CHANZO CHA USHOGA NA USAGAJI. - waleo blog

Breaking

Wednesday 25 March 2020

CHANZO CHA USHOGA NA USAGAJI.


#Durusika

Ushoga (homosexuality)ni mwenendo wa kimapenzi unaokwenda tofauti na kawaida wanayofanya mwanaume na mwanamke, yaani kupendana na kuzaliana katika familiaJinsia hizo mbili zinalenga kukamilishana katika ndoaMungu baada ya kumuumba Adamu alisema, “Si vema mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwa 2:18). Umbile la mwanaume linaelekea kukamilisha na lile la mwanamke kiroho na kimwili. Lakini roho haionekani, hivyo ni rahisi zaidi kuona jinsi miili yao inavyofaa kuungana iwe mwili mmoja. Hata hivyo tuelewe ya kuwa ukamilifu huo unafanyika katika nafsi ambazo zina vipawa tofauti vinavyowezesha kwa pamoja kukabili vizuri maisha ya nyumbani, ya uchumi, ya siasa, ya dini n.k.

Mwelekeo wa kimapenzi humaanisha muundo wa kudumu wa kimhemko, kimahaba na mivuto ya kimapenzi kwa jinsia fulani. Mwelekeo wa kimapenzi kwa kawaida humfanya mtu kupenda jinsia tofauti na ya kwake yaani, kuwa na mvuto kwa wahusika wa jinsia nyingine, jambo ambalo linawezesha uzazi kadiri ya maumbile. Hata hivyo kuna mashoga/wasagaji (mwanaume anayevutiwa na wanaume/mwanamke anayevutiwa na wanawake), na watu wanaopenda jinsia zote mbili (mwanaume au mwanamke anayevutiwa na jinsia zote mbili; kwa Kiingereza huitwa (bisexual).Mbali na wale wasio na mwelekeo wowote wala kusikia mvuto wowote wa namna hiyo (kwa Kiingereza huitwa (asexuals). Mwelekeo ukifuatwa unageuka tabia.


CHANZO
Vivutio vya msingi ambavyo huunda mwelekeo wa kimapenzi wa watu wazima kwa kawaida huibuka katikati ya utoto na kubalehe. Hakuna makubaliano kati ya wanasayansi juu ya sababu halisi ambazo humfanya mtu kuwa na mwelekeo wa kupenda jinsia ileile ya kwake au kupenda jinsia zote mbili badala ya jinsia tofauti tu kama ilivyo kawaida. Wengi wanafikiria asili (biolojia) pamoja na mazingira vinachangia. Lakini mara nyingine ni kwamba mtu ameathiriwa na tukio ambalo amefanyiwa hasa utotoni au amekubali mwenyewe kujaribu kufanya na hata akazoea kiasi cha kushindwa kujinasua.

Kati ya wale ambao wakati wa kubalehe wanayumba kwa muda fulani katika kujitambua, wengi wao baadaye wanakomaa vizuri katika mwelekeo wa kawaida. Kumbe watetezi wa ushoga wanataka hao vijana wapewe dawa za kusimamisha ubalehe ili baadaye iwe rahisi kuwafanyia upasuaji wa kubadili viungo vya uzazi. Ukweli ni kwamba suala si kila mtu kuamua awe wa jinsia gani, kana kwamba mwili hauna maana, bali kujitambua na kujikubali alivyo.
Binadamu, akiwa na akili na utashi, halazimiki wala hapaswi kufuata mielekeo yake yote, bali anatakiwa kuidhibiti, la sivyo ataharibika upande wa afya ya mwili na ya nafsi vilevile. Mbali ya kuharibu maisha ya jamii,mfano, mtu anaweza kuwa na mwelekeo wa kuwazini watoto wadogo, mwingine wa kula kupita kiasi, n.k. Wakifuata mielekeo hiyo wataleta madhara tu. Hivyo wafikirie kabla ya kufuata mwelekeo wowote na wazingatie maadili mema.
Watu wana mang'amuzi tofauti juu ya mwelekeo wao wa kimapenzi. Baadhi wanajitambua kwa muda mrefu kabla hawajaanza uhusiano na wengine. Baadhi hujihusisha na vitendo vya kimapenzi kabla ya kujitambua na kuchukua msimamo juu ya mwelekeo wao. Pengine mashoga, wasagaji na wapenda jinsia zote mbili hukumbana na unyanyapaa, na hata ukatili mkubwa kwa sababu ya mwelekeo wao wa kimapenzi tofauti na kawaida. Wengi hubaguliwa kwenye shulevyuo, na sehemu zao za kazi, wananyimwa huduma za afya na haki, na hupata msaada mdogo kutoka kwa wanafamilia na marafiki. Ubaguzi na unyanyapaa hufanya iwe vigumu kujitangaza kuwa shoga, msagaji, au mpenda jinsia mbili.
Wakati hili ni tatizo la kimataifa, hali ni mbaya hasa katika sehemu kubwa za Afrika. Kituo cha Utafiti cha Pew mnamo mwaka 2007 kiligundua kuwa 3% tu ya watanzaniawakenya, na waganda wanaamini kuwa ushoga unapaswa kukubalika. Hivyo katika nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), isipokuwa Rwandangono ya jinsia moja huchukuliwa kuwa ni uhalifu na pengine adhabu yake ni kifungo cha muda mrefu. Matokeo yake, ni wachache tu walio wazi kuhusu mwelekeo wao wa kimapenzi, wakati wengi wanalazimishwa kuishi kwa usiri na uwongo, ili waendane na maadili yaliyokubalika katika jamii yao.
Chuki dhidi ya mashoga, kwa Kiingereza (homophobia) ina madhara makubwa kwa afya ya akili na ustawi wa watu walio mashoga, wasagaji na wapenda jinsia mbili, hasa ikiwa wanajaribu kuficha mwelekeo wao wa kimapenzi. Unyanyapaa na ukatili vinazidisha mafadhaiko waliyonayo tayari kutokana na kutambua tofauti iliyopo kati ya mwili wao na mwelekeo wao. Mara nyingi wanashindwa kukabili hali hiyo na kujikubali walivyo. Hivyo wako katika hatari ya kuingia ulevi wa aina mbalimbali kujiua kuliko wenzao wanaovutiwa na jinsia tofauti. Watu wanaotamani kuwasaidia wanaweza kufanya kazi na mashirika husika kuwapatia ushauri nasaha pamoja na kupambana na unyanyapaa.
Mashoga, wasagaji na wapenda jinsia mbili wanaotaka kupunguza unyanyapaa wanaweza kuwa wazi kuhusu mwelekeo wao wa kimapenzi, huku wakichukua tahadhari muhimu ili kuwa salama kadiri iwezekanavyo. Kuwaambia watu wengine kuwa wewe ni mpenzi wa jinsia moja au tofauti huitwa, kujitokeza. Mara nyingi hiyo ni hatua muhimu ya kisaikolojia kwa watu walio mashoga, wasagaji na wapenda jinsia mbili. Kati yao wanaohisi lazima wafiche mielekeo yao ya kimapenzi huripoti wasiwasi wa mara kwa mara kuliko mashoga na wasagaji ambao wako wazi. Japokuwa unapaswa kujitokeza ikiwa unataka na uko tayari. Ingawa unatumaini kuwa marafiki na familia watakupokea na inawezekana kwamba hawatakubali. Ikiwa unategemea wazazi wako kifedha, unaweza kutaka kungojea. Inawezekana kwamba wanaweza kuguswa vibaya na kujaribu kukufukuza nyumbani, kukuweka kwenye ndoa ya jinsia tofauti au kwenye matibabu mabaya ya kiakili. Kama utajitokeza, ni vizuri kuanza kwa kumwambia mtu ambaye una uhakika kuwa atakuwa na mtazamo chanya. Kujitokeza kunaweza kuwa moja ya kazi ngumu sana utakayokabiliana nayo katika maisha yako, lakini pia inaweza kuwa moja ya kazi zenye tunu sana. Kujitokeza ni njia mojawapo ya kuthibitisha hadhi yako na hadhi ya watu wengine walio wasagaji, mashoga, na wapenda jinsia mbili.

KIAFYA
Miongo mingi ya utafiti na uzoefu ya kitabibu imepelekea mashirika ya afya na ya afya ya akili kuthibitisha kuwa mielekeo hii si ugonjwaShirika la Afya Ulimwenguni (WHO) liliondoa ushoga kutoka kwenye orodha yake ya magonjwa ya akili mnamo 1990 na kwamba mapenzi ya jinsia moja si magonjwa na hivyo hayahitaji matibabu. Hadi leo, hakuna utafiti wa kutosha wa kisayansi kuonesha kwamba tiba inayolenga kubadili mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja ni salama au inafaa. Kwa kuongezea, inaonekana kwamba uhamasishaji wa matibabu ya mabadiliko huchangia mazingira mabaya kwa mashoga, wasagaji na wapenda jinsia mbili.
Tafiti tofauti kote ulimwenguni zimegundua kuwa mtu 1 hadi 10 kati ya 100 wanavutiwa na watu wa jinsia yao. Ushoga umekuwepo katika jamii na tamaduni nyingi, na pia hutokea katika spishi 500 hivi za wanyama.Jambo hilo linatumiwa na watetezi wa ushoga kusema kwamba ni kawaida ya kimaumbile. Lakini wanaosema kuwa ushoga ni kinyume cha maumbile wanamaanisha maumbile ya binadamu yanayotakiwa kuongozwa na akili na utashi, si silika tu kama ilivyo kwa viumbehai wengine wote. Kwa mfano, ubakaji unafanywa na wanyama mbalimbali, lakini kwa binadamu haufai kabisa.
Moja ya dhihirisho la mapema zaidi ulimwenguni la ushoga kati ya watu ni michoro ya miambani ya Wasan wa Zimbabwe ambayo inaonyesha mahusiano ya jinsia moja ambayo ni ya maelfu ya miaka iliyopita. Michoro hiyo na vilevile ushahidi mwingine wa kihistoria unaonesha kuwa ushoga umekuwepo katika bara la Afrika katika historia yote, na si umeletwa na mataifa ya Magharibi kama inavyodaiwa. Hata hivyo sasa ustaarabu wa Magharibi unahamasisha ushoga kwa mbinu zote katika kuhimiza mienendo yoyote ya anasa isiyo na uwajibikaji kwa jamii. Katika kuwatetea umefikia pengine hatua ya kuwafanya kielelezo cha maendeleo ambayo hatimaye yamejikomboa kutoka mitindo ya maisha ya zamani na tunu zake, kama vile familia, uzazi n.k. Kwa namna hiyo unabomoa misingi yenyewe ya maisha ya jamii. Pengine wenyewe wanatangaza mtindo wao kama ndio bora na kudharau hiyo mingine (k.mf. maandamano ya "Gay Pride").


DINI
Tamaduni za kijamii au za kidini hazitakiwi kuhalalisha tena ubaguzi dhidi ya mashoga, wasagaji na wapenda jinsia mbili. Uonevu na unyanyasaji, kuwakatalia watu walio wasagaji, mashoga, na wapenda jinsia mbili fursa na heshima sawa au kuwatuhumu kwa vile walivyo au wanavyotenda si uchaji wa Mungu wala ufuataji tamaduni bali ni ubaya tu. Kuchukia maovu ni tofauti na kuchukia mwovu. Hata hivyo suala la maadili linabaki: je, ni halali kufuata mwelekeo wowote ambao tunajisikia au tumejizoesha kwa kurudiarudia matendo maovu? Tukikubali watu wafanye lolote wanalojisikia, jamii itakuwaje?
UyahudiUkristo, na Uislamu kimapokeo huchukulia tabia za mapenzi ya jinsia moja kuwa ni dhambi. Mafundisho ya UhinduUbudhaUjain, na Usikh hayako wazi kabisa juu ya mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja, na viongozi wa dini wanatoa maoni tofauti. Leo,baadhi madhehebu wanazidi kukubali mapenzi ya jinsia moja, na hata ndoa ya jinsia mojaIdadi inayokua ya madhehebu ya Uprotestanti hufanya baraka za ndoa za jinsia moja. Watu wengi walio mashoga, wasagaji na wapenda jinsia mbili wanaripoti kwamba hawaoni mgongano kati ya mwelekeo wao wa kimapenzi na imani yao. Hayo yote hayamaanishi kwamba ndio ukweli; pengine ni kupotewa na hekima au ni kujilegeza na kufuata tu mkondo. Ni lazima kufikiria uumbaji wa mtu katika jinsia mbili ili kuelewa Muumba alitaka nini, hasa alipounganisha kilele cha tendo la ndoa na uwezekano wa mimba kupatikana.
Hivyo mashoga na wengineo wanahitaji msaada wa pekee kuelewa mpango wa Mungu kuhusu jinsia na hatimaye kuishi namna ya kumpendeza. Msimamo wa Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki ni wa namna hiyohiyo: kwamba ngono inakubalika tu katika ndoa.

Zuia kitendo hicho,hakifa.

Maoni na ushauri ni hapa,,,,
                      +255767611645
                        +255715080716
                      Mwanaharakati1992@gmail.com
                      Adamgome96@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Pages