USHIRIKINA(UCHAWI) TUNATEMBEA NAO - waleo blog

Breaking

Wednesday, 19 February 2020

USHIRIKINA(UCHAWI) TUNATEMBEA NAO


#GHAIBU

Hirizi ni nini?

Hirizi ni kitu cha kuvaa mwilini kama vile karatasi iliyo na maandishi maalumu, kipande cha mti,shanga kwa mwanamke isiyo na lengo la mapambo,kembe,cheni,pete,pesa zenye tobo katikati,meno na magamba ya wanyama na ndege mbalimbali, saa za mkononi,michoro mbali mbali mwilili kwa binaadamu(tatuu),mifupa ya viumbe iliyofungwa kwenye nguo, ngozi, n.k. kinachoaminiwa kuwa ni dawa ya kujikinga na madhara.Kwa mujibu wa imani fulani,yapo mapambo ambayo wanawake kwa wanaume wameruhusiwa kuvaa.Ubaya unakuja  mara baada ya kwenda kwa mtaalamu huyo na kukukabidhi kwa masharti Fulani Fulani kulingana na tatizo lako.
Ikiwa utapewa ama kufanyiwa miongoni mwa vitu hivi, ima amekupa kiongozi wa dini yeyote ile(shekhe,padri ama mchungaji),basi tambua tiba hiyo ni ya kishirikina na nimakosa kwa yule aliyekuumba.


Mungu anasemaje kuhusu hili katika Bibilia.
Naamini umeshasikia mara nyingi watu wakisema, “Jisaidie na Mungu naye atakusaidia.” Siwezi kukataa lakini kama ni Mungu huyu ninayekuambia habari zake hapa. Imeandikwa: Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako. (Methali 3:5-6).
Sasa watu wengi wanasema kuwa kwenda kwa waganga ni katika jitihada hizo za kujisaidia. Bwana wa majeshi anasema hivi: Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute, ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. (Mambo ya Walawi 19:31)
Kitendo cha kwenda kwa mganga si tatizo,ukamwelezea unachoumwa kisha akakupa miti shamba ima ukaogee,ukanywe na kujifukiza.hii sio shida.Shida ni kupandisha mapepo ama kuchorachora ndipo ufumbuzi wako upatikane.
Na anaonya kwa ukali kabisa kuwa: Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake. (Mambo ya Walawi 20:6). Kuzini inaweza kumaanisha maana hii ya kawaida tunayoifahamu, lakini pia kibiblia, Mungu anaichukulia nchi kama mke. Nchi inapomwasi Bwana  na kwenda kwa miungu mingine, basi inakuwa inafanya uzinzi).
Pia Mungu anasema: Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao(ramli), wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana. (Kumb 18:10-12).
Uislamu na kitabu chake nao unasemaje?
Tufahamu kuwa kuvaa hirizi ni kumshirikisha Mungu (Subhaanahu wa Ta‘ala) na hiyo ni dhuluma iliyo kubwa, amali zote(matendo mema) huharibika na ni dhambi ambayo haisamehewi na Allaah. Hayo ni kwa mujibu wa kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala): “Hakika Allaah Hasamehi dhambi ya kushirikishwa na kitu chochote, lakini yeye husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah, basi bila shaka yeye amekwishapotea upotofu ulio mbali na haki” (4: 116).

Pia: “Na wakumbushe, Luqmaan alipomwambia mwanawe; na hali ya kuwa anampa nasaha. Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, maana shirki ni dhulma kubwa sana” (31: 13).quraani


Miongoni mwa njia za shirki ni kupatiwa hirizi na maalim, Shakhe na wengineo ambao huwadanganya watu kwa kuwasomea kisomo cha uwongo kisha kuwapa hirizi wavae. Waalimu wa kweli wanasoma kile kisomo kilichosuniwa(thibitishwa) na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kuondosha kwa mtu ikiwa amekumbwa na jini au amefanyiwa uchawi. Maswala ya kutumia hazina au hirizi yamekatazwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo kuwa haramu katika dini yetu tukufu ya Uislamu.


Kuhusu hilo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatueleza: “Mwenye kutungika hirizi hakika amefanya shirki” (Ahmad na al-Haakim, naye akaisahihisha).

Na kauli yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Aliyetundika hirizi na mwenye kutungika hazima basi Allaah hamtimizii shida yake, na mwenye kutungika hazima Allaah hamuondolei alicho nacho” (Ahmad na al-Haakim, naye akasema Isnadi yake ni sahihi).

Na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomuona kipofu mmoja ana kitambaa kakifunga mkononi mwake cha njano: “Kwa nini umefanya hivi?” Akasema: “Hii ni kutokana na ‘wahina’ tatizo lililonikuta”. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ivue kwani Allaah hatakuzidisha ila matatizo tu na kama utakufa na hiyo iko juu yako basi hautafanikiwa milele” (Ahmad).


Ikiwa una matatizo au ni mgonjwa vipimo ambavyo hospitalini havionekani kinachofaa kwako kufanya ni kujitibu kwa Ruqya (kisomo cha kisheria) ambamo hamna shirki ndani yake. Inatakiwa mwenye kukusomea awe atasoma zile ayah na Surah ambazo ni tiba kwako au wewe mwenyewe mbali na kusoma surah na ayah tofauti za Qur-aan, na uwe ni mwenye kusoma zile ayah ambazo zitakusaidia. Ndio katika hilo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia: “Hakuna ubaya na Ruqya kama hakuna shirki” (Muslim).


Ikiwa kutakuwa na kisomo na shirki ndani yake kama ulivyofanyiwa itakuwa haifai. Ukitizama katika hirizi ambayo utakuwa umepatiwa hakuna kitu ndani isipokuwa karatasi isiyo na maandishi au karatasi iliyochorwa tu vitu au pengine kipande cha gazeti kama alivyopata mmoja wetu kuona pindi alipomtoa msichana mmoja hirizi na kuifungua ndani yake.
Hiyo ndio hirizi na mafundisho kutoka katika dini kuu mbili duniani.Kimsingi tujiepushe nazo ili tuweze kuupata uzima wa milele
Share na wengine watupe hirizi sasa. 

No comments:

Post a Comment

Pages