FAIDA ZA BUSU KIAFYA - waleo blog

Breaking

Sunday 23 February 2020

FAIDA ZA BUSU KIAFYA


#Mahusiano

Busu ni kitendo cha binaadamu,wanyama,ndege na wadudu,jinsia ya kike au ya kiume  kwa baba ama mama,mke ama mume au rafiki kwa rafiki kupeleka mdomo wake il-hali akiukusanya pamoja na kuukunja akiuelekeza sehemu yoyote ya mwili aipendayo na kuigusa kwa mdomo huo  huku ukitokea mlio.”kuhusu ndege na wadudu kupigana mabusu hili tuwatafute wataalamu wa elimu za viumbe hivyo”
Leo nitagusia katika mabusu ambayo hupigana wapendanao na faida zake.

1. Husaidia kuiboresha afya yako
Unampombusu mkeo au mmeo kwa moyo wote na hisia zote hapa tunaongelea kumbusu kutoka moyoni
(kula denda), unapata faida kubwa kiafya ambao kitaalam tendo hilo huweza kusaidia kukupunguzia maumivu ya kichwa kwa kupumzisha taratibu misuli. Pia kitaalamu tendo la busu hukusaidia  kuingarisha ngozi yako kama inavyofanyika kwa mtu anaependa mazoezi. Hivyo basi unapotaka kulala, ni vyema ukambusu kwa hisia mkeo/mmeo upate faida hizi badala ya kumpotezea na kumrukia wakati wa tendo la ndoa.

2. Husaidia katika ufanyaji kazi wa virutibisho mwilini
Inaelezwa kuwa busu husaidia sana mwili kufanya mrejesho ambao unadhibiti ufanyaji kazi wa virutubisho mbalimbali mwilini hivyo inaweza kusaidia katika kuboresha afya yako zaidi.
3. Busu huongeza furaha na kupunguza msongo wa mawazo.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa; inaelezwa kuwa tendo la busu huongeza kitu kinachojulikana kama ‘endorphins’, na endorphins husababisha mtu kuwa  furahi. Kama hivyo ndivyo, kwa nini usiitafute furaha kwa mwenzi wako kwa njia mojawapo ya kujisikia raha kwa kumbusu tu.
Sio hivyo tu, unapoongeza furaha, unapotuliza akili na kuachia hisia zako kwa tendo la busu unapunguza kwa kiasi kikubwa msongo wa mawazo ambao ni chanzo cha magonjwa mengi.
4. Busu huongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa
Moja kati ya mambo ambayo yanaweza kuwasaidia wanandoa kujiandaa kwa pamoja na kupata hamu ya tendo la ndoa zaidi ni busu. Hii ni kwa sababu tendo hili hufanywa kwa pamoja na wawili hao huku kila mmoja akivuta hisia kwa nguvu asiyoifahamu.
Mtaalam mmoja wa masuala ya uhusiano aliwahi kutaja ‘busu’ kama tendo linaloongeza mihemko zaidi ya tendo  wakati wa maandalizi ya tendo la ndoa.

5.Busu huongeza mapenzi ya dhati.
Tendo la busu huwafanya wanandoa kuwa katika hali ya umoja zaidi kihisia. Hali hiyo huwaongezea upendo moyoni kwa kuwa tendo hilo huongea zaidi  maneno na ndio maana wakati wa tendo hilo ukimya hutawala na hisia huongea zaidi.
Kabla mama yangu kufariki aliwahi kusema kuwa, ‘tunawabusu tunaowapenda, na tunawapenda tunaowabusu’. Mbusu mkeo/mmeo na mtoto kwa dhati uwe katika nafasi ya kuongeza na kuimarisha mapenzi yenu.

Hata hivyo, unapaswa kuchukua tahadhari na kuwa na busara pale unapotaka kufanya tendo la busu na mwenzi wako kwa kuwa tendo hili kwa utamaduni wa kiafrika huhitaji  faragha  na huleta ukakasi linapofanyika hadharani.
Ni muhimu sana kuwa mwaminifu kwa mtu unayembusu maana kumbusu mwenzi wako pekee kwa kuwa kuna magonjwa mengi yanayosambaa kutokana na tendo hili vikiwemo virusi vya ukimwi. Mshauri mwenzi wako atunze vyema kinywa chake kwa kuzingatia kusugua meno kwa usahihi kabla na baada ya kula.
Wape faida hii na wenzako  wafahamu kwa kuisambaza.

No comments:

Post a Comment

Pages