UALBINO/ZERUZERU NA SABABU ZAKE. - waleo blog

Breaking

Wednesday 25 March 2020

UALBINO/ZERUZERU NA SABABU ZAKE.


#BIN-ADAM

Zeruzeru kwa Kizaramo / Kizigua  huitwa zeu,yaani nyeupe au Albino kwa Kilatini  albus, yaani mweupe.
Maana Ni mtu anayekosa pigmenti ya melanini katika ngozinywele  na macho.
Waathiriwa wenyewe nchini Tanzania waliamua kuitwa watu wenye ualbino kutokana na matumizi mabaya ya neno zeruzeru katika utamaduni wa Afrika ya Mashariki ambako watu mara nyingi waliona uhusiano kati ya waathiriwa na mapepo.
Asili
Albino huzaliwa na hali ya kukosa uwezo wa kujenga pigmenti ya melanini ambayo ni muhimu kama kinga dhidi ya mnururisho/mwanga wa jua. Watu wenye ualbino huwa na nywele nyeupe au njano, na ngozi nyeupenyeupe. Macho yao ni buluu au hata pinki.

Uwezo wa kujenga melanini mwilini hutawaliwa na jeni fulani. Kama jeni zote inapatikana kwa jozi katika kromosomu za seli. Hali inatokea baada ya kwamba jeni moja katika jozi hii ni bovu. Tabia hii ni dhaifu, yaani jeni 1 nzima inatosha kuendelea na kutengeneza melanini. Lakini jeni zote mbili zinaingia katika urithi wa watoto wakati wa kuzaa. Mtu huzaliwa na ualbino, ni hali ya kurithiwa kama wazazi wote wawili wana jeni inayoruhusu ualbino. Hii inawezekana hata kama wazazi wote wawili hawaonyeshi dalili za ualbino wenyewe. Tabia hii inaendelea katika familia na inaweza kuonekana mara kwa mara au baada ya kizazi tu. Inategemea na kupatikana kwa jeni husika katika wazazi wote wawili.
Maana yake urithi wa ualbino unaweza kuendelea katika familia kwa vizazi kadhaa bila mtoto kutokea vile. Lakini pale ambako mume na mke wenye rangi ya kawaida walio na jeni hii wanazaa pamoja watoto wanaweza kutokea albino. Kijenitiki ualbino ni tabia dhaifu na kufuatana na sheria ya Gregor Mendel inatokea kwa wastani kwa mtoto mmoja kati ya watoto wanne.

Ualbino mara nyingi huitwa ugonjwa ingawa hii inategemea jinsi ya kufafanua.
Albino huzaliwa na hali ya pekee inayoweza kupunguza uwezo wake wa kuona vizuri lakini hii si lazima. Yuko hatarini ya kuchomwa kwenye ngozi na kupata magonjwa kutokana na athari ya nuru ya jua. Hali yake haiongezeki maishani mwake isipokuwa kama hali yake inasababisha uonjwa kutokea.
Ualbino huo unaweza kuathiri watu wa kila rangi lakini kwa sababu zisizoeleweka bado unapatikana Afrika Mashariki zaidi kuliko sehemu nyingine za dunia. Kwa mfano, nchini Tanzania kuna albino 1 kwa wakazi 1,400, kumbe wastani wa kimataifa ni 1 kwa 20,000.
Watu wanaoathiriwa sana na ualbino mara nyingi huwa na matatizo ya macho, pia wako katika hatari ya kubabuka kwa jua na kupata kansa ya ngozi.

Angalizo
Tukiacha matatizo ya macho na hatari ya kansa ya ngozi, albino ni mtu wa kawaida hana afya mbaya lakini anapaswa kujihadhari asikae kwenye jua muda mrefu bila kinga.

Pengine katika jamii kuna watu wenye maono mabaya dhidi ya wazeruzeru. Kuna imani potovu, hasa katika sehemu za Afrika (ambako albino anaonekana sana kuliko sehemu nyingine za dunia ambako watu wengi huwa na ngozi nyeupe kiasi) ya kwamba miili ya albino huwa na nguvu ya uchawi. Imani hiyo ilisababisha mauaji ya maalbino kwa kusudi la kutumia sehemu za miili yao kwa uchawi. Nchini Tanzania katika miaka 2000-2015 walau watu 75 waliuawa hivyo.

Imani hizo hazifai na tuepuke kwa yule ambaye amekuumba wewe ukawa si mlemavu wa ngozi na aliye muumba mlemavu huyo wa ngozi.Uchawi haufai na unaangamuza kwa Mungu,kama tulivyoona katika makala ya asili ya uchawi ndani ya tovuti hii. MWENYEZI MUNGU UTULINDE NA MABALAAA NA MAJANGA,,,,,,.

Maoni na ushauri ni hapa..
                                                          +255767611645
                                                          +255715080716
                                                          Adamgome96@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Pages