#MAHUSIANO
Wahenga wanasema,
kosea njia utaelekezwa kwa kupita,mtoto hupotea lakini mkubwa huchelewa
kufika….Oyo,,usikosee kumpata mume ama mke mwema utajuta kuzaliwa.Katika makala
hii leo nimeona tukumbushane ama kufahamishana katika zile sifa za mume ama mke
anepasa kuolewa na kukuoa.Zifuatazo zitakusaidia kumchagua mwenzi wako.
1. Mwanamke/mume kuwa na dini, tabia na maadili mema. Dini si
ya kinadharia bali imfanye abadilike katika mambo yake yote kama kuwa
na tabia njema na maadili mema.Hii ni kwa waaminio kuhusu dini zilizokuja na
wageni,ndio sababu yetu waafrika kuwa wastaarabu.
2. Kumpendeza mume/mke anapomuangalia.
Kupendeza na uzuri ni vitu ambavyo kila mwanamme ana kile anachokiona kuwa ni
kizuri. Hivyo hapa wanaume wazingatie sana kwenye kuangalia kitu ambacho
kitampendeza amwangaliapo mkewe,mfano rangi (mweupe ama mweus)i,mnene ama
mwembamba,mwenye matiti madogo ama makubwa ama mwenye makalio madogo ama
makubwa.Hivi ni kwa uchache zaidi.
3. Kuwa ni mwenye kuingiliana na watu na mwenye
moyo wa bashasha kabisa. Mafungano ni baina ya familia mbili, yako na
yake. Kwa ajili hiyo anatakiwa awe ni mwanamke mwenye kufanya mahusiano na watu
wako wa karibu ili kuwe na maendeleo na uhusiano mwema.
4. Mwenye kuzaa/kupanda mbegu bora, na
hili kama wataalam walivyosema, ni kuangalia kizazi cha madada zake
na jamaa zake wa karibu.Na ikatokezea mumgu hakumjaalia kizazi, basi turejee
katika dini zetu zinasemaje.
Hata hivyo, muhimu zaidi ni dini na ikiwa ana sifa nyingine ziwe ni baada ya hiyo sifa ya kwanza.Unaweza
kuhoji kwa nini dini? Watu tuliowengi barani Afrika,Asia na sasa mpaka ulaya
tunaamini ya kuwa kama si kuja kwa dini zilizo mtangaza Mungu asiyeonekana (dhahania)basi
ustaarabu tulio nao hivi leo tusingekuwa nao.Mfano, zamani hizo kabla ya hizi dini watu waliamini ya
kuwa mototo mlemavu ni laana na hapaswi kuishi isipokuwa auwawe.Zilipokuja dini
zikatuelimisha ya kuwa watu wote wanahaki ya kuishi bila kujali ulemavu
wao.Hivyo basi tunaposema kigezo kikubwa cha mume ama mke ni dini kwa sababu za
msingi zifuatazo.Ndani ya hizi dini yapo mafundisho ambayo yanamtaka mtu asiwe
mshirikina,asiwe mwenye kuchezea mali kwa fujo,awe mwenye kuwaheshimu wakubwa
kwa wadogo na chochote utakachokifikiria katika akili yako basi katika dini
zetu hizi majibu yapo.”Ila ni nani utamuuliza
kazi ni kwako”.kwa mantiki hiyo, mwanamke au mwanaume kama atakuwa ameshiba katika mafunzo ya dini ni wazi ya
kwamba ndoa hiyo ni ya kudumu tukiachana na makosa ya kibinadamu.mfano mboga
kuzidi chumvi ama mume wangu anifikishi.
Share na wenzako wapate mke ama mume
mwema na sio bora niolewe/kuoa.
No comments:
Post a Comment