UTANGULIZI
Shetani ni sifa ya jini aliyepetuka mipaka kama utakavyoona chini ya makala hii.
Wataalamu wa elimu ya nafsi ya mtu au roho (Psychology) pia elimu inayochunguza habari zinazohusu asili na maendeleo ya binadamu tangu awali (Anthropology) hutuambia kwamba binadamu licha ya kumwogopa, kuhofu na kumwabudu Mungu aliye muumba wake, binadamu huyo kimaumbile anayo tabia ya kuvihofu viumbe vinavyomzidi nguvu kama vile radi, umeme, mito mikubwa, milima, mapango, mawe, wanyama, mizimu, mashetani na hata vitu vinavyoitwa “majini”.
Kutambikia vitu hivyo, hata kuvitolea sadaka ni kudhihirisha hofu waliyonayo wanadamu kwa viumbe hivyo, badala ya kumwabudu Mungu mmoja muumba wa vitu vyote ambaye kadiri ya falsafa ya kweli na maandiko matakatifu tunahakikishiwa kuwa yupo.
Majini ambayo huogopwa na watu wengi katika Afrika na sehemu nyingine duniani, kwa kufikiria kuwa wasipo yaheshimu na kuyaabudu au kuyatolea sadaka yanaweza kuleta hasara kwa watu mfano kupagawa kwa wanawake na watoto, kuleta mabalaa, kuleta mikosi, magonjwa, vifo, kupotelewa na mali n.k.
Kadiri ya ufunuo wa Mungu kutoka maandiko matakatifu pia elimu ya kweli ya falsafa kuna Mungu mmoja tu anayetakiwa aabudiwe, kuna viumbe ambavyo ni rafiki za Mungu na wanadamu ndio “Malaika” yaani malaika wema, na maadui wa wanadamu ni mashetani, pepo wabaya. Hakuna viumbe waitwao majini kadiri ya maandiko matakatifu.
Kama watu wanayaheshimu majini, wanayatolea sadaka kama miungu, wanayaomba basi hapo binadamu wamedaganyika na kupotea. Wasije wakafikiri wanayaheshimu majini kumbe ni yaleyale mashetani kwa kutofahamu kuyaainisha au kuyatofautisha kwa kukosa ufunuo wa kweli juu ya viumbe hao waitwao “Majini”
HISTORIA YA MAJINI KATIKA MATAIFA MBALI MBALI
Ukitazama historia ya mataifa mbali mbali hapo kale unaweza kugundua na kuona vitu vichache vinavyoonyesha mwelekeo unaoashiria kuwa watu wamewahi kuyaabudu hayo majini pengine hata kuyaheshimu kwa vikubwa kama vile miungu, hasa pale unapozisoma hadithi za makabila, mataifa, koo mbalimbali zinazowakilisha umaarufu wao, chimbuko lao au matendo ya umashuhuri, ujasiri, nyakati n.k.
Hadithi hizo ni (fictitious) za kubuni na hata mara nyingine zinaogofya. Kwa lugha ya kizungu zinaitwa “Myths”. Hadithi hizo zilihadithiwa kwa kitambo kirefu na hivyo kuonekana kama ukweli. Baadhi yake
zinahusika na miungu ya kike au kiume. Zipo
hadithi kama vile:
Faun: Mmoja wapo wa miungu ya vijijini ya huko Roma, mwenye sura ya mtu binadamu, mwenye pembe na mkia. Yeye hufananishwa na mungu wa vijijini ahusikaye na Roho ya maumbile, upagani n.k. mahali pengine Faun huonyeshwa akiwa na kiwiliwili cha nusu mwanadamu mwenye pembe na kuanzia kiunoni ana sura ya mbuzi, miguu na kwato.
Faun: Mmoja wapo wa miungu ya vijijini ya huko Roma, mwenye sura ya mtu binadamu, mwenye pembe na mkia. Yeye hufananishwa na mungu wa vijijini ahusikaye na Roho ya maumbile, upagani n.k. mahali pengine Faun huonyeshwa akiwa na kiwiliwili cha nusu mwanadamu mwenye pembe na kuanzia kiunoni ana sura ya mbuzi, miguu na kwato.
Sphynx: ni mnyama mkubwa (Monster) mwenye sura ya Simba , mabawa na kichwa cha mwanamke Sphynex wa Thaebes aliwatega watu wa mahali hapo kitendawili, wale wote walioshindwa waliuawa.
Oedipus aliyekuwa ameketi katika mwamba ambao huyo Sphynx alikalia alipotegua kitendawili hichoalimteremsha kutoka mwamba huo na kumwangusha akaanguka anguko la kujiua.
Hivyo ndivyo Oedipus alivyopata kuwa mfalme wa Thaebes. Kitendawili chenyewe kilikuwa hiki; “ni kiumbe gani kinachotembea asubuhi kwa miguu minne, mchana kwa miguu miwili, na jioni kwa miguu mitatu?”
Satyr: ni moja wapo wa miungu ya kigiriki wa msituni. Anaonekana akiwa na kiwiliwili cha mwanadamu na masikio ya farasi pia na mkia. Waroma nao wanamwonyesha akiwa na kiwiliwili cha mwanadamu mwanaume na masikio ya mbuzi, mkia, miguu na pembe zilizokunjika. Ni mojawapo wa Miungu inayohusika na ashki na ufuska wa kila aina kama tunavyoona duniani hivi leo.
Cyclops: hayo ni majitu makubwa yenye sura ya watu lakini wana jicho moja katikati ya uso. Hadithi yao imehusika na kisiwa cha Sicilly, wakiwa wachungaji chini ya mlima Etna Laocoon: wale waliosoma riwaya za kilatini kuhusu Trojan Horse wanafahamu sana habari hiyo. Yule kasisi aliyekuwa amepelekwa na Athena. Athena: ni mojawapo wa miungu ya kike ya olympia, mashuhuri kwa siasa, utendaji, vita na amani.
Anao uhusiano na Minerva. Minerva: ni mmoja wapo wa miungu ya kike ya kiroma ahusikaye na hekima. Mrille: ni mojawapo ya hadithi za wachaga pamoja na Mregho. Hadithi hizi mbili za wachaga zinaongea juu ya wivu na ukombozi, tambiko na msaada safi na ya kumtuliza Mungu. Sadaka yenye kukubalika (Effecacious).
Hizi nazo nyingi nyinginezo zinaonyesha machimbuko ya vitu fulani fulani, nyinginezo zina mafundisho ya aina moja au nyingine. Kumekuwako na waliothubutu kusema yale yaliyoandikwa katika kitabu cha Mwanzo ni “Myth”, Sio ajabu basi kwamba wengine walivutwa na hadithi hizo wakazipa hadhi na mtazamo wa kuwa na ukweli, na hata wakashikwa na jinamizi walipozipanga majina ya “Majini”.
FALSAFA YA KWELI NA UWEPO WA MUNGU
Falsafa ni neno litokanalo na maneno mawili ya kigiriki yenye maana ya “upendo” na “hekima”. Kwa hiyo neno “Falsafa” lina maanisha “upendaji hekima” falsafa hujishughulisha na utafutaji wa ukweli katika mambo yote na jinsi ya kushikamana na ukweli katika mambo yote. Falsafa huanza kwa njia ya mshangao yaani kitu cha kushangaza kwetu sisi falsafa hukiona cha kawaida tu.
Falsafa inakufanya uwe huru kufikiri na kujitegemea kimawazo na kimaoni. Binadamu asipokuwa na falsafa yoyote humfanya aonekane kama hana faida katika jamii.
Falsafa humsaidia mtu kushinda ndoto zake za mambo fulani. Ni kweli kuwa jinsi kila mmoja anavyofikiria hutegemea jamii, elimu, mazingira, utamaduni, dini, uchumi, tabia na siasa inayomzunguka.
Lakini falsafa inajishughulisha na mambo makuu matatu: yaani Mungu, binadamu na Dunia. Falsafa humsaidia mtu kuwasilisha mawazo yake katika mtiririko wa mawazo mantiki
inatuonyesha kwamba haiwezekani pakawepo na Miungu mingine kama yule mmoja wa kweli, pia binadamu ameumbwa na Mungu, katika falsafa hakuna mahali panapoonyesha miungu ilimwumba binadamu.
Plato na Socrates walikuwa katika kipindi ambacho watu wengi wa ugiriki walikuwa wakiabudu miungu mingi, halikuwepo wazo la Mungu mmoja kama tuelewavyo siku hizi. Lakini wanafalsafa hao waliamini juu ya kiumbe kilicho “kikuu” na “kikamilifu” kuzidi vyote.
Socrates aliamini kuwa kuna Mungu mmoja anayezidi miungu mingine yote.
Plato naye aliamini juu ya Mungu mkuu aliyemwita Demiurge, Mungu huyo alifikiriwa kuwa na uzuri na ukamilifu wote. Zaidi ya hilo wanafalsafa wote waliojua kuwa Mungu yupo na wale waliojidai kukanusha kuwa Mungu hayupo walijikuta wanafafanua uwepo wa Mungu kwa namna moja au nyingine.
Majini ni viumbe wanaosadikika kuishi katika mazingira ya kila aina; pia baadhi
ya watu wanaamini majini ni viumbe wenye
uwezo mkubwa wa kufanya vitu tofautitofauti, pia wenye uwezo wa kujibadilisha
kuwa katika hali waipendayo. Asili ya imani hiyo haijajulikana
vizuri, lakini ilikuwepo Uarabuni kabla
ya Muhammad.mtume wa mungu kwa imani ya dini ya
kiislamu.
Kwa asilimia kubwa wenye imani ya
uwepo wa majini wanasema ni viumbe wasioweza kuonekana, hivyo ni vigumu kupata
uthibitisho wa moja kwa moja kuhusiana na viumbe hao. Kadiri ya imani hiyo
majini waliumbwa na Mungu kwa kutumia moto na
wakiwa wa jinsia mbili; walikuwepo tangu Adamu kuumbwa,
hata enzi za Yesu majini walikuwepo,
mpaka alipokuja mtume Muhamad.
Uislamu huamini kuna majini
wazuri na majini wabaya kwa maana ya madhara yao katika maisha ya mwanadamu na baadhi ya Waislamu (pengine wasiofuata misingi
sahihi ya Uislamu) hufuga majini hao katika nyumba zao au miili yao
na kuwafanya viumbe hao kama wasaidizi au walinzi wa maisha yao kwa wale ambao
huamini ni majini wazuri. Lakini wengine hutumia pia majini waitwao wabaya
kuharibu na kutesa maisha ya watu wengine kwa kuwatuma kuwaingia miilini na
kuleta magonjwa, kuharibu kazi au biashara ya mtu na
hata familia.
Hata wasio na dini na
baadhi ya Wakristo hutumia majini kuponya wagonjwa na vilema na kufanya miujiza mbalimbali kama kwa mazingaombwe.
Pia wapo Wakristo ambao huwatumia majini hao katika mambo yao kama vile
kutafuta mali, watoto n.k.
Pamoja na hayo, Ukristo kwa jumla haupatani na imani hiyo,
ila kuna madhehebu kadhaa ya
Kikristo ambayo huamini uwepo wa majini kwa kuwasawazisha na mashetani. Hivyo kwao hakuna jini mzuri bali
wote ni wabaya kwa kuwa wao na mashetani ni sawa, hivyo ni adui wa Mkristo
yeyote yule kama alivyo Shetani mwenyewe. Wakristo wa madhehebu hayo wamekuwa
wakifanya maombi kwa watu ambao wanadhaniwa kuteswa na majini ili kuwafungua kutoka
katika nguvu zao za uovu,
sawa na pepo ambao Bwana Yesu (mleta habari
njema, yaani Injili) aliwatoa miilini mwa watu na
kuwapa wanafunzi wake (wafuasi wake ambao ni
Wakristo leo) mamlaka na uwezo wa
kuwatoa pia.
Kwa ujumla wake, Mungu Mmoja aliye mfalme wa siku ya malipo, anaweza kukuepusha na
kila jambo baya hapa duniani pasipo
kuangalia wewe ni wa dini gani. Majini, mashetani na binadamu wote ni wa Mungu
na ndiye asili ya vyote, na wote watarejea kwake.
jumasaidy2328@gmail.com / 0712172328
jumasaidy2328@gmail.com / 0712172328
kwa maswali,maoni na tiba kwa wanaosumbuliwa na majini.
No comments:
Post a Comment