KOCHA ALIYETIMULIWA UHISPANIA NA MADRID,KUINOA SEVILLA - waleo blog

Breaking

Tuesday 4 June 2019

KOCHA ALIYETIMULIWA UHISPANIA NA MADRID,KUINOA SEVILLA


Kocha aliyefukuzwa Uhispania na Real Madrid, ateuliwa kuiona Sevilla



Julen Lopetegui(52) amepewa kandarasi ya miaka mitatu kuinoa Klabu ya Sevilla ya Uhispania inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Alifukuzwa kuifundisha timu ya Taifa ya Uhispania siku mbili kabla ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 kuanza, baada ya kuteuliwa kuwa Kocha wa Real Madrid.

Mwezi Oktoba mwaka jana ikiwa ni miezi minne na nusu tangu ateuliwe kuinoa Real Madrid alitupiwa virango na Klabu hiyo kufuatia matokeo yasiyoridhisha hususani kipigo cha goli 5-1 kutoka kwa Barcelona.

Sevilla iliyomaliza ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo ilimfukuza aliyekuwa kocha wake, Pablo Machin mwezi Machi mwaka huu baada ya kutolewa kwenye michuano ya Europa na kumteua Joaquin Caparros hadi mwisho wa msimu.

No comments:

Post a Comment

Pages