CHAKULA CHA UBONGO - waleo blog

Breaking

Thursday 10 December 2020

CHAKULA CHA UBONGO

 #Kikokotoo

MAHITAJIA YA  AKILI

DOKEZO:

#Akili ni nini? Ni uwezo  alionao binadamu,mnyama na wadudu, ambamo ndanimwe ndio matokeo mambo mbali mbambali  wayafanyayo bila kuyabaini kuwa baya au zuri.Akili ni DHAHANIA  yaani ni kitu kisicho shikika wala kuonekana.

#Hitaji/mahitaji ni nini? Mahitaji kwa wingi,,,yaani ni jumla ya mambo yote wayafanyayo viumbe hai,kwa matokeo ya kufanikiwa ama kuto kufanikiwa(kushindwa), bila bila kuhofia uzuri ama ubaya wa hitajia hilo.

#Mahitajia ya akili ni nini? Ni ukamilifu wa matendo kwa watu wote, walio na utimamu juu ya kufanya matendo yaliyo mema.

Binadamu aliye sahihi/timamu anapaswa kuwa na maamuzi yaliyo sahihi bila kulazimishwa na mtu wa aina yeyote yule.Hapa tunapaswa kuelewa na kutafakari, juu ya ushawishi wa wazazi,ndugu,mwalimu kwa mwanafunzi,jamaa na marafiki.

Mahitajia haya ni kutoka kwa babu zetu (Urithi) kabla ya ukamilifu wake kukamilika baada ya ujio wa imani za dini.

Kwa nini DINI? Kabla ya dini DUNIA haikuwa na ubina adamu(Hummanity) kutokana na kuwatenga wanawake na kuua walemavu.  Rejea kwa mwandishi wa  kitabu cha TAKADINI  Bwana Benny J. Hanson. Dini ni mapokeo ya kumjua Mungu aliyekamilika na kufuuata sheria zake kama mkuu wa dunia na vilivyomo.

                                     BINADAMU ALIYE TIMAMU AISHIJE?


*Tabia za kinyama;binaadamu timilifu hapaswi kuishi kama mnyama,  yaani wapo baadhi ya watu huwa na tabia zisizo za kiungwana kutokana na imani za kishirikina ama  ukosefu ya mahitajia ya akili. Mfano; baba kutoka kimapenzi na bintiye na inayo fanana na hiyo.

*Heshima;wakubwa kwa wadogo,walo ndugu na waso ndugu,  heshima ni miongoni  mwa mambo ambayo yakifanywa na binadamu vinaweza kumtambulisha kuwa hitaji la akili yake ni sahihi.Wako baadhi ya watu wamelikosa hilo, pengine kwa malezi aliyoyakosa. Fursa na wakati bado anao baada ya kuona na kuisoma makala hii.

*Kujisisikia katika ukamilifu wako au kwa jambo uliaminilo katika matendo ambayo watu wengine hukuhitjia wewe kwa sababu ya ulicho nacho.Kujisikia si katika ukamilifu wa mahitajia ya akili.Kimsingi viumbe hai huishi kwa kutegemeana.  Jesus said,”Hakuna aliye twahara yule ambaye ametoka kwenye tumbo la mama yake”.

*Hofu ya MUNGU ndio msingi mkubwa wa mahitajia yaki akili kama tulivyoona hapo mwanzo ya kuwa, ukamilifu wetu wa mahitajia ya akili ulikamilika kwa ujio wa imani za dini.

 

Mambo yasiyo ya kiungwana na kibinadamu,katika uhalisia wake, ni hayafurahishi katika uso wa dunia na katika macho ya watu. Hivyo basi yatupasa kama walimwengu kuelekezana kwa lugha nzuri na zenye mvuto walau tupate kuishi kwa wema.

 

 

MAONI NA USHAURI

+255715080716

+255759133737

 

1 comment:

Pages