JINI AISHIE CHOONI, HUYU HAPA. - waleo blog

Breaking

Wednesday 25 March 2020

JINI AISHIE CHOONI, HUYU HAPA.


Tafadhali, makala hii imetazama zaidi upande mmoja wa dini,kulingana  na upatikanaji wake taarifa.Yaweza kukukera;;utusamehe kwa mapungufu haya.

#Ghaibu
JINI WA CHOONI(ghadimul ghalaa)
Jini huyu ni miongoni mwa majini wa aina mbalimbali wenye kuwadhuru binaadamu.
Jini huyu makazi yake makubwa ni kwenye vyoo na bafu yanavyotumiwa na binaadamu na hata vile ambavyo havitumiwi, tena  vimebaki kama magofu,
 Jini huyu ndiye chanzo cha balaa nyingi.
Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa akijilinda kwa MUNGU kutokana na jini mchafu tena wa hatari wakati wa kuingia chooni au bafuni na alikuwa akisema hivi, “Ewe MUNGU hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na uchafu wa chooni pamoja na wachafu (mashetani)”, na wakati wa kutoka Mtume alikuwa akimshkuru Mungu kwa kusema, “ Shukrani ni za Allah /Mungu ambaye kaniondolea maudhi ya(shetani) na akanipa afya”, kwani ukipatwa na shaytwani huyu afya yako inaharibika na chooni ndio nyumba za majini na makazi yao, kwa hiyo ziko adabu za kuingia chooni, Lazima adabu hizi zizingatiwe na kila mtu ili kuepuka kukumbana na jini huyu.
ADABU ZA KUINGIA CHOONI
a) Mtu aingie chooni kwa kutanguliza mguu wa kushoto na akitoka atanguliza mguu wa kulia.
b) Mtu asizungumze kwa sauti akiwa chooni ila kwa dharura, na wana wachuoni wakazitaja dharura hizo kuwa ni:
i) Kumtambulisha alie nje ajue kama wewe uko chooni ili nae asiingie humo, hapo itabidi ujikohoze kohoze.
ii) Kumuongoza mtu ambae ni kipofu au kumtahadharisha mtoto mdogo kutokana na jambo la hatari, hapo itakubidi useme tu.
c) Mtu asiimbe au kupiga makelele chooni.
d) Mtu asivue nguo zake zote chooni, kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo ila avue eneo ambalo anataka kujisaidia tu,yaani ashushe kidogo kiasi cha haja tu.
e) Mtu akitoka salama chooni amshukuru Mungu kutokana na usalama huo.
f) Na asimwage maji chooni wakati wa usiku ila awe kamtaja Mwenyezi mungu kwa sauti ya juu akiwa nje mlangoni.
Hizi ni baadhi ya adabu za chooni, ambazo adabu hizi mtu akizipuuzia ndipo jini huyu mchafu hupata urahisi wa kumvamia na urafiki wa madhila ukaanzia hapo.
Khaadimul-ham-maam, majini hawa wako wa aina mbili, kuna aina anayoonekana moja kwa moja chooni na yuko asiyoonekana.Wanaoonekana ni hatari zaidi,kuliko wasio onekana.
DALILI ZA MTU ALIYEINGIWA NA JINI HUYU WA CHOONI.
a) Mgonjwa hupenda kuingia chooni na kukaa huko muda mrefu.
b) Baadhi ya wagonjwa hujikuta wanasinzia wakiwa chooni wanajisaidia.
c) Mgonjwa hupenda uchafu sana na kulala bila kuoga.
d) Kupenda Kuingia chooni wakati wa kiza.
e) Mtu kuchukia kusikiliza Qur-an na adhana,na hata nasaha zozote zinazohusu dini
f) Kuonekana nyayo kwenye mwili wa mgonjwa kwa rangi ya kijivu au nyekundu.
g) Maumivu kwenye maungio ya viungo pamoja na kupoza mwili.
Na ndio maana baadhi ya watu humuita jini huyu kuwa ni subiani wa chooni. Na jini huyu yuko ambaye humtokezea mtu huko huko chooni wakaonana ana kwa ana, na akimtokezea mgonjwa humfanyia haya yafuatayo:
- Humpiga mgonjwa
- Humtisha mgonjwa
- Huanza kumchezea chezea kama vile mume anavyocheza na mkewe kwa kumshika shika sehemu za siri na kumbusu.

Haya ndio mambo ambayo jini huyu wa chooni anapomtokezea mgonjwa huyafanya.

Njia za awali za kujikinga nae ni kuomba kinga/msaada kwa MUNGU akusaidie pindi uingiapo chooni,bila kusahau kufuata adabu za chooni kama ulivyosoma.
Ikiwa una mgonjwa/wewe mwenyewe unadalili miongoni mwa hizo ulizosoma hapo,tafadhali nenda kwa wataalamu ambao hawapigi manyanga wala kupandisha majini ndipo wakutibie; bali nenda kwa wataalamu wa kisheria wa dini. Mfano

+255712172328

Mtaalamu wa tiba za kijini kwa uwezo wa Mungu.


Usisite kutushauri na kutoa maoni yako kwa chochote ukionacho kisichokupendeza hapa;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;+255767611645
                                            +255715080716

No comments:

Post a Comment

Pages