DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOONYESHA JEURI YA FEDHA - waleo blog

Breaking

Wednesday 5 June 2019

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOONYESHA JEURI YA FEDHA



Wakati joto la show ya Kahama likizidi kupanda , the Bongo Fleva finest  Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz ameendelea kuonyesha jeuri ya fedha alizokuwanazo kwa kufanya matumizi au tunaweza uhita uwekezaji mkubwa katika show yake hiyo ya leo ya Kahama.

Tumekuchambulia dondoo tatu muhimu kuonyesha jinsi alivyoonyesha jeuri hiyo hapa chini


KUKODISHA HELCOPTER KWA SHILINGI MIL 31.

Ili kuwapa radha mashabiki zake wa Shinyanga ambapo anarudi kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka saba kufanya show siku ya jana alikodi  helicopter kwa zaidi ya shilingi milioni 31 akizungumza na waandishi wa habari Dimaond amesema amefanya hivyo ili kukutana na mashabiki zake kwa karibu zaidi.


Katika uchunguzi wetu tumebaini Helicopter hiyo imekodishwa kutoka kampuni inayofanya shughuli za  Utafutaji na Uhokoaji ya Kilimanjaro Search and Rescue (SAR) Limited  ya mkoani Kilimanjaro inayofanya kazi za uokozi kwenye milima ya Kilimanjaro na Meru.


KUSAFIRISHA TEAM YAKE YA ZAIDI YA WATU 100 NA GHARAMA NYINGINE

Hii kama sio jeuri ya fedha ni nini? Je kuna msanii yoyote bongo alishwahi kufanya hivi ? Jibu ni moja tu ni mtoto wa tandale pekee. Babu Tale moja ya meneja wa msanii huyo akizungumza na waandishi wa habari amesema wamesafirisha zaidi ya watu 100 wakiwemo madancer, djs,characters, mamodel ,walinzi wake, crew ya Wasafi TV, Wapiga picha, wanamuziki wa band, waandishi na mastylist kama Noel n.k

Licha ya usafiri wa ndege kutumika kwa baadhi ya wanateam pia usafiri wa magari ya kukodi na binafsi  yaliyofanyiwa branding maalumu kwa ajili ya show hiyo yametumika kusafirisha vifaa vya bendi, wanabendi wenyewe na waandishi wa habari . Na brand ya gari maalumu la show hiyo limefanyawa na kampuni ya One Mic Tanzania ya Azma Mponda ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva.

Waswahili wanasema mkono mtupu haulambwi huwezi tu kusafirisha team bila kuwapa kidogo kitu hebu tupige tu hesabu za haraka haraka just imagine ni kiasi gani msanii huyo alichokitumia kwa watu hawa?Kuwasafirisha, kula , kulala na pesa za matumizi njiani? Kwasasa hatuna kiasi rasmi alichotumia msanii huyu kuwalipa team yake tunakuahidi kulichimba hili kwa undani na kukuletea exactly figure.

Kama hii sio jeuri ya fedha ni nini?Mashabiki wa msanii huyo mjini Shinyanga walioga mapesa aliyokuwa anarusha msanii huyo kwa mashabiki zake waliofika kumshangilia alipokuwa anapita njiani. Kwanza kabisa alishare ratiba yake atakapopita kupitia akaunti yake rasmi katika mtandao  kijamii wa instagram                                         
          Na hivi ndivyo msanii huyo alivyotoa mkono wa Idd kwa mashabiki zake na kama hii sio jeuri ya fedha alizonazo msanii huyu ni nin na je ni ipi faida yake.   Usahau kutufollow,comment na kushare

No comments:

Post a Comment

Pages