Kwa kutumia utafiti usio rasmi, utakubaliana nami kuwa
kumekuwa na mtazamo uliojengeka katika jamii kuwa mwanaume ukiwa umemuoa
mwanamke na kuwa mwili mmoja, basi una kila haki ya kumshika sehemu yoyote
uipendayo hasa wakati unahitaji kufanya nae tendo la ndoa.
Lakini utafiti na uzoefu uliokusanywa na wataalam wa
mahusiano na ndoa waliofanya mah
Kama ulikuwa haufahamu, nikujuze kuwa wanawake ni viumbe
wenye mlango mmoja wa ziada wa fahamu kuwapita wanaume. Hii nitaizungumzia siku
nyingine kwa urefu. Lakini mlango huu wa ziada ndio huwapa hisia ya ziada
pamoja na kuwafanya kujali sana vitu ambavyo mwanaume hasa mwenye haja ya
kufanya tendo anaweza asizingatie sana wakati anataka kukidhi haja yake.
Ukifuatilia sehemu hizi za mwili wa mwanamke nitakazozitaja
na nyakati zake, utabaini kuwa ni rahisi sana kubaini kuwa umegusa pasipo kwani
mwanamke katika nyakati hizo anaweza kuonesha kusita sana au hata kubadilika
kihisia.
1. Chuchu wakati miili yao inaendelea na shughuli nyingine
za ndani
Idadi kubwa ya wanawake huwa hawapendi kuguswa na wanaume
chuchu zao wakati wananyonyesha au wakati wako katika hedhi. Hiki ni kipindi
ambacho kama mwanamke ananyonyesha na mwanaume anataka kumgusa sehemu hiyo basi
maziwa yanaweza kutoka kwa kasi na kumfanya ajisikie hayuko ‘confortable’
kuendelea na zoezi la kushiriki tendo (kama hayuko hedhi).
2. Kwapani wanapokuwa wanatoka jasho
Wanaume wengine huwa na hisia za matamanio zaidi wanapoyaona
makwapa ya wake zao. Hii ni hali ya kisaikolojia inayojengeka kwa baadhi ya
wanaume. Kuna wanaume wakiona kwapa la mwanamke basi matamanio yao huongezeka
mara dufu. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hujisikia vibaya na kukosa
amani pale wanaume zao wanajaribu kuwashika kwapani wakati ambapo wametokwa
jasho.
3. Sehemu za siri kabla ya kuoga
Hili ni eneo ambalo wanawake wengi wameonesha kuwalalamikia
waume zao. Kwa mazoea wanaume wengi huwa kama wanawabaka wake zao bila
kufahamu, hasa pale wanapotoka safari zao wakiwa na matamanio. Lakini wanawake
wengi wameeleza wazi kuwa hupoteza hali ya kuwa ‘comfortable’ pale wanapoguswa
na wanaume zao sehemu za siri wakati bado hawajaoga.
Wanaume wengi hujikuta wakishiriki tendo la ndoa na wake zao
ghafla baada ya kukamilisha kazi kadhaa za ndani wakati wanawaangalia. Wanaume
wanaweza kuwa wanafurahia zaidi tendo hilo lakini wanawake pamoja na kwamba
hufurahia pia lakini mlango wao wa ziada wa fahamu huwafanya kukosa amani kwa
kiasi fulani wakati wa tendo ukilinganisha na nyakati ambazo wanajiamini ni
wasafi.
4. Nywele zao dakika chache baada ya kutoka saloon kujiremba
Ingawa unaamini kuwa mkeo alienda saloon kujiremba kwa ajili
ya kukuvutia wewe, usithubutu kutaka kuzivuruga nywele zake dakika chache baada
ya kutoka kwa mtaalam wa kutengeneza nywele, hata kama pesa aliyotumia ulimpa
wewe.
Hiki ni kama kituko hivi, lakini ndio ukweli. Wanawake
hutumia muda mrefu sana kwenye vibanda au saloon za gharama kwa ajili ya
kujiremba ili waongeze mvuto. Lakini, hugeuka kuwa walinzi wa vichwa vyao
angalau kwa saa kadhaa. Msifie uwezavyo, lakini nywele zake usizivuruge mapema
mtaharibiana ‘mood’.
Haya ni kati ya mambo machache ambayo wanaume huyaona madogo
sana na kufuatilia yale wanayoamini ni makubwa zaidi. Lakini mambo haya ni kati
ya machache yanayokwangua taratibu kuta za hisia za mwanamke kwa mumewe.
No comments:
Post a Comment