#AFYA
Ugonjwa wa selimundu unasumbua
wengi, umetengua ndoa za wengine, kwa sababu ya kutojua.
Hakuna shaka kwamba
umewahi kusafiri nje ya nchi yako na kutakiwa kupata chanjo.
Kwa wengine, chanjo
hiyo ikiwamo ya homa ya ini imeonekana kama usumbufu na udhia mtupu. Hata
hivyo, wapo wengine ambao hawaufahamu ugonjwa huu.
Kwa wanaoujua,
wanahofia kuwa ugonjwa huu una madhara makubwa pengine kuliko saratani na
Ukimwi.
Homa hiyo au
Hepatitis B inapewa uzito mdogo licha ya kuwa ni ya hatari kubwa.
Wataalamu wanaeleza
kuwa Hepatitis B au homa ya ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi, wenye
madhara makubwa na wenye uwezo wa kuambukiza kwa wepesi kuliko Ukimwi.
Kitaalamu, ugonjwa
huu, husababishwa na virusi vya Hepatitis B (HBV) ambavyo huathiri mfumo
wa utoaji wa sumu mwilini. Inaelezwa kuwa robo tatu ya watu ulimwenguni
wameathiriwa kwa muda na homa ya ini na wengine milioni 350 wameathirika moja
kwa moja.
Takwimu zinaonyesha
kuwa homa ya ini hu ua watu 600,000 kila mwaka katika sehemu mbalimbali, idadi
ya watu inayolingana na wale wanaokufa kutokana na malaria.
Maradhi haya ya ini
yanaelezwa kuwa yanaweza kusababishwa na kunywa kileo kupita kiasi au sumu inapoingia mwilini.
Hata hivyo, mara
nyingi ugonjwa huu husababishwa na virusi.
Wanasayansi kwa
upande mwingine wamegundua virusi vitano vinavyosababisha ugonjwa huu na
wanasema kwamba huenda kuna vingine vitatu.
Matokeo yake, sheria
zimewekwa katika nchi mbalimbali ambazo zinamtaka kila raia mgeni
anayetaka kuingia katika nchi husika, kupata chanjo ya ugonjwa huu ili kuepusha
maambukizi.
Kila
anayechanjwa hupewa kadi maalum itakayomwezesha kuingia katika nchi
husika ili kuthibitisha kuwa amechanjwa.
Hatari kubwa ya
ugonjwa huu inatajwa ni namna ya uambukizaji wake ambapo, unaposhika damu au majimaji ya mwilini ikiwemo mbegu za uzazi huweza
kuambukizwa.
Wataalamu
wanaeleza ubaya wake ni kuwa unaweza kuambukizwa kwa kufanya ngono na hata kwa kushika majimaji
ya mwili wa mtu aliyeathirika ikiwemo damu, mate, machozi na mkojo.
Taarifa za Shirika la
Afya Duniani(WHO) zinaeleza kuwa kirusi cha homa ya ini kinaweza kuishi
nje ya mwili wa binadamu kwa siku saba na kwa
wakati huu, kirusi hiki kinaweza kusababisha maambukizi iwapo mtu hajapata
chanjo ya kuuzuia.
Watanzania wengi bila
kujua wamekuwa wakiugua maradhi mbalimbali yanayosababishwa na homa ya ini na
bila kufahamu ini limekuwa likiathirika taratibu.
Huenda dalili zikaonekana waziwazi miaka mingi
baada ya mtu kuambukizwa. Zinapoonekana, huenda tayari ini limenyauka au lina
saratani na magonjwa hayo huua asilimia 25 ya watu walio na virusi vya HBV.
Aidha, dalili kuu zinazojulisha kuwa mtu ana homa ya
ini ni kutapika, kuchoka kupita kiasi, kuathirika kwa
ini, homa na mkojo kuwa wenye rangi ya njano iliyokolea sana.
Unaweza kuharisha na kutapika au kupata maumivu katika eneo fulani la
tumbo lako, macho na ngozi kuwa vya njano.
Homa ya ini aina ya
B, inaweza kuingia mwilini mwa mtu kwa njia ya ngono, kama ilivyo Ukimwi na
magonjwa mengine ya zinaa. Hivyo basi, majimaji katika mwili
wa mwanadamu yanaweza kuwa chanzo cha maambukizi.
Watu wengi
wanaendelea kuambukizwa kwa kutiwa damu yenye virusi hivyo, hasa katika nchi
ambako hakuna vifaa bora vya kuchunguza virusi hivyo katika damu. Virusi vya
HBV vina uwezo mkubwa zaidi wa kuambukiza kwa kulinganishwa na virusi vya
Ukimwi.
Hata kiasi kidogo cha
damu yenye virusi hivyo kama ile inayobaki kwenye wembe,
inaweza kupitisha virusi hivyo na tone la damu iliyokauka kwa juma moja au hata
zaidi inaweza kumwambukiza mtu virusi hivyo.
Madhara mengi huweza
kumkumba mtu aliyepata maambukizi ya homa ya ini, kwani anaweza kupata shinikizo la damu, anaweza kuathirika
ubongo au hata kupooza sehemu ya mwili wake.
Angalizo ambalo
wataalam wanaeleza ni kuwa baada ya mtu
kuambukizwa homa hiyo, hawezi kupona, kwani dawa kuu ya ugonjwa huu ni chanjo
ya kuzuia homa ya manjano (yellow fever vaccination).
TANBIHI:Hakikisha kabla ya kuoa/kuolewa mnapima maradhi
tofautitofauti wewe na mwenziwako.Tahadhari kuchangia vitu vyenye ncha kali na
uepuke zinaa.
No comments:
Post a Comment