WANAWAKE WANAOHITAJI KUOLEWA - waleo blog

Breaking

Wednesday 19 February 2020

WANAWAKE WANAOHITAJI KUOLEWA

 
Kazi ni kwenu.

#Mahusiano


            Najua ni ndoto ya kila mwanamke anaejitambua kwamba katika maisha ni lazima aolewe awe na mume mmoja na aishi nae na wazae watoto ili kuendeleza dunia yetu japo kuoa au kuoelwa sio lazima lakini ili ueleweke vema na uipe heshima jamii yako na wewe mwenyewe pia, basi ni vema ukifika wakati wa kuoa au kuolewa ufanye hivyo

            Hata hivyo kwa upande wa wanawake imekuwa ni shida kutokana na kuwa waamuzi wa kuoa au kutokuoa niwanaume na hivyo mwanamke anaweza kuwa anatamani litokee jambo hilo lakini ikawa tofauti. Ukweli usiopingika ni kwamba katika maisha yako kama mwanamke au mwanaume utakutana na wanawake wengine au mwanamke utakutana na wanaume wengine kadhaa ambao sio sahihi kwako kabla ya kuja kukutana na chaguo lako alie sahihi. Sasa hapo hapo ndio shida ilipo maana wengi tumekuwa tukichezeana na kuishia kuumizana tu halafu unakuta mwanaume anakuacha anaenda kuoa mwanamke mwingine au mwanamke anaenda kuolewa na mwanaume mwingine kabisa baada yakuona aliye nae hana malengo kimaisha .Hapa leo nitakueleza wewe mwanamke ambae umekuwa na boys wengi wameishia kuplay na wewe; nini ufanye kupata boys wote waanze kukuona wewe ni wife material?

1.       Hama nenda mbali kwa ndugu wa mbali, lakini ambae ana sifa nzuri na ana ushuhuda mzuri kwa watu wa eneo alipo. Hapa ukweli ni kwamba watu wanaokufahamu ni vigumu kuwafanya wageuke na kukuona wewe wafaa wakati wanafahamu wewe umetembea na marafiki zao kadhaa , Zaidi watakuwa wanapoonana habari zako kama vichekesho tu na kukuchukulia wa kawaida sana.      

2.       Badili kabisa tabia, mavazi na mienendo yako ukiwa ugenini huko. Wanaume wanapenda mtu mwenye tabia nzuri na mwenendo mzuri lakini kwa anaejua historia yako bado hata ukibadilika bado akikumbuka zamani ataona wewe wa kawaida sana lakini ugenini kuna watu wa heshima zao watakaokuona na kukufauata kwa nia njema baada ya kukutathimini na kuona una mienendo mizuri katika maisha na wataona wafaa kuwa mwenza wa maisha kwao. Hapa nikukumbushe usifanye kuigiza yaani badilika full kama ni nguo fupi za ajabu sana acha kabisa, kama ni ulevi au umbea au kuongea sana acha kabisa.

3.       Anza kusali.Hapa tena usifanye tu kuigiza kama unataka mume bali we fanya kama sehemu ya kutumika kwa Mungu kulingana na dhehebu lako au dini yako inavyokutaka na usiwaze wanaume walioko kanisani ndio wakuone we amini dunia ni kubwa na ina watu kiasi walioko kanisani/msikitini, wanaweza kuwapa taarifa wengine wengi sana na ukaja olewa na mtu mstaarabu tofauti na ulijidharau na kujikadiria mwanzo na utapata jeuri hata ya kuwakataa baadhi ya wanaume wenye hadhi zao ikiwa hujaridhika nao maana najua hata mwanaume awe na pesa bado lazima akuvutie kisura pia ili umkubalie na ili umpende siku zote maishani.

4.       Ugenini uwe mpole mkarimu, sio muongeaji sana ila mwenye ushauri mzuri kwa wengine. Wanaume woote duniani tunapenda mwanamke mpole tukiamini hatutasumbuana katika ndoa hata ikija kutokea kusumbuana tunaamini upole wako utakufanya uwe unamskiliza mume , na hivyo ukiwa muongeajiu sana tayari wanaume tunaanza kuona wewe sio aina ya kuoa.

5.       Ugenini shirikiana na watu, kwenye mambo yote ya furaha na  ya huzuni.Hapa sasa kama kuna msiba ni wakati wako kushiriki kuteka maji,kupika,kuosha vyombo nk ikiwa msiba unakuhusu lakini. Na kama pia kuna sherehe basi vivyohivyo husika kwa namna zote .Wanaume huwa wana kazi zao kwenye matukio kama hayo lakini ndio muda  wanaume hupeana stori kuhusu watu mnaoonekana pale na vile mnavyoweka bidii, basi wao ndio huzidi kuambina sifa zako na hivyo katika kundi la wengi zitaibuka sifa zako za nyumbani , za kanisani, za kazini nk na wapo watakaoona kumbe wewe ndiye mtu waliyekuwa wanamtaka siku zote wawe naye katika maisha. Sasa kitu kimoja usifanye ni hivi, sehemu hizo kamwe usikae kundi moja ukapiga stori na wanaume . We kaa na wanawake wenzio ukiwa mskilizaji zaidi na pia wanaume wasalimie kwa heshima zao na usiwe na muda nao lakini usioneshe dharau hata kidogo kwa yeyote yule.maana huwa zinasambaa habari kama ulezi uliomwagika.

6.       Ugenini lazima utafute kazi Fulani ya kufanya ambayo itakuingizia kipato .Amini wanaume wanaona unapambana wanajua yule nikimuweka ndani nikampa mtaji wa laki tano tunaweza kufika mbali kimaisha . Na pia ukiwa huna chanzo cha pato wapo watakaojua wewe unahongwa ndio unapata hela ya vocha. Jitahidi uwe na bishara ya kukaa sehemu moja kama ukishindwa basi pata hata ya kutembeza ila kama yawezekana biashara ya kukaa sehemu moja kama kuuza maandazi , juice , mikate, matunda na mbogamboga nk itakuwa njema maana katika kutembea kwingi wapo watakaokufikiria vibaya japo hutakiwi kujali sana hayo; ila nasema kama ipo chini ya uwezo wako fanya biasghara ya kukaa eneo moja , unaweza kuwa fundi cherehani , kufungua mgahawa . Lakini nasisitiza tena usizoeane na wanaume huko ugenini yani wakawa wanakutania kupita kiasi mpaka wanakushika , kamwe usifanye hivyo , na pia nakusisitiza kamwe usionyeshe dharau yeyote kwa yeyote yule mwanaume atakayekufuata kukutongoza ukamkataa kistaarabu hatakusema vibaya badala yake ataeneza habari za kwamba dada yule ana msimamo na hapo wapo watakaokuja kukujaribu basi msimamo wako uwe thabiti na imara katika kujiridhisha kwamba wana nia gani na wapo watakaokuja kweli kwa nia njema baada ya kusikia habari zako za msimamo mzuri  watasema hakika huyu akikubali kwangu yafaa awe mke wangu na hapo unakuwa kwenye nafasi ya kuamua nani nakufaa katika watakaokuja kwako.

7.       Marafiki wazuri tu ndio unaohitaji huko ugenin.i Hapa uwe makini wanaume huwa wanasema kikundi cha akina Fulani yani wakijumlisha marafiki wote hivyo kama wewe pia uko na marafiki wanaosifika vibaya basi moja kwa moja umeshapata sifa mbaya tena watasema hata mgeni yule ameshaharibikiwa mapema hivi.Ugenini usiwe na haraka ya kusoeana na watu wala haraka ya marafiki, jitahidi ujiridhishe kuwa marafiki hao hawatakuletea sifa mbaya ndipo ujenge urafiki nao.Kumbuka marafiki wastaarabu watakuwa wanafahamiana na wanaume wastaarabu. Pia hivyo hata wewe unajiweka katika nafasi ya kufahamika kwa wanaume wastaarabu ambao wataamini wewe pia u mmoja na wale marafiki zako.

8.       Ugenini usizurule wala kutembeatembea mitaani hovyohovyo , ukitoka kutembea ukiwa unajua unaenda kwa nani na kufanya nini sio kila siku wanaume wanajua wewe utakuwa pale varandani kwa akina nani mnapiga stori zenu. Hiyo itajenga sifa mbaya sana kwako. Unatakiwa uonekane tu kama unaenda kazini , unaenda kanisani , unaenda sokoni unaenda dukani , unaenda sehemu maalumu. Hata mwanaume anaekuvizia awe anawaza atakupataje sio anauliza anaambiwa yule sasa hivi atapita hapa mbona yupo  kwa tahira Fulani .. mara paap kweli unapita basi ndio kabisaa anaona wewe chapa tupa kule.nadhani umeelewa hapo

9.       Ugenini jitahidi kupendeza na kuwa msafi muda wote , wanaume huwa tunaamini sisi ni majembe ya kazi hivyo kuwa rafu sio kesi sana ila mwanamke hata unapotoka shambani bado hutakiwi kuwa mchafu yani unakuwa nadhifu wakati wote . Unajua kwa wakristo biblia inasema mwanamume utakula kwa jasho, lakini kwa manamke eti mwanamke ni pambo la ndani yani. Sasa hapo nadhani unanielewa haimaanishi wanaume tuwe wachafu lakini wanaume kuwa wachafu itahesabika kama sababu ya kazi, lakini popote pale ukikutwa mchafu watasema hajiheshimu.. kama huamini iko hivi mwanamke mchafu akipita pale posta dar es salaam au akiingia kwenyedaladala na nguo chafu na amejaa majasho watu watalalamika na kusema mwanamke gani mchafuuu ,,, lakini mwanaume akiingia hivyo watu husema duuuh kazi kazi aisee hatari mwanamke usafi kipaji chako inabidi usikosee uwe msafi tena pendeza siku zote wakati wote na hasa unapotoka nje.


Anza na hatua hizi sasa na uone mabadiliko Mungu akipenda.
Sambaza na wengine wabahatike kuolewa.

No comments:

Post a Comment

Pages