#HISTORIA
Mpira wa miguu ( soka au kandanda) ni mchezo unaochezwa na jumla ya wachezaji
ishirini na wawili katika timu mbili, kila timu ikiwa
na wachezaji kumi na moja.
Lengo hasa la mchezo huu ni wachezaji kuumiliki mpira kwa
kutumia miguu na kufunga goli, yaani kuuingiza
mpira katika wavu wa
wapinzani mara nyingi zaidi.
Matumizi ya mikono ni marufuku
isipokuwa kwa mlinda mlango katika
eneo maalumu na wakati wa kurudisha mpira baada ya kutoka nje ya uwanja ama
wachezaji wengine kurusha kwa mikono baada ya kutoka nje eneo ambalo si la
mlinda mlango yaani goli kipa.
Michezo mbalimbali ya kuchezea mpira inaweza kupatikana katika
kila uwanja wa jiografia na historia. Wachina, Wajapani, Wakorea na Waitalia, wote hao walikuwa wakicheza mpira zamani
kabla ya enzi zetu. Wagiriki na Waromania walitumia michezo hiyo kuwaandaa
wapiganaji kabla ya vita.
Ilianza wakati mashirikisho mawili (Shirikisho la Mpira wa miguu
na Mpira wa Ragbi) yalipotawanyika. Shirikisho la kwanza
lilibakia Uingereza.
Mnamo Oktoba 1963, Vilabu 11 vya London vilituma wawakilishi katika mkutano wa Freemasons ili kujadili na kuweka kanuni
zilizokubalika kusimamia mechi zilizochezwa
kati yao.
Mkutano huu ulipelekea kuanzisha kwa Shirikisho
la Kandanda (Football Association).
Miongoni mwa kanuni zilizowekwa ni zile za kukataa utumiaji wa mikono kushika mpira na kunyang'anyana kwa nguvu. Soka na Ragbi zilifarakana tarehe hiyo.
Miaka minane baada ya kuanzishwa, Shirikisho la Kandanda (FA)
lilikuwa na wanachama 50. Shindano la kwanza la kandanda - Kombe la FA -
lilianza mwaka huo, likifuatiwa na lile la Ligi ya
Ubingwa miaka 17 baadaye.
Wachezaji wawili wa Kilabu ya Darwin, John Dove na Fergus Suter walikuwa wa kwanza kulipwa kwa mchezo wao. Kitendo hiki
kilikuwa mwanzo wa soka ya
kulipwa iliyohalalishwa mwaka wa 1885.
Mwamko huu ulipelekea kuanzishwa kwa mashirikisho ya kitaifa nje
ya Uingereza (Great Britain). Baada ya Shirikisho la kandanda la Uingereza, mashirikisho
yaliyofuatia ni ya Uskoti (1873), Wales (1875) na Eire (1880).
Mataifa mengine mengi yalianzisha mashirikisho ya kandanda
kufikia 1904 wakati shirikisho la soka duniani (FIFA) lilipoanzishwa. Tangu hapo, kandanda ya
kimataifa imekuwa ikikua licha ya vikwazo mbalimbali.
Kufikia 1912, FIFA ilikuwa na wanachama wa mashirikisho 21, idadi iliyoongezeka
na kufikia 36 mwaka 1925.
Kufikia 1930 - mwaka ambapo kwa mara ya kwanza kulikuwa na mashindano
ya Kombe La
dunia, FIFA ilikuwa na wanachama 41. Idadi hii
ilizidi kuongezeka na kufika 51 mnamo 1938 na 76 kufikia 1950.
Baada ya Kongamano la FIFA la mwaka 2000, kulikuwa na wanachama 204 na idadi hii inazidi kukua kila
mwaka.
Maagizo ya kandanda hupitiwa na kufanyiwa mabadiliko kila mwaka
(Mwezi Julai)
na Shirikisho la kandanda
duniani (FIFA).
Uwanja una umbo la mstatili. Hakuna kipimo kamili,
ila kanuni zinasema urefu ni
baina ya mita 90 na 120, upana kati
ya mita 45 na 90. Kwa michezo ya kimataifa urefu uwe baina ya mita 100 - 110 na
upana baina ya mita 64 na 75.
Goli ziko kwenye pande fupi zaidi. Kuna alama ya bendera kwenye
kona zote 4 za uwanja. Mwaka 2008 IFAB ilijaribu kusanifisha vipimo kuwa
mita 105 kwa 68, lakini kanuni hii ilisimamishwa baadaye.
Mstari ni mpaka wa uwanja. Wakati mpira uko kwenye mstari hata
kwa kiasi kidogo unahesabiwa bado uko ndani ya uwanja. Kwa goli kukubaliwa
sharti mpira uwe umepita mstari wa goli kabisa.
Kuna wachezaji wa aina tatu: walinzi, wachezaji
wa kiungo na wachezaji
wa mbele au straika. Goli kipa au mlinda
lango ni mmoja kati ya walinzi.
Ni uamuzi wa kocha kuhusu idadi ya wachezaji wa kulinda lango, wa kiungo au wa
mbele, ikitegemea mfumo uliotumika. Mfumo wa 4,,4,,2 umekuwa maarufu
miongoni mwa timu nyingi. Mfumo huu hujumlisha walinzi wanne pamoja na mlinda
lango, wachezaji wanne wa kiungo na wawili wa mbele. mshambuliaji lazima akawa
mtu mwenye ujuzi mkubwa na mwenye nguvu za kushambulia
Katika ligi za
kitaifa na kimataifa, alama hutunukiwa kwa timu baada ya mchezo. Timu
iliyoshinda hupewa alama tatu huku timu
zilizotoka sare hupewa alama moja kila moja.
Ikiwa ni lazima mshindi apatikane, hasa kwenye mechi za finali,
mchezo huwa na muda wa
ziada kama timu hizo ziko sare.
Iwapo sare hiyo huendelea mchezo huamuliwa kwa mikwaju ya penati.
Shirikisho
la Soka Duniana (FIFA) ndilo shirikisho kuu linalosimamia kandanda duniani. Wanachama
wake ni mashirikisho ya kandanda ya nchi mbalimbali. Kufikia mwaka wa 2000,
lilikuwa na wanachama 204 kutoka pembe zote za dunia. Shirikisho hili huandaa
mashindano mbalimbali ya soka kama vile Kombe la Dunia la
FIFA na pia huwatunuku wachezaji.
Huu ni mchezo wa mpira wa miguu (football),michezo mingine inafuata
hiyo basi usiache kutufolow kwa makala taamu na mbalimbali za michezo.
Share wengine nao waujue na waikumbuke.
No comments:
Post a Comment