📚 TABIA YA KUGHAIRISHA SEHEM 3⃣ - waleo blog

Breaking

Sunday 16 June 2019

📚 TABIA YA KUGHAIRISHA SEHEM 3⃣



#SAIKOLOJIA

Muendelezo.
➡ NJIA ZA KUDHIBITI KUGHAIRISHA KATIKA SABABU ZA KISAIKOLOJIA KUHUSU KUGHAIRISHA MAMBO.
Katika sehemu iliyopita tuliangalia sababu za kisaikolojia kuhusiana na tabia hiyo.
   ➡ Ili tuweze kuelewana vizuri katika sehemu hii ya tatu muhimu sana kuwa umeisoma sehemu ya pili.
         Njia za utatuzi zitazingatia kundi au aina saba (7) ya watu  katika tabia ya kughairisha.
 
AINA AU MAKUNDI SABA NA NJIA ZA UDHIBITI WA TABIA YA KUGHAIRISHA  MAMBO     
     Hiyo imefafanuliwa katika kitabu kijulikanacho kwa jina la vizuizi vya kughairisha ( Ant procrastination).
🌐 Tuangalie aina moja hadi nyingine na udhibiti wake
 1⃣ KUNDI AU AINA YA WATU WANAOPENDA KUFANYA VITU BILA KUJALI CHOCHOTE.
      Kwa kifupi hili ni kundi la watu wasio na vipaumbele katika maisha yao. Kwasababu hiyo ni rahisi sana kupoteza uvumilivu wanapo kosa au kuchelewa kupata matokeo na kupelekea kughairisha.

NJIA ZA UDHIBITI KATIKA KUNDI HILI
      Unachotakiwa kufanya ukiwa katika kundi hili hakikisha unaanza na kuendelea kuishi maisha yako Kwa malengo kwa kila unachofanya au kutaka kufanya.
➡ Jiulize lengo lako ni lipi unapofanya au kutaka kufanya jambo furani. Kuweza kuweka na kutimiza malengo itakuondoa kabisa katika tatizo hilo( elimu ya kuweka na kutimiza malengo itafundishwa).
2⃣KUNDI AU AINA YA WATU WANAOGHAIRISHA KWASABABU YA KUTOJUA HATUA ZA KUZIFUATA KATIKA KAZI AU JAMBO HUSIKA.
Watu hawa hupenda na fufanya vitu lakini hufanya bila kujua na kufuata njia sahihi katika kazi hiyo na kumpelekea kutofikia kiwango kikubwa cha matokeo,hiyo huwaumiza na kupelekea kukata tamaa na hatimaye kughairisha.

NJIA ZA UDHIBITI KATIKA KUNDI HILI
  1. Hakikisha kabda ya kuanza utekelezaji wa kazi husika anza kutafuta uelewa ( maarifa) ya kina kuhusiana na kazi hiyo.
2. Hakikisha unatengeneza na kuzingatia utekelezaji wa mpango kazi kwa kila wazo au kazi utakayoianzisha ( somo kuhusu mpango kazi litafundishwa).
3. Tafuta au jifunze kufanya kitu hicho kwa nza kwa vitendo.
 Mfano, Ukitaka kuwa mzungumzaji kwenye jamii jifunze na fanya mazoezi ya kutosha kabda ya kwenda kuzungumza ( somo litafundishwa).

3⃣ KUNDI AU AINA YA WATU WANAOGHAIRISHA KWASABABU YA KUSUBILI MPAKA MAMBO YOTE YAKAE VIZURI.
Utasikia nikipata fedha kiasi furani au nikiajiriwa nitafanya biashara furani.

NJIA YA UDHIBITI KATIKA KUNDI HILI
    Mara zote huchukua muda mrefu au isiwezekane kabisa kutimiza kila kitu ili kufanya jambo lako,hivyo hakikisha unaongozwa na kusudi ( dhamira) katika kufanya jambo lako.
     Anza na ulichonacho hapo ulipo( anza kidogo kidogo) kutimiza kusudi lako.

4⃣ KUNDI LA WATU WANAOJIONA WANAMAMBO MENGI KIASI CHA KUKOSA NAFASI YA KUFANYA MAMBO MENGINE.
     Mara nyingi hawa ni wale watu wanaona au kuzani kila kazi lazima wafanye wenyewe hawafikiri kukabidhi majukumu kwa watu wengine.

NJIA YA UDHIBITI KATIKA KUNDI HILI.
1. Tumia kanuni ya 80/20, kanuni ya Wilfred Pareto. Kanuni hiyo inasema, Fanya kazi ambayo itakupa matokeo ya 80% Kwa kuwekeza 20% ya nguvu na uwezo wako ( kanuni itafundishwa zaidi)
2. Tengeneza ratiba na hakikisha unaifuata. Chagua kazi tatu muhimu kila siku ambazo utazikamilisha.
3. Chukua siku 30 za changamoto.ieleweke tabia hiyo imejengeka kwa muda mrefu hivyo haitatoka kwa siku moja itachukua muda.
  Tengeneza mpango mkakati wa siku 30 Wa kujiondoa kwenye tabia hiyo kulingana na kundi ulilopo.

      Katika sehemu inayofuata tutamalizia somo kwa kumalizia aina tatu zilizobaki.
✳ Tuambie umejifunza nini mpaka tulipofikia.
       By
   Sixbeth Msita              🇹🇿 MSITA SUCCESS CLINIC🇹🇿
  0692786550

No comments:

Post a Comment

Pages