#ELIMIKA
Bangi ( bhang, bhangi kwa Kihindi )
ni majani ya mmea wa kike wa mbangi (Cannabis).
Ndani yake mna dawa inayosababisha ulevi unaotegemea kiasi cha dawa kinachoingia mwilini. Hata hivyo ina uwezo wa hali ya juu kukabiliana
na magonjwa sugu
kama vile kansa, kusaidia
mgonjwa mwenye maumivu makali sana na kuongeza hamu ya kula kwa mgonjwa wa
Upungufu wa Kinga mwilini (UKIMWI). Pia bangi ina saidia kusawazisha kiwango cha
presha.
Hutumika pia kwa mapishi pamoja
na maua . Hutumika kama kinywaji, kiungo ndani ya vyakula au
huvutwa.
Bangi mwanzoni ilitumika kama sehemu ya ibada ya Uhindu nchini India mnamo mwaka wa 1000 KK na baadaye ikawa sehemu muhimu ya utamaduni wa Kihindi.
Katika nakala ya zamani ya Atharvaveda, bangi inaelezwa kama mitishamba ya manufaa ambayo humaliza wasiwasi.
Maandalizi ya bangi yalikuwa takatifu kwa miungu, hasa Shiva. Moja wa sitiari za Shiva ni Bwana wa Bangi na inasemekana ni yeye aliyegundua mchanganyiko huu.
Katika kumuiga Shiva, wengi wa Wasadhu hutumia bangi kuongeza uwezo wa
kutafakari na kufikia hali ya juu kabisa kiroho. Bangi au boza
ni maarufu pia miongoni mwa Wasufi kama msaada wa kutoka nje ya nafsi.
Katika desturi asilia za Uhindi mavuno na maandalizi huja wakati wa maadhimisho
ya Holi mwezi Machi na Vaisakhi mwezi Aprili, hivyo kuhusishwa na bwana Shiva. Imekuwa sawa na Holi, mpaka kuvuta bangi wakati
huo ni kitu cha kawaida.
Wakati mwingine fuwele
hutenganishwa na majani na matumba ya Cannabis. Bangi inayochangamsha akili husaidia kueneza roho ya Holi, tamasha ambayo
hailazimishi vikwazo vyovyote. Thandai, Pakoras na Vadas, yote mapochopocho
ya kiutamaduni yenye bangi kama kiungo muhimu, huonjwa na kila mtu siku hiyo.
Bhang Ki Thandai (Kihindi) ni kinywaji maarufu katika maeneo mengi ya
India ambacho hutengenezwa kwa kuchanganya bangi na Thandai, kinywaji baridi
kitayarishwacho kwa karanga, masala, maziwa na sukari.
Mila ya kutumia bangi wakati wa Holi ni kwamba
hasa Kaskazini mwa India ambapo Holi yenyewe huadhimishwa kwa pupa huku
haijulikani mahali kwingine.
Walakini bangi hutumiwa sana kule Varanasi au Chembada, nchi ya Shiva, ambapo bangi hutayarishiwa kwenye
ngazi zake maarufu.
Popote kwenye ngazi, mtu anaweza kupata idadi kubwa ya wanaume wanaohusika katika mchakato wa kuandaa bangi.
Kutumia kinu na mchi, matumba na majani ya Cannabis
husagwa na kuwa uji mzito wa kijani. Kwa mchanganyiko huu
maziwa, siagi, na masala huongezwa. Wigo la bangi sasa ni tayari
kufanywa kinywaji kinacholewesha, Thandai, mbadala kwa pombe.
Bangi pia huchanganywa na siagi na sukari kufanya uji wa kijani, na pia
vipira vidogo vya kutafuna vinavyowasha, viitwavyo 'golees' ambavyo kwa mantiki hii inamaanisha peremende au kidonge katika Kihindi.
Kwa vile ni ya kale, bangi imekuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa India
hata imekuwa kiashirio cha mambo mengi.
Bangi huhusishwa na bwana Shiva kwani mmea wa Hampa hujulikana kama mtakatifu kwa Wahindu wa
Kaskazini mwa India. Kuna hata imani kwamba kukutana na mtu aliyebeba bangi ni ishara mbaya ya kufanikiwa. Na kama hamu ya mmea wa Hampa kunaashiria furaha, kuuona
katika ndoto kunahakikisha mafanikio kwa mtu katika siku
zijazo. Pia, kutembea juu ya jani takatifu la bangi huaminika kuashiria mabaya.
Watu wanaamini katika mali ya dawa ya mmea wa Hampa. Ikitumiwa kwa
kiwango sahihi, inaaminika bangi kutibu homa, kuhara na sunstroke, kutoa kikohozi, kuharakisha kusagwa kwa chakula tumboni, hamu ya chakula, kutibu kasoro za kuongea kwa utata,
kufanya mwili kuelewa yanayoendelea.
Baadhi ya michoro ya mapenzi kutoka kipindi cha Mughal cha India huonyesha wanandoa wakifanya ngono huku wakivuta bangi kuongeza ashiki(nyege).
Nchini Nepal, siku ya tamasha ya Wahindu ya Matta Shivaratri, bangi
hutumiwa katika aina mbalimbali kama moshi, kuchanganywwa na pipi au kinywaji. Kutoa sadaka ya bangi kwa bwana
Shiva ni kawaida wakati wa tamasha hiyo.
Singa singa/kalasinga
Wanihang kutoka jadi wanapenda bangi sana, ambayo wanaiita Sukkha Prasad yaani apatianaye amani. Katika Kisanskriti neno "Sukhi"
humaanisha furaha na "Prasad" ni sadaka kwa mungu ambayo ameionja na kuamua kugawana
na kerende.
Ilikuwa ikitumiwa kutuliza maumivu kabla na baada ya vita kwa vile wengi wa wa Nihang wakirudi
wangekuwa na majeraha makubwa. Kalasinga hufunzwa kuitumia kama dawa badala ya burudani.
Imani zetu
Matumizi ya bangi na vitu vya kuchangamsha akili vimekatazwa na baadhi
ya madhehebu ya dini ya Kihindu kama vile Shikshapatri, pia ni haramu katika Uislamu, na ni dhambi katika Ukristo. Hata hivyo, imani nyingine kama vile Rastafari wanaichukulia bangi kama vile sakramenti.
Aidha mila za mababu zimeiharamisha bangi toka zamani mpaka serikali nyingi ziliweka bangi katika kundi moja na
baadhi ya madawa ya kulevya yaliyo
hatari zaidi, kama vile kokeini, heroini n.k.
Hata sheria za nchi nyingi kuanzia karne ya 20 zimetungwa ili kukataza au kubana kilimo, matumizi na uuzaji wa bangi kutokana na matokeo
mabaya mbalimbali, hasa uraibu.
Lakini tafiti za kiafya zimethibitisha madhara makubwa na hatari zaidi
kwa afya kutokana na matumizi ya sigara, ikifuatiwa na pombe huku bangi ikiwa afadhali zaidi ya vilevi
vingine. Basi, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na ufahamu kuongezeka, asilimia kadhaa za wasomi pamoja na watafiti sasa
wanadili na uhalalishaji wa matumizi ya bangi kwa watu wazima, na tiba kwa watu wote.
Uruguay ndiyo nchi ya kwanza duniani kuhalalisha
biashara, matumizi na upandaji wa bangi. Nchi nyingine ambazo
zimehalalisha bangi ni pamoja na Jamhuri ya Czech, Kolombia, Ecuador, Mexico, Ureno, Canada,nk.
Leo ni bangi/marijuana/ganja na majina
mengine mengi ambayo huzuka na kupotea. Usiache kutufollw kwa vitu vizuri.
Share na wengine waijue bangi
No comments:
Post a Comment