#UTALII
Nge;asili ya neno
hili ni kwa kutoka katika lugha ya kiarabu,’AQRABU”
Spishi hizi ndogo huitwa visusuli.
Ana miguu minane. Mkia
wake ni mrefu na una msumari mkubwa mwishoni mwake. Kama kawaida kiwiliwili
chake kina sehemu mbili: kefalotoraksi ( cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio lakini
zimeungwa kwa upana, siyo kwa pediseli (nyembamba lenye umbo la mrija
kama kwa buibui. Mgongo wa kefalotoraksi ni mgumu
na kwa hivyo, huitwa gamba. Nge
wana macho 6-12, mawili juu ya
gamba la kefalotoraksi na 2-5
kwa kila upande wa kichwa. Msumari wa nge hutumika kwa kudunga windo na
kuingiza sumu ndani yake.
Windo akiwa amekufa, kelisera za nge zinakata vipande vidogo
vinavyowekwa katika kishimo mbele ya mdomo. Maji ya umeng'enyaji yakamuliwa
katika kishimo hiki na baada ya kumeng'enya chakula; myeyuko ufyondwa. Nge hula
arithropodi wengine na wale wakubwa
hula mijusi na vipanya wadogo pia.
Faida ya
sumu ya nge
Kabila moja nchini Afrika ya
kusini ambalo huishi porini, huchanganya
sumu hiyo ya nge na pombe ya asili kwa lengo kutibu mgonjwa yaliyopo mwilini.
Leo tuishie hapa.Itaendelea_,_,_,_,….
Ushauri ni hapo.
+255767611645
+255715080716
No comments:
Post a Comment