NDEGE ILIYOWAHI KUPOTEA KIMIUJIZA - waleo blog

Breaking

Monday 20 May 2019

NDEGE ILIYOWAHI KUPOTEA KIMIUJIZA


Tarehe 22 july, 1955 Pan american ilianza safari yake kutoka New york kuelekea Miami ikiwa na wafanyakzi 4 na abilia 57. lakini chaajabu katikati ya safari ndege hiyo ikapoteza mawasiliano na haikuwahi kuonekana tena tangu hapo wala haikufika miami kama ilivyokua safari yake.
Na hakuna aliyejua ilikuaje hadi Ndege hiyo ikapoteza mawasiliano na haikuwahi kuonekana tena hadi miaka 37 mbele ndio Ndege hiyo ikatua nchini Venezuela katika mji wa Caracas tarehe 21 july,1992.
Kutua kwa ndege hiyo kulikua kwa kushtuza sana maana hata Rada za Caracas hazikuiona kabisa kitu kilichofanya Co-Workers of control kuhoji imekuaje ndege hiyo haikuonekana kwenye mitambo yao. Mfanyakazi mmoja kwa jina la Juan de la corte ambaye ndiye aliyeshudia vizuri tukio hilo akamuuliza Pilot wa ndege ile ya Pan American Flight 914, "Vip ww mbona umetua hapa?" .
Akiwa na maana labda Rubani alikosea kiwanja cha kutua na ndege hii ni ipi? Inatoka wapi na ilikua inaelekea wapi wakidhani imetua kwa dharura. Hata hivyo Sio wao tu maana hata Pilot wa Pan American pia alishangaa baada ya kuona watu wa hapo sio wamarekani (Miami) kama alivyozoea na maswali waliyomuuliza ni kama kweli alitua uwanja ambao sio sahihi.
Ikabidi aulize, "Kwani tuko wapi hapa na nini kimetokea?" Wakamwambia, hapa ni Caracas Venezuela na leo ni 21may,1992. Pilot akabaki mdomo wazi akisema, Mungu wangu hii ndege ilipaswa kutua mjini Miami mda wa saa 03:55 22july,1955.

3 comments:

Pages