Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mama mjamzito
mimba yake kuharibika. Sababu kuu huwa ni magonjwa kama vile ugonjwa hatari wa
malaria, ugonjwa unaotokana na zinaa kama vile kaswende na kisonono na U.T.I,
dawa fulani fulani mfano Albendazole, Misoprostol, Metronidazole na kadhalika.
Lakini pia mjamzito akifanya kazi za kutumia nguvu nyingi
anaweza kusababisha mimba yake kuharibika. Lakini kuna sababu nyingi ambazo
zinasababisha mimba kutoka huweza kuzuilika kwa kwenda kliniki mapema yaani
pale tu unapohisi una mimba hata kama ni wiki mbili na kufuata ushauri wa
wataalamu.
Ukweli ni kwamba kuna wanawake wengi mimba zao huharibika na
wao hushindwa kugundua mapema na matokeo yake anakaa na mtoto mfu hata miezi
kadhaa bila kujua.
Zipo dalili ambazo husababisha mimba kuharibika kama
tutakavyoona leo hapa.
Dalili hizo ni hizi zifuatazo:
1. Kuwa na maumivu makali tumboni.
Ikiwa mjamzito atakuwa ana maumivu makali ya tumbo wakati ni
mjamzito hiyo pia ni dalili mbaya. Kwa kawaida maumivu makali ya tumbo hasa kwa
mimba kubwa ya miezi zaidi ya mitano au mimba ndogo kama mwezi mmoja, basi kuna
uwezekano mkubwa kondo imeanza kujiondoa kwenye kizazi kwa mimba kubwa au mimba
ndogo imeshindwa kuendelea kukua na moja kwa moja hiyo inaweza kuwa dalili ya
kuwa mimba imeharibika.
2. Mimba kutokukua
Ikiwa mimba itaacha kuongezeka au kukua ni dalili nyingine
ya mimba kuharibika. Kila mtu aliye mjamzito anategemea mimba iwe inakua kila
siku na iwe kubwa kulingana na umri unavyozidi
kwenda mbele, ikiwa mimba iko vilevile kwa miezi kadhaa, yaani haikui au ukubwa
wa tumbo haubadiliki ujue kwamba mimba hiyo imeharibika, ili kupata uhakika
wahi hospitali kupimwa.
3. Mtoto kuacha kucheza tumboni.
Ikiwa mtoto ataacha kucheza tumboni ni tatizo kubwa kwani
kwa kawaida mtoto huanza kucheza akiwa na wiki ya 18 mpaka 20 kwa wanawake
ambao hawajawahi kubeba mimba na wiki ya 16 mpaka 20 kwa wanawake ambao
wameshawahi kuzaa. Ikitokea mtoto aliye tumboni ameshawahi kucheza lakini
ghafla akawa hachezi au muda huo umepitiliza na bado kimya kuna uwezekano
mkubwa ikawa mtoto huyo amefia tumboni, hivyo haraka sana wahi hospitali
kumuona daktari.
4. Kutokwa na damu nyingi sehemu za siri.
Mjamzito akitokwa na damu nyingi sehemu za siri ni dalili
kwamba mimba imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza kufunguka, na hiyo
inaashiria kwamba kuna mambo mawili yameshatokea kwanza inawezekana mtoto
ameshafia tumboni au bado hajafa, lakini kama damu imetoka kwa wingi inaashiria
kuwa mtoto huyo aliye tumboni atakufa tu.
5. Kutoka na vipande vya vyame sehemu za siri.
Ikiwa mama mjamzito atakuwa akitokwa na vipande vya nyama
sehemu za siri ni dalili mbaya sana. Kutokwa na vipande vya nyama sirini ni
kuashiria kwamba kuna mtoto ameharibika tumboni. Hali hiyo ya hatari ikitokea
mjamzito anatakiwa asafishwe kuondoa masalio yaliyobaki.
6. Kupotea kwa dalili za ujauzito.
Kupotea kwa dalili za ujauzito ni tatizo lingine baya kwa
mama mjamzito. Mara kwa mara mwanamke akiwa na ujauzito anakuwa na dalili
nyingi kama vile kuwa na kichefuchefu, kukosa hamu ya kula baadhi ya vyakula,
kutapika, kulamba vitu vichachu kama vile limao, ndimu, wengine hula udogo na
wengi hubadilika sana tabia, hivyo basi dalili zote hizo za mimba zikisimama
ghafla basi ujue mimba imeharibika.
No comments:
Post a Comment