#AFYA
Kuna baadhi ya wanawake wenye kuonesha
dalili za mimba punde tu katika wiki kadhaa baada ya kushika mimba. Kuna
maswala mengi kuhusu upataji mimba na ni siku gani mwanamke anaweza kupata
mimba. Hebu tujadiliane kwa ufupi. Hedhi yaani mensturation period, ni wakati
mwanamke anaweza kujua ya kuwa hana mimba.
Damu inayotoka wakati huu huwa
nyekundu. Damu hii hutoka kila mwezi kwa wanawake walio na mzunguko wa
kawaida. Pia damu hii huchukua siku tatu hadi tano kwa wale wenye mzunguko wa kawaida.
Unapokosa hedhi, baada ya siku kadhaa kupita uliposhiriki tendo la ndoa kwa
wana ndoa na ngono kwa wazinifu, kuna dalili kubwa ya kuwa umeshika mimba.
Ni vyema kujua jinsi ya kujichunga
ili wewe na mwanawe muwe salama. Hata kabla ya kukosa hedhi
(mensturation/period). Unaweza kudhani au kutumai una mimba. Tumaini ni kwa
wale wanaopenda kupata watoto. Wakati mwingine, mimba huja na hofu, haswaa
ukiwa umefanya mapenzi kando ya ndoa. Lakini usitie shaka, mtoto ni baraka na
ni lazima na wajibu wa kila mzazi kujua wanapotarajia mwana.
Dalili za mimba kwa wanawake wengi
huonyesha katika wiki za kwanza wanapopata mimba. Hizi dalili ni tofauti kwa
kila mwanamke. Kuna wale ambao huwa na machungu na magonjwa zaidi ya wengine na
kuna wale wanaopitia hali hii kwa njia rahisi mno.
Swali ambalo kila mwanamke anaweza
kuwa nalo ni, Je ninaweza kushika mimba wakati nina hedhi?
Jibu la hakika ni ndiyo! Ingawaje
wanawake wengi hawawezi kushika mimba wakati wana hedhi. Kuna baadhi ya wengine
wanaoweza kushika mimba wakati wanashiriki mapenzi hedhini. Hii si kawaida kwa wengi lakini
kulingana na dakitari Jeannnette Lager, M.D, MPH aliyesomea maumbile ya
wanawake, anatueleza jinsi mwanamke anaweza kushika mimba wakati ana hedhi, sana
sana kwa wale walio na mzunguko mfupi zaidi yaishirini na nane.
Haya basi hebu tufafanue zaidi juu
ya ugunduzi ya kuwa umeshika mimba.
Dalili zifuatazo za
mimba ni maagizo tu ya kuelewa jinsi unavyoweza kukumbatia hali yako ukiwa na
mimba.
- Kukosa Hedhi (Missed Period)
- Utoaji damu mwepesi (light spotting/implantation bleeding)
- Kufura kwa Matiti (swollen Breasts)
- Mhemko wa hisia (Mood swings)
- Kutoa hewa ( lots of gas)
- Kutapika au kuhisi kutapika (Nausea and vomiting)
- Kufura tumbo (bloating)
- Kukojoa kila wakati (frequent urination)
- Constipation (Kuvimbika)
- Mgongo kuuma upande wa chini (lower back pain)
- Kuumwa kwa kichwa (headache)
- Kuzidi joto (increase of basal temperature)
- Uchovu (fatigue)
- Kutamani aina ya vyakula (food cravings)
- Kulia (crying)
- Kulala mara kwa mara (sleepiness)
Urahisi
na kufura Matiti
Matiti yako yanaweza kuonesha
dalili za kwanza ya mimba. Wiki mbili baada ya kupata mimba, mabadiliko ya
homoni yanaweza kufanya matiti yako kuwa makubwa kuliko kawaida, unaweza kuhisi
kujikunakuna na uchungu kiasi, pia unaweza kuhisi kama matiti yako yamejaa au
mazito.
Uchovu
Uchovu umekuwa hali na dalili ya
kwanza mno kwa wanawake wajawazito. Homoni inayoitwa Progesterone huongezeka
kwa wingi na inaweza kukufanya kuhisi usingizi kila wakati. Pia upunguzaji wa
sukari katika damu, upunguzaji wa shinikizo la damu (blood pressure) na
uzidishaji wa damu unaweza kukufanya uwe mchovu wakati wa mimba.
Utoaji
damu nyepesi na uchungu kwa tumbo la uzazi
Kuna wakati, damu mwepesi (spotting)
huwa dalili ya mimba mapema. Damu hii huwa nyepesi mno na haiwezi kulinganishwa
na ile ya hedhi. Rangi ya damu hii ni waridi au kahawia kulingana na hali ya mwanamke.
Wakati mbegu ya mwanaume na zile za mwanamke zinapokutana kumtengeneza mtoto,
mwanamke anaweza kutoa damu nyepesi kuonesha ya kwamba mwana amelazwa vyema
katika tumbo la uzazi wa mwanamke.
Damu hii huchukua siku chache sana
kutoka kulinganishwa na ile wa hedhi. Kuna wanawake wengine wenye hukosa
kuonesha damu hii nyepesi wanapopata mimba. Sio lazima wanawake kutokwa damu
wanaposhika mimba. ni muhimu kuelewa ya kuwa mwili wa kila mwanamke ni
tofauti. Pia, uchungu katika tumbo la uzazi wakati mimba hutengenezeka, unaweza
kufanana na ule wa hedhi.
Kuhisi
kutapika
Ugonjwa wa asubuhi (morning
sickness) unaweza kufanyika wakati wowote wa siku. Kuna wanawake waliosemekana
kubeba mimba ambao huwa na ugonjwa huu hivi punde wanapoamka. Kuna wengine
wanaopata ugonjwa huu wakati wa mchana na wengine wakati wa usiku. Kila
mwanamke ana utofauti kulingana na maumbile ya mwili wake.
Wanawake wengi kwa jumla hupata
(morning sickness) wiki mbili wanaposhika mimba. Kutapika huwa matokeo ya
homoni inayoitwa estrogen inapoongezeka mwilini. Kuna wanawake wengi ambao
hunusa harufu za aina mbali mbali, kama vile marashi, vyakula mbali mbali kama
mayai, kwa haraka na pia harufu zingine huwafanya kuhisi kutapika.
Ukiwa unahisi kutapika, unaweza kula
au kunusa ndimu au kula matunda kama ndimu, mizizi kama tangawizi na pia
kuhakikisha una kunywa maji mengi kwa wakati huo.
Kuna wanawake wengine husema
wanaweza kuhisi ladha ya chuma ulimini mwao. Haya yote ni kwa sababu homoni
estrogen imeongezeka mwilini baada ya mimba.
Kutamani
vyakula vya aina au Kukataa
Ukiwa umeshika mimba, unaweza
kutamani vyakula fulani, ilhali kuna vyakula mbali mbali ussivyovipenda.
Kuna wanawake wengi waliopenda mayai
na sasa hata harufu ya mayai huwafanya kutapika. Na kuna wale wanaoanza kupenda
matunda au vyakula vya aina mbali mbali wanapokuwa wajawazito.
Haya yote ni kwa sababu ya
mabadiliko ya homoni mwilini, haswa kwa muhula wa kwanza mwezi mmoja hadi mitatu
ya mimba. Pia unaweza kuhisi njaa wakati wowote wa siku. wanawake wengi
ulimwenguni huanza kula zaidi ya kawaida na hii ni ishara kubwa ya kwamba
mwanamke amepata ujauzito.
Kuvimbiwa
(constipation)
Hali ya kutoenda haja kubwa ni
kawaida kwa mwanamke yeyote aliye na mimba. Dalili hii ni ile kati ya kwanza
wakati mwanamke amepata ujauzito. Homoni Progesterone hufanya chakula kuenea
polepole kwenye matumbo na hii husababisha ugumu wa kuenda haja kubwa.
Mhemko
wa hisia
Katika muhula wa kwanza wa mimba,
utaweza kupata mhemko wa hisia. Unaweza kuhisi furaha halafu baada ya muda mchache
wahisi huzuni. Kuna wakati mwingine unaweza kujikuta unalia kwa mambo madogo
sana. Haya yote ni kwa sababu mwili wako unapitia mabadiliko kuweza
kumtengeneza mtoto.
Kuhisi
Kizunguzungu
Wakati damu linaongezeka na
shinikizo la damu kupunguza, unaweza kusikia kichwa chepesi au kizunguzungu
wakati wa kwanza kama dalili ya mimba. Wakati mwingine, ukosefu wa sukari kwa
damu unaweza kufanya mwanamke mja mzito kuzirai.
Ni muhimu wakati unaposikia uwepesi
wa mwili, kuketi chini au kujilaza na kuweka miguu juu ya mto ili damu iteremke
kichwani. Pia kuhakikisha unakula kila wakati uhisipo njaa; hii husaidia kupunguza
hali hiyo.
Kuhisi Joto
kali
Unapoamka, joto la mwili wako huwa
la kawaida kila siku. Unapopata mimba joto hili hugeuka na kuwa jingi kuliko
kawaida. Baada ya kuwa na hedhi, kuna wakati mwanamke huwa tayari kupata mimba
wakati huu, joto la mwili huongezeka halafu hurudi kuwa la kawaida baada
ya wiki mbili.
Ukigundua kuwa joto hili
halijapungua baada ya wiki mbili, basi una dalili kubwa kuwa na mimba
kama umeshiriki ngono bila kinga.
Kukosa
hedhi
Baadhi ya dalili nyingi mwilini mwa
mwanamke aliye na mimba, kukosa hedhi ni ile wa kwanza mno haswaa kama (Period)
yako ni ya kila mwezi. Utaweza kugundua umekosa mwezi wakati unapojua vyema
umefanya ngono bila kujikinga.
Kujawa
na hewa
Ni kawaida kwa mwanamke aliye na
mimba kuhisi kana kwamba amejaa hewa tumboni na pia kutoa hewa hapa na pale (kujamba). Hii ni kwa sababu tumbo la uzazi linapanuka
kuhakikisha mtoto yuko na mahali pa kukua na kuzunguka.
Kuongezeka
kwa hamu ya kula
Wanawake wengi wanapopata mimba,
ingawaje wengi wao huwa wagonjwa na wanahisi wasile vyakula kila wakati, mwanamke
akifikisha muhula wa pili, hamu ya kula huongezeka.
Sababu ya hamu kuongezeka ni, mtoto
aliye tumboni anahitaji chakula pia. Unaweza kuona mama aliyekula chakula
sahani moja, anaanza kula sahani moja na nusu na baada ya muda si mrefu anahisi
njaa tena.
Homoni zilizo mwilini hubadilika na
kumfanya mwanamke aliye na mimba kuwa na hamu ya kula kila wakati ili mtoto
aweze kupata nguvu na kukua vema.
Kulala
mara kwa mara
Wakati mwanamke amekuwa mja mzito,
Homoni (progesterone) huongezeka zaidi mwilini. Tulivyonena hapo mbeleni, homoni
hii hufanya kazi mwilini kuzembea.
Hii ndio sababu ya wanawake wengi
walio na mimba kuhisi usingizi kila wakati. Tukumbuke kuwa, mwana/mtoto
anayetengenezwa chupani mwa mamake, anahitaji nguvu zote ili kujistahimili.
Akina mama wanaochukua muda wa
kupumzika huwasaidia wanawe kukua kwa njia bora. Pia, afya ya mama huongezeka
anapochukua muda wa kulala wakati ana mimba.
Unawezaje kujua kuwa una mimba?
Baada ya kufanya ngono bila kinga,
na wakati mwanamke amefikisha umri wa kupata mimba wakati msichana huanza
mzunguko wa hedhi akiwa na dalili zote
zilizotajwa hapo awali, jaribu kwenda na kuhakikisha na daktari ili isiwe
ni alama ya chanzo cha ugonjwa fulani na wala si mimba.
Ni muhimu kuhakikisha una mimba
wakati unapofikiria u mjamzito. Pia ukisha pata uhakikisho, unaweza kuchukua
vipimo bora vya kujitunza wewe na mwanao.
Mwanamke yeyote aliyegundua yuko na
mimba anahitajika kutibiwa vyema na wale walio karibu naye. Kila mwanamke
anastahili kuoneshwa heshima haswaa wale wanaobeba maisha ndani yao.
Imeaminika mwanamke aliye na furaha
kila wakati anapokuwa na mimba huweza kuzaa vizuri na watoto wao pia huwa na
furaha.
Tanbihi:Mama
mjamzito ahakikishe anapata chakula bora na salama bila kusahau mazoezi mepesi
ili uzao wake uwe bora na salamaa..
Wasambazie na wengine waelimike..
No comments:
Post a Comment