#AFYA
Miili yetu inahitaji
protini ili kujijenga pamoja na kujenga kinga ya mwili. Vyakula vya protini
vinatia ndani nyama, samaki, kuku, kunde, maziwa n.k Watu wengi huamini nyama
na maziwa kama vyakula vyenye protini na virutubisho. Na wengi hudhani kula
vyakula hivi huonesha hali nzuri ya kiuchumi.
Nyama nyekundu ni
pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo na sungura. Utafiti wa hivi karibuni kuhusu
protini unathibitisha kwamba kula nyama nyekundu kunaweza kuhusishwa na hatari
kubwa ya kifo.
Tafiti zinaonesha kuwa
nyama nyekundu ikitumika kwa wingi ni kati ya vyakula vinavyosababisha aina
mbalimbali za saratani kama ile ya kinywa, koo, utumbo mpana, mapafu na kongosho. Pia ina lehemu kwa wingi ambayo huweza
kuongeza hatari ya kupata magonjwa
ya moyo, shinikizo kubwa la damu, saratani, kisukari na kiharusi.
Kama unatumia nyama
nyekundu inashauriwa isizidi nusu
kilo kwa wiki. Inashauriwa kutumia
zaidi nyama nyeupe, ambayo ni kuku, bata mzinga na samaki nk. Hata hivyo, kutumia protini inayotokana na
mimea badala ya protini inayotokana na wanyama katika mlo wako huhusishwa na
upungufu wa hatari ya kifo.
Wanasayansi kwa muda
mrefu wamehusisha nyama nyekundu ya
kusindika na wigo mpana wa
magonjwa sugu, kama vile saratani, kisukari na
ugonjwa wa moyo.
Utafiti mpya
unaonyesha kwamba bado uhusiano huo upo wakati ukichunguza ulaji wa protini kwa
ujumla.
“Ingawa ni muhimu
kujua ni kiasi gani cha protini watu wanapaswa hutumia ili kufaidika kiafya,
kuhusu suala la lishe, watu kutambua ni aina gani ya vyakula wachague ili kupata
protini ni suala la muhimu pia”.
Watafiti waligundua
kuwa uhusiano kati ya ulaji protini na hatari ya kifo uliambatana na maradhi au
kuishi angalau moja ya maisha yasiyokuwa ya kiafya kama vile kuvuta sigara,
kunywa pombe kupita kiasi, kiribatumbo au kutofanya mazoezi.
Ongezeko la asilimia
10 katika ulaji protini za wanyama umehusishwa na ongezeko la asilimia 2 la
vifo kiujumla na ongezeko la asilimia 8 la hatari ya kifo kutokana na maradhi
ya moyo na mishipa.
Hata hivyo, kuongezeka
kwa asilimia 3 katika ulaji protini ya mimea kumehusishwa na asilimia 10 ya
kupungua kwa vifo kwa ujumla na asilimia 12 ya kupungua kwa vifo vitokanavyo na
maradhi ya moyo na mishipa.
Mtafiti mmoja wa tiba
lishe anasema, ulaji protini za wanyama umekuwa ukihusishwa na kiwango cha juu
cha insulini ya ukuaji kipengele cha kwanza, protini ambayo imekuwa inahusishwa
na matokeo mabaya ya afya, ambapo ulaji mwingi wa protini ya mimea umekuwa
ukihusishwa na kushusha shinikizo la damu na kuboreka usikivu wa insulini.
Anasema inawezekana
kwamba virutubisho vingine katika vyakula zaidi ya protini vinaweza kusababisha
madhara, mfano nyama nyekundu zilizosindikwa huwa na sodiamu nyingi, nitriti na
nitrati, ambazo zote zimekuwa zikihusishwa na matokeo mabaya ya afya.
Mfano wa nyama hizo ni soseji, nyama za kopo, hotdog, salami na
bacon.
Inashauriwa kuepuka
kutumia nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa chumvi, mafuta, kemikali au
kukaushwa kwa moshi. Nyama zilizosindikwa zimethibitishwa kuongeza hatari ya
kupata saratani hata zikitumiwa kwa kiasi kidogo tu.
Vyakula
vyenye protini ya mimea kwa wingi
Wanasayansi bado
hawajapata kipimo,yaani hawana uwezo kwa sasa wa kugundua kama mtu anatumia
aina gani ya protini kati ya protini ya wanyama na protini ya mimea, wangeweza
kufanya hivyo wangesaidia kutoa uelewa mzuri kwa jamii juu ya jinsi gani
vyakula hivyo husababisha vifo vya watu.
Vyanzo vizuri vya
vyakula vyenye protini ya mimea ni pamoja na mikate ya ngano isiyokobolewa,
nafaka zisizokobolewa, karanga, maharagwe ya soya na kunde.
TANBIHI: kwa sasa watu wengi husumbuliwa na ugonjwa wa magoti au sehemu
za viungio vya mwili yaani dalili za malaria,uti ama typthod na kuchukua hatua
za kutibu na,baada ya siku maumivu yako pale pale. Hizo ni dalili za ugonjwa wa
Bruccelosis unaosababishwa na ulaji wa nyama nyekundu kupitiliza.Epuka na
chukua hatua kasha jitibie.Wataalamu wanasema ya kwamba ugonjwa huu wa gaut
ukipuziwa, basi humpelekea mtu kuwa chizi.Hivyo basi uonapo dalili hizo chukua
tahadhari na uanze tiba.
No comments:
Post a Comment