#WOSIA
Tafadhali, huenda baadhi ya maneno yasikupendeze utusamehe, lengo ni
kukumbushana ili jamii ibadilike.
HADITHI ZA KWELI.
Amesimulia mtoto wa
omari ya kuwa, mtu mmoja alikuja kwa kipenzi cha mungu wa zama zilizopita,
(rehema za Mungu na amani zimshuke) akasema: “Nimekuja kukupa ahadi
ya utii juu ya kuhama pamoja nawe kwenda
kupigana vita juu ya maisha yetu ya baadae”Kipenzi cha mungu yule akamuuliza yule kijana: “Je, kati ya wazazi
wako wawili yupo aliye hai?” Akasema kijana: “Ndio, wote wapo hai.” Kipenzi
akamuuliza: “Je, unatafuta ujira mkubwa kutoka kwa Mungu wako?” Akajibu kijana
yule: “Ndio.” Kipenzi wa mungu akasema: “Rudi nenda ukawafanyie wema wazazi wako.”watu wawili walishuhudia tukio hili la
kweli..
Katika dini Fulani
nimewahi kusikia wakisema; wazazi wamepewa nafasi, uzito na heshima ya kipekee.
Mwenyezi Aliyetukuka anasema: “Na Mola wako mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu
yeyote ila yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee,
naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata ‘Ah!’. Wala usiwakemee.
Na sema nao kwa msemo wa heshima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa
kuwaonea huruma. Na useme, ‘Mola wangu mlezi! Wahurumie wazazi wangu
kama walivyonilea utotoni.” (Injili, Zaburi na Furukan, 17:23-24).
Hapa Mungu aliyetukuka anawakumbusha watoto
kuwafanyia wema na ihsani wazazi wao, kwa kuwa hiyo ni ibada inayopendwa na
kuridhiwa na yeye. Mwenyezi Mungu aliyetukuka nautukufu wake ameahidi malipo
makubwa duniani na mbinguni kwa yeyote atakayechunga haki za wazazi wake
wawili na kuwaheshimu. Ni ubaya ulioje kwa mtu anayepuuza jukumu hili. ’’Na aamini mwenye kuamini’’ methali za
sulemani.
Namna
ya kuwafanyia wema wazazi
Kuna namna nyingi za kuwafanyia wema wazazi.
Miongoni mwa hizo ni kuitika wito wao na kutekeleza mahitaji yao kadiri inavyowezekana
pia kuwapa heshima na hadhi ya juu. Usiwe mwenye kuwatembelea wazazi wakati
wa matukio maalumu,kama vile siku za sikukuu, bali watembelee mara kwa mara na ujipendekeze kwao.
Namna nyingine za kuwafanyia wema wazazi
wawili ni kuwashauri katika mambo mbalimbali na kuthamini ushauri wao, kuwaombea mema kila wakati, kuwahimiza kudumisha mambo
mbalimbali ya kheri kadiri watakavyoweza, kuwaheshimu wakati wote na katika
mazingira yote, mbele za watu, hata mkiwa peke yenu.
Watunze wazazi wako kadiri inavyowezekana na kamwe usiwatelekeza
au kuwaacha wafanyakazi wawahudumie
pasi na juhudi zako
kuonekana. Vilevile, waheshimu wazazi wako na uwaoneshe watu kuwa hiyo ni
tabia yako na si maigizo.
Mambo
yasiyofaa kufanyiwa wazazi
Haifai kuwaliza au
kuwahuzunisha wazazi, iwe kwa kauli au vitendo. Hilo ni jambo baya mno mbele ya mwenyezi
Mungu. Haitakiwi mtoto awe ndio chanzo cha wazazi wake kutokwa na
machozi. Pia, ni dhambi kuwakemea, kuguna, kukiuka amri yao halali kwa Mungu na maelekezo yao, kuwakunjia uso au kunyanyua sauti juu yao.
Ni ukweli kuwa; wapo baadhi ya watu
wanaoonesha nyuso za bashasha kwa watu wengine lakini wanawakunjia uso na
kuwakasirikia wazazi wao na kuwatazama kwa dharau hususani pale wanapowataka
wawasaidie kazi au majambo mbalimbali.
Haifai, na pia ni haramu kubishana na wazazi, kuwatukana, kutowashauri katika mambo mbalimbali, kutothamini
mawazo yao, kuingia chumba au nyumbani mwao
bila hodi, kuwavunjia heshima kwa kufanya vitendo viovu kama wizi, kutukana au kuanzisha ugomvi na ndugu na
jamaa zao. Kufanya hayo kunaweza kuwaingiza wazazi wako katika tuhuma
mbalimbali na hivyo kuishi na majonzi na huzuni. ‘’Jiepushe’’
Pia, haifai kuwalipisha wazazi madeni yasiyowahusu au kufanya kosa litakalopelekea
aitwe shule, chuo ama sehemu yoyote ile ambayo itakua na usumbufu kwao kwa
sababu yako tena kwa makusudi.Hafai kutaja aibu zao mbele ya watu wengine,
kuwalazimisha wakununulie vitu wasivyo na uwezo navyo, kumfadhilisha mke juu yao,
kuwapeleka kwenye nyumba za kulelewa wazee wakati una uwezo wa kuwahudumia, kuwafanyia ubakhili na
kufanya masimbulizi, yaani kuhesabu mema uliyowafanyia.
Ukaishi hivi na wazazi wako, basi kwa hadithi
ileee niliowahi kuisikia nikipita sehemu Fulani,wewe ni wa peponi kwa wale
waaminio kwayo, na kitakacho kuchelewesha kwenda huko Paradaise yaani peponi ni
kifo tu.Tujitahiidi ndugu zangu.
Share kwa wingi ili watu wakumbuke,waelewe ili
wazazi nao wale Bata(vitu vizuri ) za watoto wao.
No comments:
Post a Comment