KUGHAIRISHA MAMBO - waleo blog

Breaking

Wednesday, 29 May 2019

KUGHAIRISHA MAMBO




LENGO LA MADA:
     Kumuwezesha msomaji Wa makala hii kudhibiti tabia ya kughairisha mambo
SEHEMU YA 1⃣
Kughairisha ni tabia ya kutofikia mwisho wa wazo au kazi uliyoianzisha.
➡Kwa mujibu wa tafsiri hiyo kughailisha kumegawanyika katika aina kuu mbili,ambazo ni,
1⃣ Kughairi kwa kuwaza tu na kutofanya kabisa.
       Katika aina hii mtu anawaza kutaka kufanya jambo fulani lakini mwisho wa siku hafanyi chochote.
2⃣ Kughairi Mara baada ya kuanzisha jambo furani.
      Katika aina hii mtu anaanza kufanya jambo furani na kabda ya kufika mwisho analiacha labda kwa sababu furani furani.

SABABU ZA TABIA YA KUGHAIRISHA
      ➡ Utafiti unaonesha 99% ya watu wasiofanikiwa kufikia kiwango cha juu husababishwa na tabia hiyo ( kwa mujibu wa kitabu cha George Washington).
Hiyo tafsiri yake ni kwamba watu wengi wanaathiriwa na tabia hiyo ya kughairisha mambo.
➡ Watu wote waliofanikiwa ni wale walioweza kuendelea kufanyia kazi mawazo yao bila kujari magumu wanayopitia,pia adui mkubwa wa mafanikio ni tabia ya kughairisha mambo unayowaza au kuyafanya ( kwa mujibu wa kitabu cha sayansi ya tabia).
      Sababu kubwa ya watu Kughairi ni kupenda kuwaza, kuangalia na kufanya vitu kwa sura ya nje.
Maana yake ni kwamba unasikia au kuwaza au unaona jambo Mara Moja unahamasika kutaka kulifanya jambo hilo.
📖 Swali la msingi hapo kwanini watu wanawaza,wanaangalia na kufanya vitu kwa sura ya nje.
Majibu ya swali hilo yanapatikana katika Utafiti wa,
1⃣ KISAYANSI
2⃣ KISAIKOLOJIA.

1⃣SABABU YA KISAYANSI KUHUSU KUGHAIRISHA MAMBO
   Sababu hiyo ni kwa mujibu wa Utafiti ulioandikwa katika kitabu cha SAYANSI YA TABIA, na hapo tutaangalia tabia hiyo ya Kughairi.pia kwa mujibu wa walimu,wahamasishaji na waandishi wa vitabu mbalimbali.
📖 Huu ni Utafiti uliofanywa na wanabaiolojia kuhusiana na ubongo wa binadamu.
       Wanabaiolojia wanasema katika ubongo kunamifumo miwili inayohusiana na tabia na maamuzi (mifumo hiyo inahusiana na tabia na maamuzi yote,mabaya na mazuri).
Mifumo hiyo inajulikana kama,
1. Pre- cortex system na
2. Basal ganglia system.
Mifumo hiyo hufanya kazi kwa kukinzana katika maswala ya tabia na maamuzi.
📚 pre- cortex system kwa kawaida huzaliwa nao ukiwa umelala na hukomaa kati ya miaka 5-25 kwa baadhi ya watu.Mfumo huo huusika na matendo au tabia isiyo ya kawaida kama vile,
➡Maono,Njia na maamuzi sahihi,
➡Mitazamo,imani,malengo na kuchukua hatua stahiki.
  Mfumo huo ili ukomae au ufanye kazi unakuhitaji wewe uushughurishe au uamulu unataka ukufanyie nini.Unaposhindwa kuushughurisha mfumo huo kwa nguvu na weredi mkubwa utatawaliwa na mfumo huo mwingine,ambao ni
📖BASAL GANGLIA SYSTEM.
Basal ganglia system ni mfumo unaozaliwa nao ukiwa umekomaa kabisa na upo tayari kwa kufanya kazi. Mfumo huo unakijisehemu kijulikanacho kama kijisehemu cha raha au furaha ambapo sehemu hiyo huzalisha kemikali zinazoelekeza mwili na akili katika matendo,mawazo,na vitu vya raharaha au furaha.
  Sasa kwasababu ya kutawaliwa na mfumo huo ambao umezaliwa ukiwa  umekomaa ndio maana watu weng hupenda kuwaza, kuona na kufanya vitu kwa sura ya nje. mfumo huo unahakikisha hauruhusu akili wala mwili kuingia katika vitu vitakavyokupa nafasi ya kuwaza au kufanya vitu vya mafanikio kwasababu vitu hivyo vinakuhitaji uumize akili ili uwezekufikia
NINI UNAPASWA KUFANYA ILI UWEZE KUUTUMIA MFUMO WA PRE-CORTEX DHIDI YA BASAL GANGLIA SYSTEM. 
   Utafiti unaonesha pre-cortex  pamoja na kuwa unazaliwa ukiwa haujakomaaila unanguvu kuliko huo mwingine kama ukiupa kazi ya kuifanya (kuupa mazoezi ya kufanya kazi). Hiyo ni kama ilivyothibitiswa na  vitabu mbalimbali vya sayansi , kwamba ubongo wako unauwezo mkubwa kama utaupa kazi ya kufanya >ili mfumo huo ufanye kazi unakuhitaji ufanye kwa umakini na uangalifu mkubwa mambo yafuatayo  1.Uoneshe mfumo huo unatakakufanya jambo gani. Hapo mfumo utaanza kutafsiri hilo jambo au kazi husika.
2.Uambie au uweke malengo (smart goal) mahususi yenye makusudi ya kutatua jambo fulani, hapo mfumo utaamka kwasababu unaona kunajukumu la kufanya ambapo linatakiwa lifanyikekazi.
3.Tengeneza mpango kazi na taratibu ya utekelezaji wa jambo husika.  
      Najua ni changamoto kwa watu wengi kutengeneza malengo, mpango kazi, pia wapo wanaoweza kutengeneza hivyo  vyote lakini hawawezi kuvizingatia.
Kwa kuzingatia utafiti mbali mbali  tutafundisha vitu vyote hivyo na namna ya kutofuata utekelezaji wa malengo tuliyojiwekea.
Kimsingi hiyo ndio sababu ya kisayansi na namna unavyoweza kuidhibiti tabia ya kughairisha mambo kwa mujibu wa sababu ya kisayansi
Katika sehemu inajayofuata tutaangalia
UTAFITI WA KISAIKOLOJIA KUHUSU TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO.
ISHI MAISHA YAKO KWA UHURU  NA FURAHA
                                                     BY   SIXBETH MSITA 
               CALL:0692786550 

                                  MSITA SUCCESS CLINIC

No comments:

Post a Comment

Pages