Inatoka ukurasa uliopita(mwendelezo)
Mitaala
Somo la taaluma ni tawi la elimu ambalo
hufunzwa rasmi katika vyuo vikuu ama kupitia njia zingine kama hizo. Kwa
kawaida, kila somo huwa na masomo mengine ama matawi na mipaka ya kuyabainisha
mara nyingi huwa si dhahiri na na mara nyingine husababisha utata. Mifano ya
masomo ya kitaaluma yenye upana ni kama vile sayansi asilia, hesabu, sayansi ya
komputa, sayansi za jamii, sayansi za binadamu na sayansi za matumizi.
Kwa wakati huu, kugawika kwa elimu
katika mitindo tofautitofauti hukubalika na wengi. Huenda ikawa kuwa mitindo ya kujifunza ndiyo ya kawaida.
·
Kuona: Masomo yenye
misingi ya kutazama kwa makini na kuona kile kinachosomwa.
·
Kusikiza: Kusoma kwa
misingi ya kusikiliza maelezo/habari.
·
Masomo husishi: Kusoma
kwa misingi ya kutumia mikono na vitendo husishi.
Imedaiwa kuwa kulingana na mtindo wa
kujifunza unaopendelewa kwa mbinu tofautitofauti za kufunza huwa na matokeo ya
viwango tofauti. Umuhimu wa nadharia hii ni kuwa kunakofaa na inapaswa
kutumia mbinu mbalimbali za kufunza zinazojumlisha mitindo yote mitatu ya
kufunza ili wanafunzi tofautitofauti wapate fursa ya kujifunza kwa njia
inayowafaa.
Kujifunza
Kujifunza ni kutaka kujua juu ya jambo
fulani ambalo hukulijua kabla. Hata jambo zuri kuhusu kujifunza ni kwamba
hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kukiweka mbali nawe kitu hicho ambacho
umejifunza.
Walimu wanapaswa kuelewa somo vilivyo
ili kuwasilisha umuhimu wake kwa wanafunzi. Shabaha hapa ni kuunda misingi ya
ujuzi kamili ambayo wanafunzi wanaweza kutumia kujijenga zaidi kwani wamewekwa
wazi kwa matukio mbalimbali ya maisha. Walimu wazuri huweza kutafsiri habari
kama hukadiria vizuri, hutumia mazoea na hekima hadi kwa elimu husika ambayo
mwanafunzi anaweza kuelewa, kuhifadhi na kupititishia wengine.
Utafiti kutoka Marekani unatoa maoni
kuwa ubora wa walimu ndio kigezo kinachoathiri mafanikio ya wanafunzi, na kuwa
nchi zinazopata alama za juu katika mtihani au majaribio ya kimataifa zimeweka sera chungu
nzima zinazohakikisha kuwa walimu wanaoajiriwa ndio bora.
Teknolojia ni kigezo muhimu katika elimu. Tarakilishi/kompyuta na rununu yaani simu za mkononi zinatumiwa katika nchi
zilizoendelea kuimarisha elimu iliyothibitishwa na kukuza njia mpya za elimu
kama vile elimu ya mtandao (masomo ya mbali). Wanafunzi hupata fursa ya
kuchagua wanachotaka kusoma.
Kuenea kwa tarakilishi pia kunamaanisha
kuongezeka kwa programu za kompyuta na kuongeza habari mtandaoni. Teknolojia
hutoa vifaa muhimu vinavohitaji ujuzi mpya na uelewa wa wanafunzi zikiwemo njia
nyingi za mawasiliano, na huleta njia mpya za kuhusisha wanafunzi kama vile
mazingira ya kujifunza.
Teknolojia inatumiwa si tu katika
wajibu wa kutawala katika elimu bali pia katika kuwaelekeza wanafunzi. Matumizi
ya teknolojia kama vile virusha maandishi (power point) na ubao mweupe hutumiwa
kunasa akili za wanafunzi darasani. Teknolojia vilevile hutumiwa kuwatahini
wanafunzi. Mfano mzuri ni mfumo wa kuvutia hadhira (ARS),ambao huruhusu majibu
ya mitihani moja kwa moja pamoja na majadiliano darasani.
Teknolojia pia imekuwa mojawapo wa
maktaba katika elimu ambamo vitabu, ripoti za utafiti, n.k. huchapishwa. Tovuti
zinazochapishwa vitabu, ripoti na tansifu zimekuwa na manufaa kwa wasomi.
Zinawapa uwezo wa kupata vitabu maalum kwa ujumbe fulani tofauti na maktaba za
kizama ambazo humlazimu mtu kusoma kwa urefu na upana kupata ule ujumbe. Tofuati
hizi hufuata mpangilio, mwingine zikiruhusu watumizi kupakua vitabu bila
malipo, nyingine zina malipo ya muda, il-hali nyingine hulazimu mtu kununua
kile kitabu anachokihitaji.
Teknolojia za habari na mawasiliano (ICT)
ni seti ya vifaa na rasilimali mbalimbali zinazotumiwa kuwasiliana, kuunda,
kueneza na kuongoza habari. Teknolojia hizi ni pamoja na kompyuta, mtandao,
teknolojia za kusambaza habari redio na
televisheni, simu kuongea na pia kwa ujumbe
wa maandishi yaani (sms).
Kuna mvuto unaoongezeka kuhusu namna tarakilishi na mtandao vinavyoweza
kuimarisha elimu katika viwango vyote, yaani mseto wa elimu rasmi na ile isiyo
rasmi.
Teknolojia za habari na mawasiliano za
awali, kama vile redio na televisheni, zimetumiwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa elimu wazi na ile
ya mbali, hata hivyo kupiga chapa ndiyo njia nafuu zaidi, inapatikana kwa
urahisi, na hivyo basi ni mbinu iliyotawala katika nchi zilizoendelea na zile
zinazoendelea.
Matumizi ya tarakilishi na mtandao
(ikiwa vinatumika) bado ni changa katika nchi
zinazoendelea, na hii ni kwa
sababu miundo msingi ni michache na ghali. Kwa kawaida teknolojia kadhaa
hutumiwa kwa pamoja bali si mbinu pekee ya kupokelewa. Kwa mfano, Kothmel
Community Radio Internet hutumia matangazo ya redio na kompyuta pamoja na
teknolojia ya mtandao, na hivyo hurahisisha kugawa habari na kutoa nafasi za
elimu katika kijiji fulani Sri Lanka.
Chuo Kikuu cha Uingereza (UKOU) kilichoanzishwa mwaka wa 1969 kama taasisi ya elimu ya kwanza ulimwenguni
kujitolea kutoa elimu ya wazi na ya mbali, bado hutegemea vifaa vilivyopigwa
chapa na kuongezea redio, runinga na kompyuta. Vivyo hivyo, Chuo Kikuu cha
Indira Gandhi
nchini India huweka pamoja matumizi ya chapa, sauti zilizorekodiwa,
video, redio na teknolojia ya vielezo vya kusikiza mkutano.
Dhana ya masomo yanayosaidiwa na
kompyuta (CAL) limetumiwa kwa
wingi kuelezea teknolojia katika masomo.
Nadharia ya elimu
Nadharia ya elimu ni nadharia ya azma,
matumizi na ufafanuzi wa elimu na kusoma. Historia yake inatokana na wataalamu
wa elimu kutoka Ugiriki kuanzia karne
ya 18. Katika karne ya 20 mbinu za kusoma
zimetumia nadharia katika kufunza, kutathmini na katika sheria za elimu ambazo
hupatikana katika vitengo mbalimbali kama ifuatavyo:
Uchumi
Sababu zimetolewa kuwa kiasi cha juu
cha elimu ni muhimu kwa nchi ili kuwezesha ukuaji haraka wa uchumi. Uchunguzi unaotegemea nadharia huunga mkono nadharia za
kutabiri kuwa nchi
maskini zinapaswa
kukua haraka kuliko nchi
tajiri kwani
nchi hizi zinaweza kutumia teknolojia mpya kabisa ambayo imeshajaribiwa na nchi
tajiri.
Hata hivyo, kuhamisha teknolojia
kunahitaji viongozi wenye maarifa na wahandisi wenye uwezo wa kutumia mashine mpya ama mazoezi ya uzalishaji yaliyokopwa ili
kuziba mpaka kwa miigo. Hivyo basi, uwezo wa nchi wa kujifunza kutoka kwa nchi
kiongozi ni jukumu la wafanyakazi wa nchi hiyo.
Utafiti wa hivi karibuni wa
vitambulishi vya kujumuisha ukuaji wa kiuchumi umesisitiza umuhimu wa vyuo
asili vya uchumi na majukumu ya ujuzi tambuzi.
Kazi hii imetia motisha idadi kubwa ya
utafiti lakini pia inaelekea kuleta mabishano kwa kiasi fulani. Ubishi mkubwa
unahusu jinsi ya kufasiri matokeo ya kusoma.
Saikolojia
ya elimu ni
uchunguzi wa jinsi watu hujifunza katika mandhari ya elimu, maingiliano ya
elimu, saikolojia ya kufunza na saikolojia ya jamii za shule. Ingawa maneno “saikolojia ya
kielimu” na “saikolojia ya shule“ mara nyingi hutumiwa kwa kubadilishana, watafiti
na wananadharia wanaweza kutambuliwa kama wanasaikolojia wa elimu, il-hali
weledi wanaopatikana shuleni au mandhari yanayoana na shule hujulikana kama
wanasaikolojia wa shule. Saikolojia ya elimu inajishughulisha na utaratibu wa
kutoa elimu kwa watu na umma kwa jumla na umma mdogo, kama vile watoto wenye
vipaji na wale wenye ulemavu.
Saikolojia ya elimu inaweza kueleweka
kwa sehemu kupitia masomo mengine. Saikolojia ya elimu vilevile huarifiwa na
saikolojia, ikileta uhusiano baina ya utabibu na biolojia. Saikolojia ya elimu pia huarifu masafa mapana ya masomo
maalum yakiwemo mpango wa mafunzo. Teknolojia ya elimu, mtaala uliokuzwa,
masomo yaliyopangwa, masomo maalumu, sayansi tambuzi na sayansi masomo. Katika
vyuo vikuu, idara za elimu ya saikolojia zimehifadhiwa katika vitivo vya elimu.
Hii ni kwa sababu ya uwezekano wa ukosefu wa uwakilishaji wa maudhui ya
saikolojia ya elimu katika utangulizi wa vitabu vya saikolojia.
Sosholojia ya elimu; ni somo linalohusu jinsi taasisi za kijamii na huathiri michakato
na matokeo ya elimu kinyume chake. Kwa
wengi, elimu hueleweka kama mbinu ya kushinda vizuizi, kufanikisha usawa na
kupata amani na hadhi kwa wote (Sargent 1994). Wanafunzi
wanaweza kutiwa motisha na hamu ya maendeleo na uboreshaji. Elimu hutambuliwa
kama mahali ambapo watoto huweza kujikuza kulingana na mahitaji yao ya
pekee. Jukumu la elimu linaweza kuwa ni kukuza mtu binafsi hadi kilele.
Uelewa wa shabaha na mbinu za michakato ya utangamano wa kielimu hutofautiana
kulingana na dhana ya sosholojia iliyotumika.
Katika nchi
zinazoendelea idadi na
uzito wa shida zilizoko kwa kawaida ni kubwa. Watu wa vijijini wakati mwingine
huwa hawana habari kuhusu umuhimu wa elimu. Hata hivyo, nchi nyingine
zina wizara
ya elimu na katika
masomo mengi, kama vile kujifunza lugha za kigeni, kiwango cha elimu kimo juu
kuliko katika nchi zilizoendelea. Kwa mfano, katika nchi zinazoendelea ni
kawaida kupata wanafunzi wakizungumza lugha nyingi za kigeni kwa usanifu
mkubwa, il-hali jambo hili ni nadra katika nchi
zilizoendelea ambapo
idadi kubwa ya watu huzungumza lugha moja.
Vilevile kuna shinikizo la kiuchumi
kutoka kwa wazazi ambao hupendelea watoto wao wapate pesa kwa muda mfupi kuliko
faida za elimu ya muda mrefu. Utafiti wa hivi karibuni kuhusu ajira ya watoto
na umasikini zimependekeza kuwa familia zilizokumbwa na umasikini zinapofikia
kiwango fulani cha kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, wazazi huwarejesha watoto
wao shuleni. Hii imethibitshwa kuwa kweli mara tu kizingiti kinapovukwa. Hata
kama uwezekano wa thamani ya kiuchumi ya ajira ya watoto inaongezeka baada yao
kurudishwa shuleni.
Ukosefu wa vyuo vikuu bora na kiwango
cha chini cha kukubalika katika vyuo hivi ni dhahiri katika nchi zilizo na
idadi kubwa ya watu. Baadhi za nchi zina mitaala mikuu inayoweza kubadilika kwa
urahisi, inayofanana na yenye miundo zaidi.
·
Kutokana na utandawazi shinikizo kwa wanafunzi katika
shughuli za mtaala zimeongezeka
·
Kuondolewa kwa asili mia fulani ya wanfunzi kwa ajili ya
uboreshaji wa masomo; kwa kawaida hufanywa shuleni baada ya daraja la kumi.
India inakuza teknolojia na mtandao.
India ilizindua EDUSAT, elimu ya
setilaiti ambayo inaweza kuwafikia wengi kwa gharama ya chini. Kuna pia mpango
ulioanzishwa na shirika la OLPC, kundi lililotokana na maabara ya MIT
lililoungwa mkono na mashirika makuu ili kukuza kompyuta ya kupakata ambayo
ingeghalimu $100, ili kuwezesha
kuwasilisha elimu ya programu ya kompyuta. Kompyuta hizi zimesambaa kote
kufikia mwaka wa 2009. Kompyuta hizi zinauzwa au kutolewa kama msaada. Hii
itawezesha nchi zinazoendelea kuwapa watoto wao elimu kwa kutumia mitambo.
Barani Afrika, shirika la NEPAD
limezindua programu ya masomo ya mtandao inayotoa vifaa vya kompyuta na masomo
ya mtandao kwa shule zote za msingi na upili kwa kipindi cha miaka kumi.
Vikundi vya binafsi kama vile Wamormoni, wanajikakamua kuwapa watu fursa ya kupokea elimu katika
nchi zinazoendelea kupitia miradi kama vile Perpetual Educational Fund. Mradi
wa maendeleo kimataifa inayofahamika kama nabuur.com, com iliyoanza kwa msaada wa rais
wa Marekani Bill Clinton, hutumia mtandao kuwezesha ushirikiano wa watu binafsi
kuzungumzia maswala ya maendeleo ya jamii.
Elimu inaendelea kuwa jambo la
kimataifa. Si vifaa vyake tu vinavyoendelea kuathiriwa na mazingira ya
kimataifa yenye ukwasi bali pia mabadiliko ya wanafunzi katika viwango vyote
yanayochangia kuendesha jukumu hili muhimu. Kwa mfano kule Uropa, programu
ya Socratis Erusmus imechechemua mabadilishano kati ya vyuo vikuu vya Uropa.
Vile vile, Shirika la Soros hutoa fursa nyingi kwa wanafunzi kutoka
Asia ya kati na Uropa mashariki. Wasomi wengi hudai kwamba ingawa mfumo fulani
unaweza kuzingatiwa kuwa bora au mbaya kuliko mwingine, kuzoea aina tofauti ya
elimu mara nyingi huonwa kuwa elementi muhimu ya kuzoea masomo ya kimataifa.
Dini na elimu
Elimu katika dini ya Uislamu ni muhimu kwa wake na waume.Kinyume na dhana ya
kawaida, kutafuta aina zote za maarifa, yawe ya kitaaluma, ya kidini au ya
kidunia yanaruhusiwa kwa watu wa umri wowote. Hata hivyo, masomo ya umri mdogo
huonwa kuipa akili fursa ya kumakinika bila kuathiriwa na shida na majukumu ya
maisha ya utu uzima.
Moja ya maandiko katika Bibilia yana
sema,”Mkamate elimu usimwache aende
zake”. Methali
Kwa maoni, ushauri na chochote kile ukifikiriacho usisite
hapa;;;;;;;;;;
+255767611645
+255715080716
Mwanaharakati1992@gmail.com.
No comments:
Post a Comment