#MALEZI
KIJANA NI
NANI?
Kijana ni
rika kuanzia miaka kumi na tano {15}
hadi arobaini {40}.Baadhi ya wataalamu wa elimu ya upevukaji huamini ya kuwa,
ujana ni pale tu mtu atakapoanza kuonesha dalili za ukuaji yaani kubalehe
hadi miaka arobaini na tano . wataalamu hawa huamini ya kuwa miaka hii ya 45,mtu
huanza kupunguza uwezo wa kufanya kazi zote zilizokuwa zikifanywa alipokuwa
kijana mfano,uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu. Leo katika makala hii
nimeona nikuletee machache yahusuyo misingi bora ya
kijana kama ifuatavyo.
Mchapakazi; kijana yeyote yule anaejielewa juu ya safari yake ya
maisha yaani, anakotoka na anakoenda basi nilazima ahakikishe anafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha anafika malengo
yake. Wapo baadhi ya vijana hujihakikishia maisha bora na il-hali hana shughuli
yeyote ya kiuchumi anayoifanya, “Hili nalo ni tatizo la kiakili, wasaidiwe hawa
“.
Utu; vijana wengi hudhani ya kwamba rika alilo nalo ni lakufanya fujo zote katika
dunia ,!!. Hapana huu si msingi wa kijana mwema ambaye anatarajiwa na wengi kwa
matumaini mbalimbali. Utu ndio heshima
na adabu ambamo ndani yake kunapatikana vitu kama kujitolea na kujitoa mfano,kusaidia wadogo kwa wakubwa awesavyo na kujitoa
katika mambo ya kijamii. Kijana bora lazima awe na……
Utii; Utiifu kwa wazazi wako, utiifu wa sheria mbalimbali
kama vile sheria za nchi , nyumbani, kazini
na hata sheria zako binafsi ni lazima uzitii na kuziheshimu ili
kufanikisha mambo mbali mbali. Baadhi ya vijana hushindwa kuwaheshimu na kuwatii
wakubwa kwa wadogo, huo si msingi wa kijana
bora. Haipendezi kwa kijana kuwafokea na kuwatukana wakubwa wala wadogo,
isipokuwa misingi ya kijana bora huonesha njia bora ya kuwaelekeza wote
waliomkosea na kuwakosea kasha kuwaomba/kuomba msamaha.Wapo baadhi ya vijana
huondosha utii kwa wazazi wao, kwa sababu mzazi /wazazi wake kushindwa
kumtimizia mahitaji yake muhimu kama kumsomesha na kijana huyo huona ugumu wa
maisha aliokuwa nao ni kwa sababu ya kukosa elimu huku watu aliosoma nao wakiwa kama kielelezo cha maisha
bora walionayo. “Usilitazame kwa ubaya na kulifyonya/kufonya
jiwe ulilo likwaa kisha likakuangusha,bali yatazame kwa umakinifu yale ya mbele
yakumezeayo mate”.
Saad S.Dunga mwandishi.
Tamaa; misingi ya kijana bora ni lazima kuwa na tamaa chanya
ya kupambana kwa njia za halali na
salama kumzidi yule ambaye amemtamani na alivyovitamani. Msingi huo utamfanya
kuwa na mafanikio mazuri katika jamii yake na kumuepushia lawama baada ya
kupitwa na muda.
Mila; kijana bora ni lazima awe mrithi wa mila mbali mbali kutoka kwako na
hata sehemu zingine duniani. Kinachotushinda vijana ni kupupia mila na desturi
ambazo maadili yake katika jamii zetu zina
muonekano mbaya mfano, mila za wageni wengi wa mataifa ya Ulaya kuvaa heleni kwa
wanaume. Huu si muonekano wa kijana bora. ‘’Tubadilike’’heleni ni moja ya pambo
kwa wanawake. Kijana bora ni lazima aepukane na mila na desturi za ulevi,kwa sababu ulevi hupunguza heshima na si katika misingi ya
kijana bora.’’Unalo hilo!!!?, badilika’’. Ili misingi bora yote hiyo iweze
kusimama katika ubora wake yampasa kijana awe-
Mcha mungu; ucha mungu ni hali ya kuwa mnyenyekevu na utiifu kwa
amri na makatazo yote aliyoyakataza MWENYEZI
MUNGU. Kimsingi huu ndio msingi mama wa misingi ya kijana bora.Ucha
mungu huu ni kwa wale waaminio visivyoonekana
kwa macho.’’Fikiria uwezavyo’’.
Ili kijana awe na misingi
bora na sio bora misingi , basi hutatikana /anapaswa kuchagua sehemu pa kuishi
palipo sahihi na anachokihitaji katika misingi yake mema. lakini pia makundi
sahihi ya kushirikiana nayo katika
shughuli zake. Tuwaandae vijana wetu kaika malezi ya kiMungu.
Tunaipongeza serikali yetu
ya Tanzania
kwa kuzuia baadhi ya vilevi, lakini pia ingefanikisha/kuamua
kupiga marufuku kwa vilevi vyote viaribivyo akili,
huenda tungefanikisha kuwapata vijana waliokuwa madhubuti wa kuijenga inchi yao
kikamilifu zaidi. Mungu ibariki dunia, Mungu ibariki Tanzania na viongozi wake
wooote.Lakini pia tunakuomba Mungu wa haki utuepushie majanga makubwa kama ya
Maradhi yatishayo na majanga makubwa ya kiasili.Amina
Tafadhali ishee na wengine
wapate faida nao.
Maoni na ushauri
hapa,
0767611645
0715080716
Ipo vzr
ReplyDelete