MLO KAMILI,HUTUEPUSHA NA MAGONJWA. - waleo blog

Breaking

Sunday 26 January 2020

MLO KAMILI,HUTUEPUSHA NA MAGONJWA.


#AFYA

Miongini mwa vitu vya msingi sana katika afya na maisha ya binadamu yeyote ni chakula bora na mlo kamili.Mlo kamili ndo msingi wa afya njema,kujengeka vizuri kwa mwili,kinga ya mwili na kupendeza kwa ngozi na nywele zetu

Mlo kamili ni mlo ambao  una virutubisho vya  aina zote katika kiasi sahihi kama inavyotakiwa na miili yetu.Mwili wowote utakapopatiwa chakula bora na mlo kamili kama inavyotakiwa utapata faida zifuatazo


·                     Mwili utajengeka vizuri kila siku
·                     Utakuwa na kinga umara dhidi ya magonjwa
·                     Hautapata magonjwa yanayosababishwa na lishe mbaya na ulaji mbaya kama kisukari, shinikizo la   
              Damu.
·                     Hautakuwa na ngozi na nywele dhoofu
·                     Hautapata matatizo  mengine kiafya  yatokanayo na mapungufu ya madini

                     MLO KAMILI UNATAKIWA UWEJE?

 Kimsingi mlo kamili ni rahisi sana kwa kuwa una mahitaji machache tu na mengi kati ya hayo ni vyakula hivi hivi tunavyokula kila siku.Changamoto  kubwa sana katika hili ni kukosa uelewa wa mlo kamili unatakiwa uweje na kushindwa kupanga vyakula ili vitengeneze mlo kamili.

MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI
Hivi vinatakiwa angalau viwe nusu ya sahani yako na ni kwa milo yote ya siku kula sana matunda na mboga za aina mbalimbali na rangi mbalimbali.




VYAKULA VYA KUKUPA NGUVU(WANGA/ CARBOHYDRATES)
Hivi vinatakiwa viwe robo tu ya sahani yako mifano ni vyakula vinavyotokana na mahindi,mpunga,mtama,ngano n.k hizi zina virutubisho vingi zaidi na faida nyingi kuliko mbegu ambazo zinazokobolewa tayari.Badala sembe kula dona na badala ya mkate mweupe( white bread kula brown bread





VYAKULA VYA KUKUPA PROTINI
Hivi vinatakiwa kuwa robo tu ya sahani na tumia zaidi protini zinazotokana na jamii ya maharage na mbegu zingine,kuku na samaki. punguza kula nyama nyekundu kama vile ngombe na mbuzi.

Ni  rahisi kama hivyo, na hivyo vyote watu wengi wanavipata na kula. Kosa kubwa wanalolifanya watu wengi ni kutofahamu mpangilio wa milo yao na kujikuta wakila zaidi mlo mmoja.


Cha kuongezea hapo ni maji na mafuta ya kupikia.
Kunywa maji ya kutosha, angalau lita mbili kila siku. Kunywa kama maji au vinywaji vingine salama kwa afya yako kama vile juisi, chai, kahawa na maziwa; japokuwa unatakiwa usinywe sana maziwa na kahawa (Kikombe 1-2 kwa siku).
Tumia mafuta mazuri ya kupikia, salama kwa afya yako. Mfano ni mafuta ya mzaituni . Usitumie mafuta mengi, kijiko cha chakula kimoja hadi viwili yanatosha sana kwa chakula chako. Epuka kupikia mafuta yatokanayo na wanyama, epuka kupikia mafuta yanayokuwa kwenye hali ya kuganda.
Bila kusahau mazoezi mepesi.



 Anza sasa. Fanya hivyo kwa milo yote na kila siku. Mlo wa asubuhi, mlo wa mchana na mlo wa usiku. Afya njema na muonekano mzuri unakusubiri.......Share, like, follow na maoni ili wengine nao waelimike  na kupata vitu vizuri kutoka kwetu. Asante.


No comments:

Post a Comment

Pages