#Utalii
Bundi
ni ndege mbuai wa familia Tytonidae na jenasi mbalimbali ya familia Strigidae. Leo tutaitazama familia ya Strigidae.Kizazi hiki kinaainishwa
katika nusu familia na
jenasi moja ya nusu familia Striginae.
Bundi
hawa wana kichwa kikubwa chenye umbo la mviringo, mkia mfupi na rangi ya kamafleji. Kwa
kawaida jike ni mkubwa kuliko dume. Mabawa yao ni marefu na mapana. Hula ndege na wanyama wadogo wadogo,hasa
wagugunaji. lakini watambaaji na wadudu wakubwa pia. Jike huyataga mayai 2-7 katika
tundu la mti au tago lililoachwa na
ndege mwingine na pengine katika sanduku la kutagia.
Bundi
wengi huwinda usiku na hupumzika mchana. Manyoya ya uso yapeleka mawimbi sauti kwa vipenyo vya masikio ambavyo kimoja kipo juu
kidogo kuliko kingine. Hivyo wanaweza kumkamata mbuawa bila kumwona. Mbuawa
hawezi kumsikia bundi akija, kwa sababu mabawa ya bundi hayafanyi sauti yo yote
kwa kuwa kingo ya mbele ya manyoya ya mabawa yamekerezeka kerezeka na lile ya
nyuma lina matamvua. Hii inapunguza vurugu ya hewa na kwa uvumi.
Baadhi
ya jamii chache zimekuwa zikihusisha bundi na ushirikina ama uchawi, hivyo kutia wengi mashaka, hasa wanaposikia sauti ya ndege huyo nyakati za usiku.
Usiogope wala kuhuzunika pindipo usikiapo mlio
wa bundi usiku,bali yakupasa kufahamu ya kuwa ni hali yake ya kawaida kama
ilivyo kwa wanyama wengine wakiwa wanatoa mlio,mfano mbuzi,ng’ombe n.k.Utofauti
wa bundi ni kulia usiku na mapokeo ambayo tuliyapokea kwa babu zetu kuwa ni
uchuro.
Usomapo
makala hii,ninaamini utakuwa mwalimu kwa wengine wa kuwaondoa hofu..
Usisite
kutunasihi pale tutelezapo, kwa maana mkamilifu ni MUngu pekee..
Ushauri
na maoni,,,,
+255767611645
+255715080716
Adamgome96@gmail.com
No comments:
Post a Comment