za kitoto na kuzirudia katika mtindo wa
Bongo Flava aliotamba nao kwa jina la TAKEU.Aliupeleka muziki wa kitanzania mbali sana, hasa katika
nchi za Burundi, Rwanda, Kongo na nchi zingine za Afrika.Ubaya ulioje!? hakudumu sana, hasa kwa kuendekeza anasa za
maisha na kuepelekea kuanguka mazima katika fani ya muziki. Buibui, Mpaki, Nurueli, Bab Lee, Snoop Lee, Man X na wengine wengi.
Professor Jay katika
upande wa wasanii wa kiume, alionekana kuunyanyasa sana muziki wa kizazi kipya
katika miaka ya 2001-2005. Zama hizi Professor Jay alionekana kutokuwa na
mpinzani, inasemekana yeye ndiye aliyesababisha wazee wasikilize muziki wa
kizazi kipya. Ilikuwa mwaka 2000 na kibao chao cha Chemsha Bongo ambamo maneno
mazito aliyoongea humo yalipelekea wazee wengi kusikiliza muziki huu. Kabla ya
2000, wazee wengi waliona muziki wa kizazi kipya ni kama uhuni tu. Huenda
Professor Jay ndiye aliyevutia vijana wengi kuingia katika muziki kama jinsi
ilivyo kwa siasa, Zitto Kabwe kuvutia
vijana wengi kujiunga na siasa.
Huwezi
kutaja muziki wa kizazi kipya bila Prof. Jay. Mb Doggy ndiye
mwanzilishi wa muziki wa mapenzi mazito, hata kama awali waliimba, lakini si
kwa kiwango cha Mb Doggy. Mwaka 2005-2006 ilikuwa ni kipindi chake cha
kuunyanyasa muziki wa kizazi kipya. Mb Doggy kutoka Tip Top Connection alionesha
uwezo wake mkubwa sana katika tasnia hii. Miaka hii ya 2005-2006 Ferouz nae
alikuja juu sana. Lakini hakwenda mbali.
Ni
miaka hii, alipokuja Matonya, Abby Skills, Enika, Ali Kiba, Queen Darleen
ijapokuwa alikuwepo tangu enzi za historia ya Kweli ya Dully Sykes, lakini
hakuwa msanii kama msanii mpaka kipindi hiki. Kipindi hiki muziki wa taarab
ulipamba moto. Mwaka wa 2006, Jahazi
Modern Taarab ilianzishwa chini ya uongozi wake Mzee
Yusuph.
Mzee Yusuph aliufikisha mbali sana muziki huo, alisababisha kila mtu asikilize
taarab hasa kwa tungo zake. Baadaye zikazuka bendi nyingine nyingi tu za
taarab.
Katika
miaka ya 2010.
Katika
kipindi hiki, muziki wa kizazi kipya na muziki wa dansi ulibadilka sana. Vijana
wengi walikuja katika muziki wa dansi. Lakini Bongo flava imepiga hatua
maradufu. Msanii kama Diamond Platnumz ameupeleka mbali muziki wa Tanzania nje ya nchi kwa
kiasi kikubwa kupita msanii yeyote yule tangu muziki huu ulipoanza. Katika
kipindi hiki, rundo la wasaniii wa muziki wa Bongo flava walibatizwa kama
wabana pua, waliongezeka na kuigana kupita kiasi. Watayarishaji wa muziki huu
waliongeza maradufu. Bongo flava, ilianza kuchukua miundo mbalimbali ya miziki
mingine kama vile Kwaito, Zouk Rhumba, Singeli, Raggae, muziki
wa Nigeria hasa waliiga na kadhalika. Na ndicho kipindi
kilichoanza na ushamba katika muziki, hasa kwa kuanzisha makundi maarufu kama team
kati ya msanii na msanii.
Lakini
timu zilizokuwa na ushandani mkubwa ni za Ali
Kiba na Diamond. Kipindi hiki
ndicho walichovuma akina Ben Pol,
Top C., Bob Junior, Darassa, One
Incredible, Nikki
Mbishi, Nikki
wa Pili, Geez
Mabovu, Baraka da Prince, Galatone
Tena, Samir, Belle
9, Kassim
Mganga, Nuh
Mziwanda, Z.
Anthony, Dullayo, Sam
wa Kweli, Barnaba, Marlaw, Izzo
Business, Mabeste, Linah, Gosby, Godzilla na wengine wengi tu. WCB lebo ya muziki iliyozalisha wasanii wapya kama Harmonize, Rayvanny. Vile imechukua wasanii wengine
maarufu kama Richie Mavoko. Kwa pamoja wameweza kuutingisha muziki wa kizazi kipya kwa
mwaka wa 2015/2016. Vilevile kuanzia
Agosti 2015, Darassa ameonekana kuutawala muziki wa kizazi kipya kwa kiasi
kikubwa sana. Hasa kufuatia yeye anafanya hip-hop. Huenda Darassa ni msanii
pekee wa hip-hop aliyeweza kufikisha watazamaji wengi kwa muda mfupi
katika Youtube kuliko msanii yeyote yule wa hip-hop wa kitanzania
hasa kwa kufuatia kibao chake cha Maisha na Muziki na Too Much kilichotoka Julai 15 na Muziki Novemba 23,
2016. Vilevile kipindi hiki ndicho kulipozaliwa muziki wa Singeli.
Wanamuziki maarufu wa Singeli ni pamoja na Man
Fongo, Msaga
Sumu, Sholo
Mwamba na wengine wengi.
Haya
bwana, huo ndio muziki wa Tanzania na asili ya muziki kiujumla
Sambaza
kwa wengine waujue/wakumbuke.
Maoni,ushauri
hapa.
0767611645
+255715080716
No comments:
Post a Comment