Waziri Mkuu atangaza wanawake kuanza kupanda mabasi bure
Waziri Mkuu wa jimbo la Dheli nchini India, Arvind Kejriwal
siku ya jana alitangaza usafiri wa bure kwa wanawake wote wanaosafiri kwa
kutumia mabasi na treni za serikali.
Hatua hiyo inakuja baada ya visa vya kina mama kunajisiwa
ndani ya magari ya kibinafsi kuongezeka. Waziri Mkuu alisisitiza kuwa usafiri
wa umma ndio salama zaidi kwa wanawake wote.
Serikali ya India itatumia dola za Marekani Milioni 172 kila
mwaka kulipa nauli za wanawake hao, hata hivyo hatua hiyo imeonekana kuwa ya
kisiasa, kwa kuwa jimbo hilo linajitayarisha kupiga kura mwaka ujao.
No comments:
Post a Comment