Habari ya muda huu ndugu wasomaji
wetu, karibuni tena tujadiliane mambo mbalimbali unayopaswa kuzingatia pindi
unapoachwa na mpenzi wako .
1: Usiharakishe uhusiano mpya.
Unapoachana na mpenzi wako basi jipe
muda kutafakari mapungufu yako na wapi ulikuwa unakosea.
Kuanzisha uhusiano mpya baada ya
kuachwa huwa mara nyingi unaenda sehemu ambayo sio sahihi na utajiku unaambulia
kuachwa.
Utahitaji mtu wa kukufariji na yeye
akatumia mwanya kukupa care as if he/ she is into you.. but hakuna kitu kama
hicho mtachokana mapema na kusiwepo na mapenzi ukabaki unatanga tanga na
usipokuwa makini basi utatumika sana.
2. Usiseme hauta penda tena.
Kosa la mtu mmoja basi usijumuishe
kwamba watu wote watakuwa kama mpenzi wako, ikakusababisha kutokupenda watu
wanatofautiana.
Haina maana aliyekuumiza kila mtu
ataku cheat au kwasababu mpenzi wako alikuwa anakutukana na kukupga ukahisi basi
wote wapo hivyo.
Ni vizuri ukamsoma mtu tabia zake
kabla hujajiingiza kwenye uhusiano. Anza kutengeneza muelekeo wa penzi
unalotaka.
3. Acha upweke jichanganye na watu.
Watu wengi wakiachika basi
wanajisahau na kuanza kuomboleza na kuacha kufanya mambo ya msingi.
Ukiomboleza uhusiano wako uliopita
mama/baba hapo utakuwa hujaacha wala kuachika.
Changamka jichanganye na watu na
ufurahi, hii itapelekea kusahau mapema na kufanya mambo ya maendeleo.
Haitakiwi wewe kuwa mnyonge wakati
ulie achana naye anaruka majoka anafurahi maisha na mambo yake yanaenda.
Nataka nikueleze, maisha ni mafupi
achana na kufikiria kuachwa na mpenzi wako. Unatakiwa kujua kuna maisha baada ya
kuachwa.
4. Ukiachwa kubali.
Usimgande mtu asiye kupenda na
misamaha isiyokuwa na tija.. kama alikuacha inamaana anasababu nyingi za
kukuacha.
Ukishaona katika uhusiano wako mtu
kosa dogo anakimbilia kutoa maneno ya kuachana ujue hakupendi bali anakutumia
tu kimwili.
So akikuacha achika, usimtafute wala
nini wala hakuna mambo ya tubaki kuwa marafiki na blah blah .. kama kachoka
kuwa mpenzi wako ambae mna share vitu vingi zaid ya urafik ataweza kuwa rafiki
huko ni kupotezeana muda na kuchoshana.
5. Acha mambo ya kukumbushia ni ujinga uliopitiliza.
Kama mliachana mkiwa wapenzi na kila
mmoja akaenda njia yake.. mnakumbushia nini!?? Akili zenu zinawaza nini? Mnajua
kama kuna magonjwa!?? atabak kuwa mpenzi tu aliyeachwa na unatakiwa kwenda
mbele usikubali kurudi nyuma.
Suala la kuanza kukuambia mkutane na
kuanza kukumbushiana huku ni sawa hamjaachana ila mnaendekeza umalaya.
Usiwe tegemezi kwenye mahusiano yako
kwani kuachwa umeanza wewe mpaka ushindwe kuendesha maisha yako.
Hakuna jambo ambalo unadharaulika
kama kuachwa halafu unaanza kumng’ang’ania mtu ambaye hana muda na wewe.
Hebu tubadilike jamani kuna maisha
baada ya kuachwa acha kuumiza akili kisa umeachwa.
Share,like,comment na usisahau
kutufuatilia.
No comments:
Post a Comment