PUNYETO,WANAWAKE/WANAUME NA ATHARI ZAKE - waleo blog

Breaking

Wednesday, 19 February 2020

PUNYETO,WANAWAKE/WANAUME NA ATHARI ZAKE


#AFYA

Punyeto ni tendo lolote la kujitafutia ashiki(nyege) binafsi hasa kwa kuchochea viungo vya uzazi. Wanaochukua hatua hiyo ili wajipatie kionjo cha kuridhisha kinachofanana na kile cha tendo la ndoa kwa kawaida wanasukumwa na msisimko uliowapata, pamoja na haya ya kujitafutia mtu na hofu ya kuambukizwa maradhi ya zinaa.

Kufanya hivyo ni kupotosha maana ya jinsia kwa binadamu, ambayo ni kufanya wawili wawe kitu kimoja kwa nguvu ya upendo ambao uanze rohoni na kukamilika katika muungano wa miili yao.
Upendo maana yake ni kujitoa kwa muungano na mpenzi unaoleta tunda lake katika mtoto, ambaye ni kwa pamoja wa baba na wa mama, akiwaunganisha upya ndani mwake.
Katika tendo la kujichua hakuna lolote kati ya hayo: hakuna upendo wala kujitoa kwa wengine, hakuna muungano wala uzazi, isipokuwa kujitafutia iwezekanavyo furaha ya kimwili (ashiki) iliyokusudiwa na Mungu kuwa sehemu ya furaha nzima ya muungano wa ndoa.
Katika tendo hilo la ubinafsi mtu yuko peke yake na kubaki peke yake: halengi chochote nje ya mwili wake, hivyo anazidi kuzama ndani mwake badala ya kustawi kwa kujiwekea malengo mema (mf. ndoahakihuduma kwa wenye shida, n.k.). Matokeo yake ni kupoteza nguvu za mwili na hasa kuvuruga msimamo wa nafsi kwa kujisikia mnyonge, mwenye kosa na mtumwa wa tendo ambalo analikinai mara tu baada ya kulitenda. Hatimaye anaweza kupata matatizo katika tendo la ndoa.
Hata hivyo elimunafsia inatueleza pia urahisi kwa mtu asiyekomaa kimapendo kufuata njia hiyo danganyifu, tena ngumu kuachwa baada ya kuzoeleka.

MADHARA YA UPIGAJI PUNYETO KWA MWANAUME



1. PUNYETO INAUA NGUVU ZA KIUME

Upigaji wa punyeto unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwani kipindi unapiga punyeto jua ile mishipa inayofanya uume usimame unakuwa unaichua na uume unakuwa umesimama kwa muda mrefu, sasa ikitokea ukawa unafanya hivi kila siku ile mishipa inalegea na uume unakuwa unakosa nguvu hata ukisimama haui strong unakuwa kama umelegea.

2. KUWAHI KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO NA KUSINYAA KWA MAUMBILE YA UUME

Mara nyingi mtu aliezoea kupiga punyeto huwahi kumaliza mapema pindi akiwa anafanya tendo la ndoa na wakati mwingine uume hushindwa kusimama kwa mara ya pili na kujikuta anashindwa kurudia tendo ikiwa mwenzake bado hajaridhika na anahitaji kuendelea kufanya tendo hilo.

Athari nyingine ni kama zifuatazo


3.Uchovu wakati wote
4.Maumivu ya nyonga
5.Kusinyaa kwa Nywele
6.Maumivu ya kende
7.Maumivu ya kiuno

Hayo ni baadhi ya nukuu zangu!

Kuna faida nyingi sana ambazo utazipata endapo utaachana na tabia ya upigaji punyeto na hiyo napenda iwe sababu ya wewe msomaji kuachana hicho kitendo.
Kuacha punyeto ama mtindo flani wa maisha inahitaji utambuzi, uamue na pia uweze kujicontrol wewe mwenyewe, inahitaji nguvu ya ndani yako kushinda vishawishi , zifuatazo ni njia ambazo utaanza kutekeleza ukiwa nyumbani kwako bila gharama yoyote na zitaanza kukupa matunda, lazima uwe mwaminifu kufuata kile ninachoelekeza maaana ni njia ambayo imewasaidia vijana wengi.

1.PATA MUDA MWINGI WA KUPUMZIKA

Baada ya shuguli za kawaida haikisha unapata mda wa kupumzika, lala mapema ili uweze kuipa akili mda wa kuchambua na kutunza taarifa za muhimu na kufuta zile zisizo za muhimu. Hakikisha unalala mapema hapo ndipo utaongeza uwezo wa akili kuweza kupambana na hisia na mawazo mabaya.

2. MATUMIZI YA MBOGAMBOGA NA MATUNDA KWA WINGI

Utafiti wa kisayansi unaonesha kwamba matumizi mazuri ya vyakula vya mbogamboga na matunda Husaidia kuongeza uwezo binafsi wa kujisimamia juu ya tamaa na mihemko mbalimbali, matumizi ya vyakula vilivyosindikwa  ni chanzo cha kushindwa kujizuia na hapo safari yako ya kuachana na upigaji punyeto itakwama.


3. FANYA MAZOEZI NA USHUGULISHE MWILI

Maozezi yanasaidia mwili kutofikiria kufanya mambo machafu sababu mara nyingi unakuwa bize, akili inapokuwa inashugulishwa basi uwezekano wa kuleta fikra mbaya ni mdogo sana


4. ACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO

Tafiti zinasema kwamba vijana wengi wenye umri kuanzia miaka 15 mpaka 30 ndo kundi kubwa lililoathirika kwa kutazama picha za pono, piacha au video za ngono huleta msukumo kwenye akili ili kuweza kujiridhisha na hivo hupelekea watu kupiga punyeto ili kukata ile kiu ya  tamaa zao za mwili.


SULUHISHO KWA MTU ALIYEATHIRIKA NA UPIGAJI PUNYETO WA MUDA MREFU:

Athari za kujichua mara nyingi hujitokeza kwa hali ya kutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.

Kuna baadhi ya watu huweza kuanza kuona athari zake mapema zaidi na baadhi yao huchelewa.

Jitahidi sana kufuata hivyo viepushi punyeto ili uitunze afya yako.

No comments:

Post a Comment

Pages