#TIBA MBADALA
Tafiti mbalimbali za wataalamu wa lishe, zinaonyesha kwamba
uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka maradufu kama itachanganywa na
mdalasini.
Asali inafahamika kama chakula muhimu kinachosaidia kupambana na
magonjwa yatokanayo na uzee.
Tafiti mpya za wataalamu wa dawa lishe zimeonyesha kwamba asali
inafahamika vyema duniani kama ‘silaha’ ya kiajabu katika kupigana na magonjwa
mbalimbali.
Uchunguzi uliofanywa na jarida la World News kuhusu tiba, umeonesha
kuwa kuna umuhimu wa asali na mdalasini kuchanganywa pamoja.
Maumivu ya viungo vya mwili
Katika utafiti uliofanyiwa Chuo Kikuu huko Copenhagen, madaktari
waliwapa wagonjwa 200 wa maumivu ya mwili, mchanganyiko wa kijiko kimoja cha
asali na mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa.
Asilimia 73% ya wagonjwa hao walipata
nafuu ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli zao kama kawaida.
Kukatika kwa nywele
Asali ikishachanganywa na mdalasini
pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo cha kuotesha nywele.
Mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua
kichwani na kuachwa kwa dakika 15.
Ukungu wa miguuni (fangasi)
Kama una fangasi miguuni changanya
kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini (vya chai),
pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa
sabuni na maji.
Maambukizo kwenye kibofu cha mkojo
Chukua glasi ya maji ya vuguvugu
yaliyochanganywa na vijiko viwili vya mdalasini na kijiko kimoja cha asali ili
kuondoa bakteria kwenye kibofu. Kunywa mchanganyiko huu badala ya maji ikiwa
ambukizo la kibofu linakuwa sugu.
Mchafuko wa tumbo
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu
kama dawa inayofaa kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu.
Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii
tiba ya maajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
Kula asali pamoja na mdalasini kunaweza
kuondoa machafuko ya tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi
huko India na Japan.
Chunusi
Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja
na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bakteria
utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.
Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu wa
tiba mbadala.
jumasaidy2328@gmail.com/ 0787779285/0712172328 kwa matatizo mengine na pia ni tabibu kwa
wasumbuliwao na mapepo wachafu(mashetani )
No comments:
Post a Comment