Baadhi ya nchi Barani Afrika zikiwemo Rwanda na Uganda
zimesherehekea Sikukuu ya Eid al-Filtr leo, Jumanne.
Mbali na nchi hizo, Waislam katika nchi za Somalia,
Ethiopia, Sierra Leone na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) nao
wameshiriki ibada ya Eid baada ya kukamilisha mfungo wa
Ramadhan.
Huko jijini Kigali, Sheikh Salim Hitimana amewaongoza
Waislamu katika sala maalumu iliyofanyika katika viwanja vya Nyamirambo.
Kwenye sala hiyo Sheikh Hitimana amewasihi Waislamu
kuendelea kutenda mema kama walivyokuwa wakifanya katika kipindi chote cha
Ramadhan.
“Nautakia Umma wa Kiislamu Eid Mubaraka, nawanasihi
waendelee na matendo ya upendo, kujikagua nafsi zao na kumcha Allah na kufanya
kazi kwa bidii kama walivyofanya katika kipindi chote cha mfungo,” amesema.
Kutokana na nchi ya Saudi Arabia kuwa nchi yenye ushawishi
mkubwa hasa linapokuja suala la muandamo wa mwenzi na kutangaza kuwa leo ni
Sikukuu ya Eid, baadhi ya Waislamu watasherehekea leo sikukuu hiyo, japo
mamlaka za nchi zao hazijatangaza Eid.
No comments:
Post a Comment