#Burudani
Muziki wa Tanzania ni
jina la muziki wenye asili ya Tanzania ya leo. Kama ilivyokuwa kwa binadamu wengine, wakazi wa eneo ambalo limekuwa nchi ya
Tanzania, walikuwa na utamaduni wao. Utamaduni huu ulikuwa ukitofautiana kati ya kabila na kabila. Moja ya vipengele ilikuwa muziki. Kiasili,
hatukuwa na muziki katika makabila yetu
kabla ya ujio wa wageni, na hivyo hakuna kabila lenye tafsiri ya neno muziki.
Lakini
tuliimba, tulicheza ngoma,
tulipiga vyombo mbalimbali, ila tulikuwa na utamaduni mwingine kuhusu kitu hiki
tunachokiita siku hizi muziki. Watafiti wanatuambia tulikuwa na ngoma, ambayo
tafsiri yake ni kubwa kuliko muziki.
Ngoma
ilikuwa ni chombo kile kilichotoa muziki, ngoma ilikuwa shughuli yenyewe, kwa
mfano ngoma ya mavuno,
ngoma ya mashetani
na kadhalika, na pia tulicheza ngoma. Pamoja na kukosekana kwa maandiko yenye
kina kuhusu hali ya ngoma katika kipindi hicho lakini tunajua watu waliimba na
kucheza ngoma kwa matukio mbalimbali, hali ambayo inaendelea mpaka leo.
Wajerumani ndio waliotuletea neno muziki, na katika wakati wao wa
utawala ndipo kuliingia muziki wa bendi za askari na kuingizwa katika
shule ya kwanza ya serikali wakati huo na Tanga School
ni moja wapo. Katika kipindi hiki pia mchango wa madhehebu mbalimbali kuingiza muziki
na vyombo vya muziki vipya ulitoa mchango katika kuongeza kasi ya huu muziki
mpya.
Pengine
unaweza ukasema kuwa, kipindi hiki kwaya nazo zilianza kushika kasi, hapa
unaona kama neno kwaya pia ni jipya lililotokana na neno la Kiingereza choir. Historia inatueleza kuwa Mjerumani
hakufanya jitihada za kuzuia muziki wa kiasili, hivyo basi muziki mpya na wa
kiasili ulienda sambamba.
Mwingereza alileta mabadiliko mengi katika muziki wanchi hii. Askari
waliotoka vitani KAR maarufu kama askari kea walirudi na hadithi kuhusu muziki, vyombo vya muziki,
na hata muziki walioukuta katika safari zao vitani, vyombo kama akodian
na magitaa
makavu yaani, yasiyotumia
umeme yaliingia wakati huu. Kutokana na watu wa makabila mbalimbali
kuchanganyika na miji kuanza kuzaliwa kukaanza kuweko na utamaduni mpya.
Muziki
uliyokuwa unakubalika kwa makabila yote ulianza. Aina ya muziki maarufu kama Beni
ilienea katika ukanda mzima wa Afrika
Mashariki. Waafrika waliokuwa wamesoma nao
wakaanza kuwaiga Wazungu hata kuanza kuteengeneza Club zao ambazo zilikuwa maarufu
kama Dancing Clubs. Katika club hizi
kulipigwa nyimbo mbalimbali kwa kutumia santuri na wapenzi kucheza muziki
katika staili mbalimbali kama vile Cha cha, Tango, Foxtrot, swing, waltz n.k.
Inasemekana
clabu ya kwanza Tanzanyika ilianza Tanga, ikiitwa Young Noverty Dancing Club, na baadaye Dar es Salaam ikawa
na Young Generation Dancing Club. Club hizi zilikuwa ndio chanzo cha bendi
za kwanza Dar es Salaam Social Orchestra ambayo baadaye ilikuja kuwa
bendi maarufu Dar es Salaam Jazz Band, na pia kulikuweko na YMCA
Social Orchestra,
wakati huu ilikuwa katika kipindi cha kati ya 1920 na 1935. Baada ya vita ya pili ya dunia
1945, Wamarekani waliweka radio yenye nguvu
katika mji unaoitwa sasa Kinshasa, redio hii iliweza kusikika sehemu
nyingi, Afrika mashariki, Kati na Magharibi. Kuanza kwa lebo maarufu ya Loningisa
nchini Kongo mwaka 1947 ilianzisha kusikika na kuigwa kwa muziki wa
Kikongo kuanzia wakati huo.
Lebo
ya Galotone
ya Afrika
Kusini pia ilisambaza santuri ambazo
ziliingiza staili za Jive katika nchi hii na kwa miaka mingi vijana walikuwa na
vikundi wakicheza jive, na bendi kadhaa ziliiga upigaji wa jive ukiambatana na
upigaji wa filimbi kumuiga mwanamuziki Spokes Mashiyane. Magitaa ya umeme kwa bendi za muziki wa dansi yalianza
kutumiwa kati ya mwaka 1957 na 1959, Dar Jazz tena hutajwa kama bendi
ya kwanza ya muziki wa dansi kuanza kutumia gitaa hilo, ikifuatiwa na Western
Jazz na bendi nyinginezo.
Kwenye
mwaka 1954 Kenya ikaanza kuwa kituo kikubwa cha kurekodi muziki, na kwa
miaka mingi iliyofuata bendi za Afrika Mashariki zililazimika kwenda Kenya ili
kutoa santuri. Kuna wanamuziki wengine mpaka leo hufikiriwa ni Wakenya au
nyimbo zao kudhaniwa kuwa zilitoka Kenya kwa mfano Frank Humplink na dada zake
ambao walitoa vibao ambavyo bado vinasikika katika anga za muziki hadi leo, embe dodo, tufurahi tarusi n.k
Pamoja
na mapungufu yanayotajwa ya utawala wa chama kimoja, kulikuweko na mambo
yaliyowezekana kutokana na hali ya chama kimoja kuwa na dira inayoeleweka na
hivyo kuelekeza kila kitu kadri ya matakwa ya chama. Sanaa ya Tanzania haikukwepa mwongozo wa TANU, sehemu za kazi , vijiji , miji viliagizwa kuwa na vikundi
vya utamaduni ambavyo vingekuwa ndio
vikundi vya burudani baada ya kazi na pia jukwaa la kuelezea mipango na malengo
ya chama na serikali. Zikatengenezwa bendi za majeshi, polisi, JWTZ,
Magereza, Uhamiaji, mashirika ya umma nayo hayakuwa
nyuma, BIMA, TANCUT, DDC
Mlimani, UDA na miji nayo ikawa na bendi Kurugenzi Arusha Kurugenzi
Dodoma. Na ni ukweli usiopingika nyimbo nyingi maarufu kama zilipendwa
zilipatikana katika kipindi hiki.
Bendi
zilitunga nyimbo, ambazo zilipitia katika kamati iliyozipitia kabla ya kuruhusiwa kurekodiwa na kurushwa hewani. Kwa
upande wake serikali nayo ikatengeneza idhaa/chanel tatu katika redio ya taifa,
External Service, iliyokuwa ikitangaza kwa lugha ya Kiingereza na lugha ya nchi
za kusini zilizokuwa zikipigania uhuru wakati huo, kukaweko na Idhaa ya biashara
ambayo ilikuwa na vipindi vikitangaza biashara mbalimbali vilivyodhaminiwa na
wafanya biashara. Katika idhaa hii, uliweza kusikia muziki kutoka popote
duniani, lakini kwa makusudi kabisa kukaweko na idhaa ya taifa ambako huku
ungesikia kila aina ya muziki wanchi hii, pamoja na kuwa kwa sasa kuna vituo
vya radio zaidi ya 80 vimeshindwa kufanya kazi hii iliyoweza kufanywa
na kituo kimoja cha taifa.Ubaya ulioje,
kituo hicho cha taifa kimeshapoteza muelekeo wake uliokuweko awali.
Katika
miaka ya mwanzoni ya 1960, bendi ziliingia katika utamaduni wa
kunakili nyimbo kutoka Kongo na kuimba Kiswahili tu. Kuna nyimbo kama napenda
nipate lau nafasi, mtoto wacha
kupiga mayowe na nyingi sana ambazo zilikuwa ni za kunakili moja
kwa moja nyimbo za Kongo. Hali ilifikia kuwa mbaya mpaka bendi nyingine
ziliingilia kati na kutunga nyimbo za kuwaasa wenzao watunge nyimbo zao.mfano;Koma koma koma kaka wewe tunga zako. ilikuwa baadhi
ya maneno ya kuwafanya wanamuziki waliokuwa wakiiga waache kuiga.
Lakini
pamoja na haya kulikuweko na wanamuziki waliokuwa wakiangalia na kuiga nyayo
kutoka nchi za magharibi na baadaye wakichanganya vyombo na melodi za kiasili
na kuanza muziki uliojulikana kama Afro Rock, na kuwa sambamba na nchi nyingine katika Afrika.
Katika kipindi hiki mwanasiasa mmoja aliwahi kupiga marufuku muziki wa bugi,
ambao ulikuwa ni maonyesho ya muziki ya mchana yaliyokuwa yakisha saa kumi na
mbili, na kwa kupiga marufuku muziki huo ilikuwa ni sawa na leo upige marufuku
wanamuziki wa kizazi kipya. Pengo aliloliweka halijaweza kujazwa tena.
Katika
miaka ya 1980/1990
Katika
kipindi hiki kulikuweko na mfumo wa utawala wa shughuli za Utamaduni ambao
pamoja na kuweko maafisa utamaduni wa wilaya, maafisa utamaduni wa mikoa , pia
kulikuweko na baraza la muziki la
taifa (BAMUTA).Kulizaliwa vyama ambavyo
vilifanya kazi kubwa katika kuunganisha wanamuziki kama vile CHAMUDATA na Tanzania Taarab Association. Na itakuwa ni makosa kutotaja show iliyokuwa kubwa sana na
iliyounganisha wanamuziki wa nchi nzima TOP
TEN Show.
Show
hii iliyowezekana kwa ushirikiano wa BASATA, umoja wa vijana, radio Tanzania na halijawahi kutokea tena onyesho lenye ukubwa wa aina hiyo
mpaka leo. Kuvurugika kwa mfumo wa uongozi wa utamaduni kwa kuwaondoa maafisa
utamaduni walioko chini ya wizara ya utamaduni umeacha shughuli za utamaduni
mkononi mwa wafanyabiashara pekee, ambao kwao lengo ni kupata faida za
kiuchumi.Matatizo na matokeo ya kufa kwa utamaduni si lolote kwao. Serikali
inatakiwa ichukue mzigo huu wa kufadhili ukuaji na uendelezaji wa utamaduni, na
kuacha shughuli za biashara ya kazi za sanaa kwa wafanya biashara.
Zama
hizi ndizo zilizozaa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo flava. Zama hizi kuna mapinduzi makubwa sana katika muziki nchini
Tanzania.Bendi nyingi za muziki wa dansi zilianzishwa, hasa kwa wale wakongwe
na kuunda bendi zao binafsi. Kukua kwa teknolojia na kuanza matumizi ya tarakilishi/kompyuta
katika utayarishaji wa muziki. Hapa hasa vijana ndipo waliposhika hatamu na
muziki wa kizazi kipya. Ottu Jazz Band miaka hii walitumia mtindo wa "Discipline"
na walitingisha hasa katika miaka hii. Miaka hii ndipo palipoanza kuwa na
taasisi au kampuni kubwa za uburudishaji wa muziki kama vile Radio One, Clouds FM, Radio Uhuru, Times FM na nyingine nyingi tu.
Sehemu
kubwa ya vijana waliozaliwa miaka ya 1980 na 1990 mwanzoni walianza hamasa ya
kutaka kuwa wanamuziki na kujishughulisha na kazi za muziki kwa kiasi kikubwa
sana. Kipindi hiki ndiko kulikotokea makundi mbalimbali ya muziki wa hip hop
ikiwa ni pamoja na Gangwe
Mobb, Dewplomatz, S.O.S B., Kwanza
Unit, Underground Soulz, Hard Blasterz, na wengine wengi tu. Kipindi hiki ndicho alipoibuka Saleh Jabri anayesemekana kuanzisha muziki wa hip hop kwa kiswahili nchini Tanzania. Moja ya kazi za
Saleh ni ile aliyorudia wimbo wa Vanilla Ice "Ice Ice Baby"
kwa kutia maneno ya Kiswahili.
Katika
miaka ya 2000/2010
Katika
kipindi hiki, muziki uliokuja juu sana ulikuwa "Bongo
Flava na muziki
wa dansi ambao hasa vijana wapya au wa
muda kiasi walirudi kwa kasi katika kipindi hiki. Hapa bendi ambazo zilijaribu
katika kipindi cha miaka ya 1990 katikakati na mwishoni zilirudi na zilivuma
kupita kiasi. Bendi kama African Revolution iliyokuwa inatumia jina au mtindo
wa chumvi-chumvi tutalamba ilirudi na jina la "Tam-tam" chini ya uongozi
wake kocha wa dunia Mwinjuma Muumini. Vilevile T.O.T
Plus Band, The African Stars,
akina Bob Rudala, Jungle Survivors Band
na nyimbo yao ya Maprosoo, Malaika Band, Extra Bongo, Double M Sound ya Mwinjuma
Muumin, Mchinga
Sound, Diamond Sound, Akudo Impact, Inafrica
Band na bendi nyinginezo nyingi
zilitingisha katika zama hizi. Chuchu Sound Band
ni miongoni mwa bendi zilizotamba sana mwanzoni mwa miaka ya 2000. Waliimba
mtindo wa chakacha au mduara kwa lugha maarufu. Bendi hii ilikuwa tishio katika
mtindo huo. Bila kuisahau Kilimanjaro
Connection Band. Itaendelea
No comments:
Post a Comment