#UTALII
Hifadhi
ya taifa Mikumi ipo katika nchi ya Tanzania, mkoa wa Morogoro, wilaya ya Kilosa, mamlaka
ya mji mdogo wa Mikumi.Mbuga hii ya Mikumi imeanziswa
mwaka 1964.Neno Mikumi limetokana
na miti mingi aina ya Mikoche /Mkumbi [ Mikumbi] kwa
wingi,ambayo ilikuwa mingi
sana eneo husika.Kauli
mbali mbali zilisemekana kwamba
kutokea kwa neno mikumi ni matokeo
ya mzungu kushindwa kutamka
neno Mkumbi na kusema Mkumi,
na tangu hapo ndipo ikawa
sababu ya kutokea kwa
neno Mikumi.Mbuga hii ya ya mikumi ina
kilometa za mraba 3,,230
sq na ni hifadhi ya tano{ 5} kwa
ukubwa nchini Tanzania, na ya
kwanza ni hifadhi ya Ruaha ya pili Serengeti, Katavi na Mkomazi.
Katika hifadhi ya taifa mikumi kuna miti mbali
mbali ya asili, ndege na wanyama.Katika wanyama wanaojulikana kama big
five yaani Kifaru,Tembo,Simba,Chui
na Nyati. Katika hao big five hifadhi ya mikumi wapo wanne {4} tu yaani big four, ambao ni Tembo, Chui,Simba na
Nyati.
TEMBO
Tembo ndio mnyama
mkubwa duniani.Tembo wapo wa aina
mbili duniani ,yaani {a}
African Elephant (b) Asian
Elephant. Tanzania anapatikana wa aina
moja tu ambaye ni African Elephant..Tembo anaishi miaka 60-70 na Tembo mkubwa ana kilo 6000 dume na jike
kilo 4000.Lakini pia Tembo anashika
ujauzito miezi 22
hadi miaka 2 na mtoto
wake akimzaa anakuwa na kilo 120 hadi
150..
Tembo mkubwa kwa siku anakula majani kilo zisizo pungua 150-300.Tembo
pia katika masaa ishirini na nne [24] ya kila siku,
anatumia masaa 18
kula chakula usiku na mchana..
Tembo husumbuliwa na maadui zake wakuu 2.Ambao ni
binadamu na pia magonjwa..
INAENDELEA
#USISAHAU KUFUATA(FOLLOW
) BLOG YETU KWA HABARI NA MAKALA
MBALI MBALI.
Kwa maswali binafsi
kuhusu wanyama na shughuli za utalii
Piga simu no 0717475992/0782080716.
No comments:
Post a Comment