#UTAWALA
Maana ya kitongoji /mtaa.
Kitongoji ni sehemu ya kijiji, mamlaka ya mji mdogo au mamlaka ya mji.
Eneo la kijiji linatakiwa kugawanywa katika vitongoji visivyozidi vitano kulingana na idadi ya kaya na jiografia ya eneo husika.
Mkutano wa wakazi na kitongoji
Mkutano wa wakazi wa kitongoji unahudhuriwa na wakazi wa
kitongoji wenye umri wa kuanzia miaka 18 na
kuendelea. Mkutano wa kitongoji una mamlaka ya kumchagua na kumwondoa mwenyekiti wa
kitongoji”kisheria”. Mkutano wa kitongoji hufanyika mara moja kila mwezi ili
kujadili ustawi na maendeleo ya
kitongoji. Ila unaweza kuitiswa na mwenyekiti wa kitongoji wakati wowote jinsi
atakavyoona inafaa na pindi jambo la dharula lenye manufaa ya kipekee kwa
wanakitongoji.
Kazi na majukumu ya mkutano wa wakazi kitongojini.
v Mbali
na mambo mengine, mkutano wa wakazi kitongojini utakuwa na majukumu yafuatayo.
·
Kupokea na kujadili taarifa za
utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya kitongoji kama zitakavyowasiliswa na
mwenyekiti wa kitongoji.
·
Kujadili taarifa za
utekelezaji wa mikakati ya kupambana na umasikini.
·
Kujadili hali ya ulinzi na
usalama na maendeleo katika kitongoji.
·
Kuweka mikakati kupambana na
ugonjwa wa UKIMWI.
·
Kupokea maelekezo kutoka
Halmashauri ya kijiji na kuweka mikakati ya utekelezaji wake katika kitongoji.
Kazi za mwenyekiti wa kitongoji
Mwenyekiti wa
kitongoji atakuwa na kazi zifuatazo;
·
Kuitunza rejesta/takwimu/idadi ya wakazi
wa kitongoji na habari nyingine muhimu
zinazohusu maendeleo ya kitongoji kwa jumla, ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za vizazi
na vifo.
·
Kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa
watu na mali zao waishio katika eneo lote la kitongoji.
·
Kuhamasisha ulipaji wa kodi na ushuru
mbalimbali, kama utakavyoamuliwa na kuwekwa mara kwa mara na halmashauri ya
wilaya, mji, manispaa au jiji.
·
Kusimamia katika eneo lake suala zima la
hifadhi ya mazingira hususani vyanzo vya maji, misitu nk.
·
Kusimamia suala la afya katika eneo lake
ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kampeni za afya za kitaifa, kimkoa au
kiwilaya dhidi ya magonjwa ya
kuambukiza, na hasa vita dhidi ya UKIMWI na ya mlipuko.
·
Kusimamia utekelezaji wa kanuni za kilimo
na ufugaji bora ili kuinua hali ya lishe na uchumi wa wakazi wa kitongoji.
·
Kufuatilia na kuhakikisha kuwa kila mtoto
mwenye umri wa kwenda shule anapatiwa nafasi na kushirikiana na viongozi wa
shule katika kudhibiti utoro shuleni.
·
Kuhamasisha elimu ya watu wazima(ngumbaru).
·
Kusimamia na kuwahamasisha wakazi wa
kitongoji katika kutekeleza shughuli za
kujitegemea .
·
Kusuluhisha migogoro midogo midogo
isiyostahili kushughulikiwa na baraza la kata na mahakamani.
·
Kuwakilisha kitongoji katika serikali ya
kijiji.
·
Kuwaongoza na kuwahamasisha wakazi wa
kitongoji washiriki katika sherehe za taifa na mikutano ya hadhara
itakayoandaliwa na kuitishw serikalini au halmashauli.
·
Kutekeleze kazi nyingine atakazopangiwa na
halmashauli ya kijiji, wilaya, mji, manispaa au jiji.
·
Mwenyekiti anaweza kuteua kamati ya
ushauri yenye wajumbe wasiozidi watatu ambao ni wakazi wa kitongoji hicho kwa
ajili ya kushauri juu ya mambo mbalimbali yenye maslahi kwa kitongoji
kinachohusika.
Hizo ni kazi kuu za mwenyekiti wa kitongoji/mtaa.
Baki nasi kwa vizuri vijavyo.
Kwa ushauri na chochote kile
kilichokukwaza na kukufurahisha nk, usisite kutucheki hapa:
+255767611645
+255715080716
Mwanaharakati1992@gmail.com
No comments:
Post a Comment