#Utalii
Ngiri, gwasi au mbango ni
wanyama wa jenasi katika familia Suidae.
Hizi ni aina za nguruwe-mwitu wenye sugu kubwa kichwani, madume hasa (sababu ya jina kwa Kiingereza: warthog).
Wana pamba ndefu, zile za dume ndefu kuliko zile za jike. Hula manyasi, mizizi, beri na matunda mengine, gamba la miti, nyoga na hata mayai, mizoga na pengine wadudu na wanyama wadogo.
Wakila hupiga magoti ya mbele na wakitoroka kitisho huweka mkia juu wima.
Nguruwe ni wanyama wa familia Suidae. Nguruwe-kaya hufugwa kote duniani.
Spishi mbili zinaitwa ngiri.
Tabia na maelezo
Nguruwe ana pua kubwa, macho madogo na mkia mdogo unaokuwa
umejikunja na mfupi, uliopinda au ulionyooka. Huwa ana mwili mkubwa, miguu
mifupi na nywele zilizojiviringisha. Ana kwato nne kwa kila mguu, huku mbili
kubwa za mbele zikitumika kutembelea.
Kuzaa huwezekana msimu wote wa mwaka katika ukanda wa tropiki,
lakini hasa misimu ya mvua. Nguruwe jike huweza kubeba mimba akiwa na miezi 8
mpaka 18. Kisha ataanza kupata hedhi kwa muda wa siku 21 kama hajashika mimba.
Nguruwe dume huweza kushiriki masuala ya uzazi katika umri wa miezi 8 mpaka
10. Kwa uzao mmoja, wanaweza kupatikana watoto 6 mpaka 12, waitwao vibwagala. Kisha kuachishwa kunyonya, familia mbili au
tatu zinaweza kuishi pamoja mpaka msimu mwingine wa kujamiiana.
Nguruwe hawana tezi za jasho, hivyo nguruwe hujipoza kwa kutumia
maji au matope wakati wa joto kali. Pia hutumia matope kama njia ya kujikinga
na kuunguzwa na jua. Zaidi, matope huzuia wasiathiriwe na inzi na vijidudu.
Nguruwe wanaofugwa nyumbani hukuzwa na wakulima kwa ajili ya
nyama na ngozi. Nywele zao ngumu hutumika pia kwa kutengeneza brashi. Baadhi ya
spishi za nguruwe, kama vile wale wa Asia, huwekwa kama wanyama wa ndani wapenzi.
Chakula
Nguruwe ni omnivora, yaani wanakula nyama na majani. Nguruwe
hula mabaki na hujulikana kwa kula chakula chochote, kujumuisha wadudu, minyoo,
magamba ya miti, takataka na hata nguruwe wengine. Wakiwa mwituni hula majani,
nyasi, mizizi, matunda na maua. Kwa nadra, nguruwe wakiwa wanafugwa, huweza
kula watoto wao kama wakichukizwa sana.
Nguruwe wa kawaida wana kichwa kikubwa chenye pua ndefu
iliyoimarishwa kwa mfupa mgumu na mduara wa tishu ngumu mbele. Pua hiyo
hutumika kuchimba udongo ili kutafuta chakula na ni ogani yenye uwezo mkubwa wa
kuhisi.
Nguruwe huwa na seti kubwa ya meno 44. Meno ya nyuma
yametoholewa kusaga, na huendelea kukua na huchongwa na misuguano ya meno
yenyewe.
Nguruwe wanaochungwa mwituni kwa msaada wa wachungaji, wana
uwezo mkubwa wa kunusa, na hutumika kutafuta uyoga katika nchi nyingi za Ulaya.
Nguruwe wa nyumbani hutambulika kwa jina la kisayansi Sus
scrofa. Walianza kufugwa karibu miaka 5,000 mpaka 7,000 iliyopita.
Walizaliwa na rangi ya kahawia na kuendelea kuwa wa kijivu. Meno chonge ya juu
huwa kama ndovu za kipekee zilizopinda nje na kuelekea juu. Urefu wa nguruwe
huweza kufikia milimita 900 – 1800 na uzito wa kg 50 – 350.
Nguruwe wana akili na huweza kufundishwa kazi na mbinu
ndogondogo. Hivi karibuni, wamefurahia kupewa nafasi kama wanyama kipenzi wa
ndani na, hasa wale nguruwe wadogo.
Huyo ni
Ngurue/kiti moto kwa lugha zetu za mtaani .kwa uchache tufuatilie ufaidike
zaidi
No comments:
Post a Comment