HUDUMA YA KWANZA KWAALIYEPATA MSTUKO. - waleo blog

Breaking

Wednesday 25 March 2020

HUDUMA YA KWANZA KWAALIYEPATA MSTUKO.



#AFYA

Tumewapoteza ndugu, rafiki na jamaa zetu wengi kwa sababu ya mshtuko(Shock) iliyosababisha kifo chao. Hii ni kwa sababu watu wengi hawajui jinsi ya kumsaidia mtu mwenye mshtuko kabla ya kumpeleka hospitali. Leo Mwenyezi Mungu akipenda nakuletea makala inayokufundisha hatua zote za kufanya ili kumsaidia mtu mwenye mshtuko. Naomba uwe na mimi mpaka mwisho wa makala hii.

Tuanze kwa kujua kuhusu mshtuko.
Damu huzunguka kwenye mwili wa binadamu kutoka kwenye moyo na kusambaa kwenye sehemu zote za mwili kwa kupitia mirija ya damu inayotumika kusafirishia hiyo damu, wakati huu damu inayozunguka mwilini huwa imebeba hewa ya oksijeni kwenye ogani  na misuli  yote ya mwili. Hii hutokea kwenye hali ya kawaida ya moyo kufanya kazi.

 Mshtuko ni pale mfumo mzima wa kusafirisha damu mwilini unaposhindwa kufanya kazi vizuri. Hali hii hutokea mara nyingi baada ya mtu kupata ajali, maumivu au ugonjwa wa ghafla  hasa kama huu ugonjwa wa ghafla una ambatana na maumivu.
Sababu kubwa sana zinazoweza kusababisha mshtuko ni kuvuja damu kwa wingi inayozidi lita 1.2 kwa muda mfupi, upungufu wa maji mengi mwilini unaosababishwa na kuharisha, kutapika, utumbo kujisokota  na kuungua moto.

Dalili za mtu aliyepata mshtuko
Mtu aliyepata mshtuko anaweza kukosa hewa kwenye akili, dalili zingine za mtu mwenye mshtuko ni;
  • Mapigo ya moyo kwenda kwa kasi.
  • Mgonjwa kuwa dhaifu.
  • Mgonjwa anapauka mwili.
  • Mwili kuwa wa baridi na ngozi kukakamaa.
  • Kutokwa na jasho.
  • Anabadirika rangi  hasa kwenye midomo, vidole au kwenye masikio.
  • Kizunguzungu.
  • Kichefuchefu na hata kutapika.
  • Huvuta pumzi kwa shida.
  • Hupata   Kiu cha maji
  • Kutokutulia lakini pia anakuwa mkali.
  • Kupiga miayo sana.
  • Kutokujitambua na mwisho moyo unashindwa kufanya kazi na mgonjwa anaweza kufa.
Baada ya kuzijua dalili za mtu mwenye mshtuko, twende sasa tukajifunze namna ya kumhudumia huyu mgonjwa kwa huduma za dhalula kabla ya kumpeleka hospitali.

Jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu mwenye mshtuko.
  • Mlaze mgonjwa chini sehemu ya wazi na yenye hewa safi. Hakikisha ulipomlaza siyo pa baridi sana na weka miguu yake juu kidogo zaidi ya kichwa ili kusaidia damu kuzunguka hadi kwenye akili kichwani.

  • Mtie moyo mgonjwa mara kwa mara pindi anapoanza kuzinduka.

  • Fungua na ulegeze sehemu zote za mwili wake zilizofungwa na kukazwa kwa nguo zake kama kiunoni, shingoni mikononi n.k.

  • Fanya utaratibu wa kumpeleka hospitali.

  • Mpime mgonjwa vipimo vya kuangalia mapigo ya moyo.

  • Kama mgonjwa hajitambui kabisa. inabidi umfungue kwenye njia ya hewa na umuangalie kama anapumua vizuri. Utamtambua kwa kuangalia kama kifua  kinapanda na kushuka hata kama ni kwa shida. Lakini kama hapumui vizuri tumia kiganja chako kusukuma kidogo kifua chake kuelekea ndani mara kwa mara huku ukiendelea kuangalia kama ameanza kupumua. 

  • Mshtuko (shock) ni ugonjwa unaotishia maisha ya binadamu kwani unatokea pale hewa safi ya oksijeni inapokosekana kwenye ogani muhimu za mwili kama vile akili, moyo na mapafu. Kwa hiyo  mgonjwa anahitaji huduma za haraka sana anapopatwa na mshtuko ili kuzuia uharibifu au kutokufanya kazi kwa ogani muhimu za mwili.
Mshtuko unaweza kuwa tatizo kubwa sana kama mgonjwa atakuwa na maumivu makali na uoga pia.


Kwa leo naomba niishie hapa lakini tukumbuke kuwa huduma ya kwanza inatolewa na mtu yeyote na si ya nesi na daktari tu. tuwajibike katika kuwasaidia ndugu zetu.
Sambaza na wengine wajifunze huduma hii ya kwanza kwa aliyepatwa na mshtuko.

Kwa msaada,maoni na ushauri ni hapa;
                                                +255767611645
                                                adamgome96@gmail.com
                                                +255715080716

No comments:

Post a Comment

Pages