Klabu nyengine za England ambazo zinamuwania Samatta ni
Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza Samatta ana
thamani ya Pauni milioni 12.
Samatta ambaye bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake na
mabingwa wa Ubelgiji KRC Genk pia amezivutia klabu za Roma ya Italia na Lyon ya
Ufaransa.
Mshambuliaji huyo ambaye aliongoza kwa kupachika mabao msimu
uliopita nchini Ubelgiji ameweka wazi kuwa anataka kuelekea nchini England
msimu ujao.
"Kwa sasa hivi siwezi kusema sana, ni kitu ambacho kipo
kwenye mchakato nasubiria kitakapokuwa tayari na wakati utakapofika nitaweza
kukizungumza. Lakini sijioni tena Genk, namuomba Mwenyezi Mungu litimie, lakini
ikishindikana bado nina mkataba na Genk," aliiambia Azam TV.
Klabu ya Brighton imekuwa ikimfuatilia Samatta kwa muda
mrefu na kocha wa timu hiyo kwa msimu uliopita Chris Hughton alikuwa akivutiwa
sana na mchezaji huyo.
Kocha mpya wa klabu hiyo Graham Potter pia anavutiwa na
uwezo wa Samatta.
Samatta ni nahodha wa Tanzania kwa sasa yupo kambini na timu
ya Taifa Stars wakijiandaa na michuano ya bara la Africa (Afcon 2019)
yatakayofanyika nchini Misri mwezi huu.
FOLLOW,COMMENT,SHARE USIPITWE NA HABARI MPYA
No comments:
Post a Comment