#UKWELI ULIVYO
MBILIKIMO/VIOMOLO/VIBURUSHUTI
Yaani watu bila kimo cha chini mno;
ni binadamu wa
makabila ambayo miili yao ni mifupi kuliko kawaida. Wataalamu wanatumia jina la Kiingereza lenye
asili ya Kigiriki Pigmy.
Watu
wa aina hiyo wa kwanza kufikiriwa ni wale wa Afrika ya Kati, kama vile Waaka, Waefé na Wambuti, pamoja na Watwa wa Rwanda na Burundi. Kumbe
kama kipimo kinachotumika ni sm. 155, kuna
makabila ya namna hiyo hata Australia, Thailand, Malaysia, fungu visiwa vya Andamani (India), Indonesia, Ufilipino, Papua Guinea mpya, Bolivia, Brazil na Asia
Kusini-mashariki.
Makabila
ya Wabilikimo yanapatikana Rwanda, Burundi, Uganda,(anitwa Teuso) Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC)(anaitwa Kimbundu), Jamhuri ya Kongo (ROC), Jamhuri ya Afrika
ya Kati, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Angola, Botswana, Namibia, Madagaska Afrika ya kusini (anaitwa Koikoi) na Zambia.
Makabila
ni tofauti kati yake, lakini ni tofauti zaidi sana na binadamu wengine. Vipimo
vya DNA vinadokeza kwamba wana asili moja, ya zamani sana kati
ya miaka 60,000 iliyopita yaani kuliko
aina nyingine zote za watu isipokuwa Wasani.
Mbali
na makabila ya mbilikimo, kuna watu katika makundi yoyote ya jamii ambao
wanaweza kuwa wafupi kupita kiasi kwa sababu 300 na zaidi tofauti za kiafya. Mtu wa namna hiyo kwa Kiingereza anaitwa dwarf.
Bado watu
hawa kwa jamii kubwa inasadikika wanaishi msituni na maisha yao ni ya
kijamaa.Hupenda saana kuwinda yaani ndio
maisha yao na uvuvi bila kusahaulika.Kuna wakati ilisemeka kuwa wanakula watu
walio tofauti na wao ki kimo…..Ni uzushi tu.Si
maneno ya kweli.
No comments:
Post a Comment