U.T.I NA KINGA YAKE - waleo blog

Breaking

Wednesday, 19 February 2020

U.T.I NA KINGA YAKE


#AFYA


Ugonjwa unaojulikana kama UTI, ambao ni kirefu cha maneno Urinary Tract Infection, ni maambuziki yanayopitia njia ya haja ndogo.
UTI ni miongoni mwa magonjwa yanayosumbua viungo na kumuathiri mtu wa aina yeyote.

DALILI ZA UTI
Huenda wakati ukiendelea kusoma ukajikuta wewe ni mmojawapo unayesumbuliwa na:-
-Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
-Unapata kichomi upande wa kushoto
-Mwili kupata joto kama una malaria.
-Unapata miungurumo tumboni
-Kujisikia kuchoka bila sababu
-Kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati wa kukojoa.
-Kuhisi kuunguzwa na mkojo kwenye kibofu au mrija wa mkojo.
-Mkojo kuwa na harufu mbaya na pia kubadilika rangi kuwa nyeusi au rangi ya mawingu.
-Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo  huku unapata maumivu kwenye njia ya kupitisha mkojo.

Lakini kwa vile hujafanya vipimo vya haja ndogo huna habari kwamba kinachokusumbua ni UTI.

MAAMBUKIZI YA UTI
Maabukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya yanasababishwa na viumbe kama bakteria,fangasi na virus.
Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)
husababishwa na vimelea ambavyo kitaalamu hujulikana E. Coli. Vimelea hawa huishi kwenye mfumo wa chakula hadi kwenye njia ya haja kibwa bila kuleta madhara yoyote ila wakiingia kwenye njia ya mkojo huleta maambukizi, hii hasa kwa wanawake.
Lakini wapo wanaoweza kupata ugonjwa huu kutokana na tendo la kujamiiana bila kufuata taratibu za usafi na mtu mwenye UTI sugu.


JINSI YA KUKINGANA NA UGONJWA HUU WA U,T,I.
Watu wengi tumekuwa tukitumia vyoo ndivyo sivyo na hatima yake tunajikuta tukipoteza gharama nyingi kuutibu ugonjwa huu,badala yake pesa zile zingeweza kusomesha watoto ama kufanya majambo mengine ya kimaendeleo.Kimsingi ukaenda kupima kisha ukaambiwa una U.T.I, cha kwanza unachotakiwa kukijua ni kwamba wewe ni mchafu vyooni.Hii ni aibu,kwa nini uendelee kuipata aibu hii na wakati kusafisha choo chako ni muda mchache sana!!? Badilika.

ONYO NA ANGALIZO
Haipendezi kwa mwanaume na mwanamke kukojoa wakiwa wima na tena bila kutawadha na maji safi(kuosha palipotoka mkojo au mavi).Kuacha na kufuata hivyo kutakupelekea kuepuka na kuwaepushia wenzako maambukizi ya ugonjwa huu wa U,T,I.

No comments:

Post a Comment

Pages