#GHAIBU
Ndani ya makala hii,huenda baadhi ya istilahi zikakukera, tusameeane.
Uchawi (Witchcraft)
Ni vitu visivyoonekana
kwa macho ya kawaida,isipokuwa kwa uchawi wenzake au ucha mungu.’’Kwa maana hii
inatufumbua ya kuwa,mtu akikwambia kuwa ni mchawi,basi na yeye ni mchawi.Ima anao ndani ama ameenda kwa mganga(mchawi wa wachawi) kukutazama(kupiga ramli), pia nao ni uchawi haufai kufuatwa na tujiepushe nao maana
unaangamiza’’Ucha mungu;ni hali ya kumtaja mungu kila wakati ima ukawa kanisani,msikitini
na nyumbani.Kwa kitendo hiki cha kuwa karibu na mungu kwa utulivu;Mungu akitaka
anaweza kukuonesha vitendo vya kichawi vinavyofanywa kwako...Uchawi; ni nguvu zinazotumiwa na watu wenye maarifa
maalumu yasiyo ya kisayansi katika jamii nyingi duniani, zikiwemo
za Afrika, Asia, Ulaya n.k., ingawa kuna tofauti nyingi
kulingana na mahali au utamaduni.
Lengo lake ni kujaribu bahati,majalibu kwa watu
na kujilinda na maadui wengine kimazingara, au kwa ajili ya
kujifurahisha, japo wenye imani potofu
hulichukulia maanani na kupandikiza chuki kwa ndugu jamaa hata jirani kuwa ni
mchawi.
Kwa mujibu wa vitabu vya dini, uwezo na nguvu zote za asili ni
za muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo, hivyo yeye
anampa mwanadamu uwezo tofautitofauti kama apendavyo, kwa maana uwezo
huo hufanya kazi katika hali ya
kubahatisha, yaani ni bahati, hakuna mwenye mamlaka ya kuongoza
uwezo huo wa asili ila Mwenyezi Mungu.
Hebu tuutazama Uislamu na historia ya uchawi na walioufundisha.
Baada ya kifo cha
Mtume Sulayman bin Daud a.s (mfalme)., Ibilisi alitengeneza uchawi kisha kuuviringa na
nyuma yake aliandika kuwa; mzigo huu umetengenezwa na Asif bin
Barkhiyyah kwa ajili ya ufalme wa Mtume Suleyman, na kwamba imetolewa kutoka
hazina ya ilimu. Na kwa nguvu zake kila jambo linawezekana. Na baada ya hapo aliifukia chini
ya kiti cha Mtume Sulayman a.s. Na baadaye aliifukua chini ya kiti hicho
na kuidhihirisha mbele ya watu wa zama hizo. Kwa kuyaona hayo, wale waliokuwa
wakimpinga mfalme Selemani a.s. walianza kusema kuwa Mtume Suleyman a.s.
aliweza kuwatawala kwa uchawi lakini wale waliokuwa waumin walikuwa wakisema
kuwa Mtume Sulayman a.s. alikuwa ni mjumbe wa Mungu swt na mwenye imani.
Mwenyezi Mungu swt anatuambia kuwa ni shetani ndiye asemaye kuwa Mtume Suleyman
a.s. alikuwa ni mchawi. Na jambo hilo ndilo walilolifuata na kuliamini
Mayahudi. Lakini Mtume Suleyman a.s. kamwe hakufanya tendo lolote la kukufuru
au la ushirikina hivyo kamwe hawezi kuwa mchawi. Wale wanaohalalisha uchawi ni
wapingaji kwa sababu Mashetani walikuwa wakifanya uchawi na kuwafundisha watu
uchawi na ushirikina.
Baada ya kupita zama za Mtune Nuhu
a.s., kulikuja zama moja ambamo wakazi wake walikuwa wakijishughulisha mno na
mambo ya uchawi na ushirikina, kwa sababu ya kufuata imani hizo zilizopotofu,
kulikuwa kukitendeka matendo maovu kabisa. Hivyo wakazi walikuwa wameupuuzia
ujumbe aliokuja nao Nuhu a.s,, na kwa hayo Mungu mtukufu aliwatuma malaika
wawili waliokuwa wakiitwa Harut na Marut, ambao walitumwa katika mji
uitwao Babul, katika maumbile ya mwanadamu ili waweze kuwazuia wanadamu
wasiendelee na uchawi na ushirikina uliokuwa umepindukia kiasi.
Malaika hao walitii amri ya Mungu mtukufu na walimwelezea Mtume wa zama hizo kuwa uwafundishe mambo fulani fulani
wakazi wako ili waweze kujiepusha na uchawi na ushirikina huo uliokuwa
umewapotosha kabisa. Basi Mtume huyo aliwaambia watu wake kuwa wajifunze
mafunzo hayo makhsusi ili waweze kujiepushe na uchawi na kamwe wasiwatendee
chochote wenzao. Mungu mtukufu anatuambia kuwa katika mji huo wa Babul
kulikuwapo na Mayahudi ambao wao kwa hakika walikuwa wakitenda kinyume na kile
walichokuwa wakiambiwa na Mtume huyo, yaani wao badala ya kuutokomeza uchawi,
wao ndio wakawa wanauabudu na wakawa
wakifanya uchawi. Malaika wakawaambia sisi tunawafundisheni haya kwa ajili ya
kutaka kuwajaribu na kuwajua wale waliona imani ya kurudi kwa Mungu mtukufu na hivyo kujiepusha na uchawi.
Na kutaka kuwatambua wale walioasi na kutumia elimu hii kwa ajili ya kuwadhuru
wengine.
Hapo ndipo watu walikuwa wakijifunza
uchawi za aina zote mbili yaani watu hao walikuwa wakijifunza uchawi uliokuwa
umezuliwa na Shaytani kwa jina la Asif bin Barkhiyyah na elimu waliofundishwa
na Mtume Suleyman a.s. kwa ajili ya kujikinga na uchawi wa aina yoyote. Wao
walikuwa wakijifunza uchawi hata wa kuwatenganisha mume na mke wake na walikuwa
wakiwapatia hasara kubwa sana watu.
Kadiri
ya dini mbalimbali watu wote wanaotumia nguvu hizo za asili katika hali
isiyoruhusiwa na Mungu, wapo kinyume na Mungu Muumbaji wa mbingu na dunia,
hawajui kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa nguvu zote za asili ikiwa ni pamoja na
wanadamu.
Elimu pia
inaweza kusaidia kuondoa imani hizo kwani hata baadhi ya madhehebu ya dini zinachochea
kuziamini imani hizo. wasomi wa karne ya 1- 21 na
zijazo wanapinga na watapinga imani
hizo haramu ambazo zimesababisha na zinasababisha mateso kwa wazee wasio
na hatia hasa vijijini wakishutumiwa
kuwa ni wachawi. Tena kumekuwa na mafarakano na chuki katika
jamii na familia mbalimbali kwa ajili ya imani
ya uchawi; kwa mfano, watu kuuana, kuharibiana mali kwa
kuhisiana uchawi kwa sababu ya watu waliopandikizwa imani za kishirikina.
Serikali ya Tanzania imetumia jitihada zaidi pamoja na kuelimisha wananchi
hasa kutokana na suala la imani potofu na tafsiri mbaya ya uchawi ambayo
imepelekea watu takribani 5000 kupoteza uhai toka
mwaka 1961 kutokana na mateso, kuchomewa nyumba na vibanda katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na mikoa mingine; ni
vilevile katika sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki na ya Kati. Mwaka 2008 raisi wa
Tanzania Jakaya Kikwete alilaani
uchawi kama chanzo cha mauaji ya maalbino 25.
Imani hizo potofu.
share na wengine wafahamu
No comments:
Post a Comment