#AMKA
Kipimo cha uongozi ni jinsi gani
kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.
Kiongozi bora hana muda wa kulalamika bali
anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi au watu
walio chini yake. Kiongozi wa kweli akiongea, watu husikiliza.
Au
Uongozi ni dhana, taaluma inayompa mhusika madaraka na uwezo wa
kuwawezesha wale awaongozao ili kuunganisha nguvu, stadi, vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia
malengo yao. Kuongoza ni kujua lengo la wale wanaoongozwa na njia ya kufikia
lengo lao.
Uongozi ni dhana, taaluma anayopewa
mhusika katika kuwaongoza wale waliohitaji kusimamiwa au walioamuliwa
kusimamiwa katika kufanikisha jambo fulani kwa maslahi ya wote au ya mtu mmoja
mmoja.
Aina za uongozi
i) Kuna njia nyingi za kuainisha
uongozi lakini njia ya msingi ni kuangalia jinsi kiongozi alivyoingia
madarakani na utaratibu wake wa kuongoza.
iii) Viongozi hawa wote tunaweza
kuwagawa katika mafungu yafuatayo kutokana na jinsi
walivyoingia madarakani na namna wanavyoongoza kama ifuatavyo:
·
i. Wale wanaopata uongozi kwa kurithi.
·
ii. Wanaopata uongozi kwa kuchaguliwa.
·
iii. Wanaojitawalia mamlaka ya kuongoza kwa nguvu.
·
iv. Wanaoteuliwa na mamlaka za juu zaidi.
iv) Kiongozi anayeingia madarakani kwa
mojawapo ya njia zilizotajwa hapa juu anaweza kutumia mtindo wake wa uongozi. Ipo mitindo
mbalimbali ya uongozi:
Uongozi wa kiimla ni mtindo wa kuongoza ambao
kiongozi huongoza kwa amri bila kushirikisha watu wengine
katika kufanya maamuzi. Mara nyingi uongozi wa aina hii haulengi katika
kukidhi maslahi ya walio wengi, bali tu ya yule
anayeongoza na wale wanaomlinda.
Uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kushirikisha watu katika
kufanya maamuzi na utekelezaji wake. Kwa kawaida viongozi wa
aina hii hulenga kukidhi mahitaji ya walengwa.
Viongozi wanaochaguliwa mara nyingi huwa
wanapewa muda wa kuongoza, na wale viongozi wanaojiteua hujipatia wao wenyewe
muda wa kuongoza au hata hapo watakapoamua kuachia madaraka.
Sifa za
kiongozi bora
i. Awe na ufahamu. Kiongozi ni lazima
awe na ufahamu mkubwa
juu ya taasisi anayoiongoza,
malengo yake, mazingira na matatizo yake.
ii. Awe mwaminifu. Kila taasisi
inalenga kufikia shabaha fulani. Ni wajibu wa kiongozi kuwaongoza
wanataasisi ili wafikie malengo yao. Kwa hiyo kiongozi ni lazima aweze kubuni
mikakati na mbinu zitakazoiwezesha
taasisi anayoongoza kufikia malengo yake katika kuonesha njia.
iii. Awe na maadili mema. Kiongozi ni lazima
akubalike katika jamii na
taasisi anayoiongoza. Ili akubalike hana budi kuzingatia maadili ya msingi ya
jamii na taasisi yake. Kiongozi mwongo, mlevi, mvivu, asiye mwaminifu n.k.
hawezi kuwa kiongozi mzuri.
v. Awe anakubalika na watu
anaowaongoza.
vii. Awe anakubali kushauriwa au
kupokea ushauri kutoka kwa wengine.
Viii. Awe ana uwezo wa kujifunza kutoka
kwa watu wengine waliofanikiwa.
Mungu
ibariki Afrika,Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania, uipe amani ya milele,uwajaalie
viongozi wake waendelee na wawatendee mema wanaowaongoza pia uwatenze nguvu
wasiozitakia mema nchi zao na za wenzao..Aamina.
Share na wengine wapate faida.
No comments:
Post a Comment