SIFA KUU ZA MWALIMU BORA. - waleo blog

Breaking

Wednesday 25 March 2020

SIFA KUU ZA MWALIMU BORA.


#WITO

Mwalimu,kiasili ya neno hili ni ELIMU,,,il-mu kwa kiarabu na kufanyiwa unyambulishaji na kupatikana neno MUA-LIM/MAALIM/AALIM na ndio tukapata kwautohoaji wa neno mwalimu kwa Kiswahili,  kwa Kiingereza teacher, school teacher na pengine educator, ni mtu anayesaidia wengine kupata ujuzimaarifa na tunu.
Kazi hiyo inaweza kufanywa na yeyote katika nafasi maalumu, kwa mfano mzazi au ndugu akimfundisha mtoto nyumbani, lakini kwa wengine ndiyo njia ya kupata riziki inayomdai karibu kila siku kwa miaka mingi, kwa mfano shuleni. Huko mwalimu anatakiwa kuwa na shahada au stashahada, kadiri ya sheria za nchi na ya ngazi ya elimu inayotolewa.
Majukumu ya mwalimu yanaweza kutofautiana kadiri ya utamaduni husika.
Mara nyingi ni pamoja na kufundisha kusoma na kuandika, kuhesabu, kufanya kazi fulani ya mikono, kushirikiana katika jamii, kufuata dini na kuunda kazi za sanaa.

Kwa kawaida ufundishaji huo unadai mwalimu aandae somo kwa kufuata mtaala fulani, kutoa vipindi na kutathmini maendeleo ya mwanafunzi. Pia ni muhimu atunze nidhamu.
Nje ya madarasa, pengine mwalimu anatakiwa kuongoza wanafunzi wake katika safari za kutembelea mashambaviwandakumbimakumbusho, n.k.
SIFA KUU ZA MWALIMU BORA
Ualimu si kazi ngumu sana, kwa sababu unahusika na mambo mengi.
Umoja wa Ulaya umetaja sifa tatu muhimu:
Uwezo wa kushirikiana na wengine
Uwezo wa kutumia ujuzi, teknolojia, habari, na
Uwezo wa kufanya kazi ndani na pamoja na jamii.
Wataalamu wa sayansi ya elimu wanazidi kukubaliana kwamba mwalimu yeyote anahitaji mambo matatu:
Ujuzi yaani kufahamu mada na namna ya kuifundisha, mtaala, sayansi ya elimu, saikolojia, tathmini n.k.
vipaji yaani kupanga kipindi, kutumia vifaa, kuongoza wanafunzi, kuendesha makundi, kutathmini maendeleo na
misimamo yaani tunu, tabiaimani na uwajibikaji.

Ikiwa walimu ndio wazazi wa upili ambao huchukua nafasi kubwa ya muda wa kuwalea watoto,ndugu na wadogo wetu kimaadili mbalimbali.Je tunazifahamu changamoto za walimu wetu, ama ndio tumebakia katika kuwalaumu tu pindi watoto wetu wanapokosea na kumomonyoka kimaadili!!?. Kama mzazi sasa chukua hatua kwa kuwatembelea walimu sehemu zao za kazi na kupata mawili ma3…



Ushauri hapa dondosha..
                      adamgome96@gmail.com
                                        +255715080716
                                        +255767611645

No comments:

Post a Comment

Pages