Wanapokuwa watu wawili kwenye mahusiano, lengo lao linakuwa
ni moja ambalo ni kupendana. Lakini kuna misunderstanding ambayo huwa hahikosi
kwa wawili hawa hata kama ni wakamilifu kiasi gani. Cause no one who is perfect
always!! Ila kuna jambo ambalo huwa lipo katikati yao pia ambalo ni kuelewana,
na safari inaendelea.
Kwenye mapenzi kuna njia tofauti ambazo zinaweza kuonekana
kutatua migogoro inayojitokeza ikiwa ni pamoja na kutumia washauri, lakini kuna
dawa moja kubwa sana katika mahusiano na mapenzi kama to say am sorry, samahani
ni neno dogo sana lakini matokeo yake ni makubwa sana.
Kusema samahani haimaanishi wewe ni mjinga, au hauna akili
au wewe ndio ni mwenye makosa.
Samahani inapunguza mabishano na maneno mengi, inarudisha
maelewano ndani ya nyumba.
Inahitaji moyo husiobeba visasi, ina maana kutopiliza kisasi
kwa lililotokea hapo awali.
Lakini kwa kuliongelea swala hili ni rahisi sana lakini kwa
kulitenda ni vigumu sana, fikiria kama wewe ndio umemkosea mpenzi wako alafu
pale pale wewe ndio uombe msamaha,
unafikiri hilo ni rahisi kufanyika? Na vipi kama wewe
umekosa na ukaomba msamaha husisamehewe utafanya nini? Will u walk out?? Na ni
mara ngapi umetumia neno samahani kwa siku? Na je mahusiano yanaweza kudumu
bila samahani??
Bila shaka hakuna mahusiano yanayoweza kudumu bila kujua
thamani iliyopoa katika neno samahani, hivyo kusema samahani ni muhimu sana
katika mahusiano ili kulifanya penzi lenu liwe bora zaidi.
No comments:
Post a Comment